TAHAJUDI (Meditation): Mbinu, faida, aina na mambo ya kuzingatia

Habari zenu ndugu,jamaa na marafi. Nimekuja hapa kwa lengo moja tu, ni hivi ni mara nyingi saaana nimekuwa nikisikia hata kusoma maada mbalimbali zinazo husu ""Tahajudi"" nami nimekuwa na shauku ya kutaka kujifunza juu ya haya mambo, Ni ombi langu kwa mwenye kujua namna ya kufanya Tahajudi anifundishe maana nimekuwa nikisikia inafaida nyingi kimwili, kiakili na hata kiroho.Asante
 
Asante sana mkuu kwa hii elimu maana imenisaidia mengi.

Hivi kuna madhara yoyote kama nikivuta marijuana wakati wa zoezi?
Napenda sana wakati wa hili zoezi nivute kwanza sijui kwanini
Kwa upande wangu mm navutaga kwanza kabla sijaanza na huwa inanipa utulivu wa kutosha nikiwa nafanya meditation.
Nb: nadhani hii unategemea na kichwa cha mtu, cha muhimu ni ku-practice na pale utakapoona inakupa utulivu zaidi basi shikilia hapo hapo
 
bigstock-African-American-Woman-Meditat-92821154.jpg


Meditation au taamuli ni kitendo ambacho wengi ambao wamejifunza mambo mengi ya hekima, nguvu ya akili katika maisha ya mwanadamu, sayansi, na Imani mbalimbali, wamekuwa wakivutiwa na kufanya meditation. Mojawapo ya changamoto ya kwanza ambayo wengi wamekuwa wakikutana nayo ni akili kuhama sana kwenye meditation. Kupitia Makala hii, nitajaribu kuelezea njia mbalimbali ambazo unaweza kuzifanya katika kuhakikisha akili inatulia sehemu moja na kuongeza nguvu ya umakini na utambuzi wa hali ya akili yako.

Mwanzo
Meditation au kwa jina la kiswahi Taamuli ni kitendo cha kutazama hali (nature) ya akili na kuongeza utambuzi na umakini. Wengi wanaofanya meditation ni kwa lengo la kuituliza akili kutoka katika stress, msongo wa mawazo, kuongeza hekima, kuongeza umakini na utambuzi juu ya mtu binafsi na jinsi alivyo. Pia wengine hufanya meditation kuachana na addictions na mazoea na kuongeza willi-power. Na wapo wanaofanya meditation kuongeza uwezo wa sheria ya usumaku (law of attraction) na wengine hufanya meditation kuongeza umakini, ubunifu (mfano wachoraji, wanamuziki, wasomi n.k). Kuna sababu nyingi ambazo kila mtu binafsi anaamua kufanya meditation.

Akili ni kitu ambacho ni kitu Tata sana (very complex). Ni sehemu ya mwanadamu ambayo haijagunduliwa vyema jinsi ifanyavyo kazi na hakuna mtu anayeweza kukusaidia kufikiri au kujua jinsi akili yako ifanyavyo kazi. Mara nyingi tumekuwa watumwa wa akili zetu bila kutambua kuwa tunaweza kutawala akili zetu na kuamuru akili iwaze nini, isiwaze chochote au kuamua kuweka umakini katika jambo Fulani kwa jinsi utakavyo wewe. Akili ukiweza kuiongoza utakusaidia lakini ukishindwa utakuwa mtumwa wake utakuwa mtumwa daima. Ndipo utakuta hali kama addictions, mazoea mabaya, umakini, hekima na uvumilivu tunashindwa kuwa navyo kwa sababu hatuwezi kutumia akili zetu ipasavyo.

Tatizo linalosababisha akili kutotulia
Kwa kawaida tangu unapoamka na mpaka unapoenda kulala akili inafanya kazi. Kila wakati utawaza hichi, kisha utawaza kingine, na ukitaka kujua hilo chukua kalamu na karatasi na saa. Andika kwenye karatasi kila kitu au wazo au hisia itakayopita akilini. Mfano ukiwaza kuhusu kazini andika kwenye karatasi “kazini”, ukimuwaza mtu andika jina lake, andika kwa ufupi ili upate muda wa kuandika. Hakikisha umeandika kila kitu na kisha baada ya dakika kumi utaona ni mawazo au hisia nyingi zimepita akili. Huo ni mfano tu kuwa kwa kawaida akili huwa haitulii. Itawaza hichi, itakumbuka ya jana, utakuwa na hisia Fulani, na kila hali inakuja na kupita. Ndivyo tulivyozoea maishani.

