TAHARIRI: Wabunge msikubali hoja nzito kuzimwa bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAHARIRI: Wabunge msikubali hoja nzito kuzimwa bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 13, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  Wabunge msikubali hoja nzito kuzimwa bungeni

  • Msikubali uhuru wenu wa kikatiba kutekwa nyara na Sitta na Pinda
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, juzi baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, alitangaza uamuzi wa kuzuia kuwasilishwa bungeni hoja binafsi tatu zilizokuwa zimewasilishwa kwake na wabunge.

  Hoja zilizozuiliwa ni pamoja na ya Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa (CHADEMA), iliyotaka maelezo ya serikali kuhusu madai ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, kuingilia mchakato wa utengenezaji wa vitambulisho vya taifa.

  Sitta alisema baada ya kuipeleka hoja hiyo katika Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ambako ilijadiliwa na yeye kupewa ushauri, amekubaliana na ushauri wa kamati hiyo kuwa mchakato wa zabuni hiyo uendelee kwani umeshachelewa.

  Kwamba, baada ya mchakato huo kukamilika na kama kutakuwa na malalamiko kuhusu zabuni hiyo ilivyoendeshwa, jambo hilo linaweza kurejeshwa bungeni na kujadiliwa ili kuona ni nani alikosea.

  Hoja nyingine iliyozuiliwa ni ya Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), iliyotaka kuwepo kwa mabadiliko ya vifungu katika Katiba vitakavyoweka ukomo wa ukubwa wa serikali.

  Alisema hoja hiyo haiwezi kujadiliwa kwa vile inaingiliana na marekebisho ya Katiba, kwamba Ibara ya 98 ya Katiba inaeleza kuwa jambo kama hilo linahitaji kushughulikiwa kwa kuwasilisha muswada bungeni na si kuwasilishwa na mbunge mmoja kama hoja binafsi.

  Aidha, alizuia kuwasilishwa kwa hoja binafsi ya Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee (CHADEMA), iliyohusu mgogoro katika eneo la Chasimba, mkoani Dar es Salaam, na kwa madai kuwa ameridhika kuwa shauri hilo liko mahakamani, hivyo haliwezi kujadiliwa bungeni.

  Wakati huo huo, Spika Sitta alieleza kuwa kutojadiliwa kwa taarifa ya serikali kuhusu suala la Kampuni ya Richmond, uendeshaji usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), na utendaji wa kazi usioridhisha wa Kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) na taarifa kuhusu uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kumetokana na taarifa hizo kuendelea kufanyiwa kazi.

  Tunakukubaliana na maelezo ya Sitta kuhusu kuzuiliwa kwa baadhi ya hoja binafsi, lakini hatuungi mkono sababu alizotoa kuzima hoja binafsi ya Dk. Slaa, na kuzuia kutosomwa kwa taarifa za serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya Bunge, hususan kuhusu Richmond, TRL, TICTS na ATCL.

  Uamuzi wa Sitta kuruhusu kuendelea kwa mchakato wa vitambulisho vya taifa, wakati hoja ya Dk. Slaa ikiwa bado haijawasilishwa bungeni na kudai kukiwa na haja itarejeshwa bungeni, tunaamini kinalenga kuzima uzito na pengine kudhoofisha ushahidi wa hoja hiyo kama si kutoipa nafasi kabisa ya kuwasilishwa bungeni.

  Haituingii akilini, hoja ihusuyo kuingiliwa kwa mchakato wa zabuni ya vitambulisho vya taifa, halafu mchakato huo uruhusiwe kuendelea kabla ya hoja hiyo kujadiliwa, hivi kutakuwa na ushahidi gani mzito wa kuthibitisha kuingiliwa kwa mchakato huo wakati tayari Spika amekwisha kutoa mwanya kwa waliofanya makosa kurekebisha kasoro zao na kufuata taratibu?

  Kwetu sisi, kutojadiliwa kwa hoja hiyo, kutosomwa kwa taarifa za serikali na wabunge kutopewa fursa ya kujadili taarifa za Richmond, uendeshaji mbovu wa TRL, TICTS na ATCL, kunazidi kuahirisha utatuzi wake, ambapo wabunge kama wawakilishi wa wananchi walipaswa kuiona taarifa hiyo, kuijadili na kutoa ufumbuzi badala ya Spika kujiridhisha peke yake.

  Tunawataka wabunge warejee jinsi mjadala wa hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ulivyozimwa kwa sababu zisizo na mashiko, hivyo tunawataka bila kujali itikadi zao, kutumia mwanya mwingine wa kanuni za Bunge kumbana Spika, pale anapochukua maamuzi yasiyofaa.
   
 2. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwani Bunge ni Speaker peke yake? Naomba nieleweshwe.

  Maana kuna haja gani ya vikao vya Bunge endapo Speaker anaweza kupewa taarifa na serikali na kuamua bila kuhusisha wabunge wengine? Kama ni kanuni za Bunge ndivyo zinavyosema, basi nadhani umefika wakati waziangalie kanuni hizo upya. Maana kama Speaker anaweza kuchukua maamuzi bila kutoa fursa kwa Bunge kujadili/kuamua au hata kupendekeza ama kukubaliana kwa pamoja, hiyo hi hatari kwa uongozi wa Bunge letu.

  Nina imani kuwa maamuzi hayo ya kuahirisha kujadiliwa kwa hoja hizo hayawezi kuwa maamuzi ya Bunge kwa kuwa hawakushirikishwa kwa namna yoyote kuyafikia. Hivyo ni maamuzi ya Speaker peke yake.

  Kulikuwa na haja gani ya kuunda kamati ya kusikiliza masuala ya mgogoro wa uingiliaji wa Zabuni ya Vitambulisho vya Taifa kama ilikuwa rahisi kuamua kiasi hicho.

  Wakuu naomba kueleweshwa.
   
 3. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwani Bunge ni Speaker peke yake? Naomba nieleweshwe.

  Maana kuna haja gani ya vikao vya Bunge endapo Speaker anaweza kupewa taarifa na serikali na kuamua bila kuhusisha wabunge wengine? Kama ni kanuni za Bunge ndivyo zinavyosema, basi nadhani umefika wakati waziangalie kanuni hizo upya. Maana kama Speaker anaweza kuchukua maamuzi bila kutoa fursa kwa Bunge kujadili/kuamua au hata kupendekeza ama kukubaliana kwa pamoja, hiyo hi hatari kwa uongozi wa Bunge letu.

  Nina imani kuwa maamuzi hayo ya kuahirisha kujadiliwa kwa hoja hizo hayawezi kuwa maamuzi ya Bunge kwa kuwa hawakushirikishwa kwa namna yoyote kuyafikia. Hivyo ni maamuzi ya Speaker peke yake.

  Kulikuwa na haja gani ya kuunda kamati ya kusikiliza masuala ya mgogoro wa uingiliaji wa Zabuni ya Vitambulisho vya Taifa kama ilikuwa rahisi kuamua kiasi hicho.

  Wakuu naomba kueleweshwa.
   
 4. t

  tk JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ukiangalia namna Bunge linavyoendeshwa, unaona wazi kuwa Speaker au yeyote anayekalia kiti cha Speaker kwa wakati huo, anakuwa na madaraka makubwa mno. Sio tu kuzima kujadiliwa kwa hoja hata kumzima Mbunge kuuliza. Mbunge akionyesha kusisitiza kudai haki yake, anaambiwa kuwa analeta malumbano na Speaker ambalo ni kosa kubwa sana kwa kanuni za sasa.

  Ni ajabu kusikia wabunge wakilalamika kuhusu madaraka makubwa aliyo nayo Rais na kila mara wanazungumzia kumpunguzia madaraka. Mimi nawaomba wabunge kabla hawajafika huko, kwanza wapunguze madaraka ya Speaker.

  Kanuni za sasa zibadilishwe kuwa hoja yeyote iliyojadiliwa na kamati lazima ifikishwe na kujadiliwa na Bunge zima. Pia Mbunge akiwa na Hoja binafsi basi asizuiwe kwa namna yeyote ile kuiwasilisha kwa Kamati na mwishowe Bunge zima.

  Speaker awe kama mwenyekiti kuhakikisha utaratibu unafuatwa na nidhamu inakuwepo. Asigeuke kuwa dikteta anayeamua nani azungumze na nini kizungumzwe.
   
Loading...