Meditation na Akili.
Kwenye meditation unajifunza kuitawala na kuingoza akili kwa dakika Fulani. Mfano meditation ya Samadhi Meditation ambayo unaiweka akili katika umakini mmoja tu; ni kitendo cha kuelekeza akili katika jambo moja au kitu kimoja mfano kwenye pumzi tu. Kila saa na kila dakika tunapumua, lakini hatuweki akili zetu kwenye pumzi kwa sababu haina umuhimu kutazama pumzi kila saa. Hivyo meditation ya kuongoza akili inatumia pumzi kwa sababu ni hali ambayo wakati wote tunayo, haiitaji kuwasha mshumaa au kutazama kitu Fulani. Kuweka akili kwenye pumzi ni cheap/rahisi na haiitaji chochote. Ni mtu tu mwenyewe kutumia pumzi na kujaribu kuiweka akili sehemu moja kwa dakika chache. Unaweza kufanya meditation kwa kuweka akili yako kwenye mshumaa, kutazama bahari, kutazama chochote unachokiamini n.k. Kwa hapa leo nitazungumzia kuitawala akili kwenye pumzi.

Ukiwa unafanya meditation
Ukiwa unafanya meditation unakaa mkao ambao utakuwa huru na utaweza kukaa kwa dakika chache bila kuhama. Unaweza kukaa kwenye kiti lakini usilale kwa sababu unaweza ukasinzia kutokana na uvivu. Pia kama unaweza kukunja miguu kwa muda mrefu pia unaweza kukaa vizuri chini, juu ta mto au kitu ambacho kitaepusha maumivu ukikaa sakafuni.

Ukianza hakikisha hutasumbuliwa na utapata muda wa dakika chache kukaa peke yako. Pia unaweza kufanya meditation na wengine kwa kukaa pamoja na kila mmoja kuangalia upande wake (ili kuwa na concentration/umakini). Kwa wanaoanza tumia dakika 10. Kila wiki unaweza kuongeza dakika 5 mfano 15, halafu wiki ijayo ukajifunza 20 na kisha zoea kutawala akili kwa dakika 20 kila siku ndani ya mwezi mmoja na baadae unaweza kutumia 30 mpaka 40, sio lazima uzidi 40, cha msingi sio dakika ni umakini ndio uongeze. chukua saa au simu ikukumbushe dakika kumi zikifika. Hakikisha umeweka simu silent, na ukiwa kwenye meditation usiangalie zimebaki dakika ngapi, dedicate kuwa na subira mpaka muda utimie.

Ukianza weka akili kwenye pumzi, vuta pumzi taratibu na weka break kisha toa pumzi taratibu. Yaani unavuta pumzi, unakaa kidooogo kisha unaitoa taaratibu huku ukitazama jinsi hewa inavyoingia puani na kifua kikitanuka na hewa ikitoka na kifua kikishuka taaratibu. Ukigundua akili haipo tena kwenye pumzi usijali wala usijilaumu au kuona umekosea, ni kitendo cha kawaida akili kuhama bila kujijua. Cha msingi irudishe tena akili kwenye pumzi kama mwazoni. Endelea hivyo hivyo. Akili ikihama unairudisha kwenye pumzi. Ukiona kama unarelax na unahisi mwili umetulia sana huwa kuna kama raha Fulani unaihisi au umeme/waves Fulani ya relaxation unaiona unakuzunguka achana nayo na usiweke akili kwenye raha inayokujia ukiwa unafanya meditation wewe endelea kuweka akili kwenye pumzi na ile raha itaendelea kuwepo. Ukiiwaza utapotea, ni kama mtego.

Akili ikiwa haitulii.
Samahani kwa kuanza kuelezea mengi kwa sababu hapa ndipo kwenye mada kuu. Nilipenda kutoa introduction kwa ambao hawajui ili wafahamu na tuende sawa.

Akili huwa kwa mara ya kwanza kufanya meditation inahama sana. Sio tatizo ni hali ya kawaida. Ni udhibitisho kuwa akili inahitaji kutulizwa. Kuna njia mbalimbali ambazo unaweza kufanya. Unaweza kuhesabu pumzi inapoingia. Ukahesabu Moja….mbili…tatu na kufika kumi kisha rudi tisa, nane, saba, sita….. mpaka sifuri kisha anza tena moja, mbili…na kuendelea.

Njia nyingine, ukiona akili inahama, mfano unawaza kuhusu jambo Fulani, sema kwa taratibu “akili najua unawaza kuhusu masuala ya kazini, rudi kwenye pumzi”. Kusema hivyo sio kwamba unaongea na akili bali inakupa mazoea ya kujua kinachoendelea akili na kukifanyia maamuzi. Ukiona unawaza kuhusu kitu Fulani mfano pesa zako ulipoziweka sema “akili najua unawaza pesa zangu, rudi kwenye pumzi” kisha endelea kuweka umakini kwenye pumzi.

Baada ya kufanya meditation mara kwa mara utaona kuhama kwa akili kumepungua na unaanza kuona raha kufanya meditation. Pia baada ya meditation utakuwa unahisi Amani na kama ulikuwa umeshusha mzigo mzito akilini. Pia katika maisha utakuwa makini na kinachoendelea akilini mwako na kukusaidia kujitambua vyema.

Asante.


Haya ndo mambo sasa,twende kazi,siyo kila tukifungua jf tunakutana na siasa na lawama tu.bora tuwe tunajifunza mambo mengine
 
Kwenye meditation kutumia kitu kama marijuana ilihali kikiwa kinakusaidia kufikia hali ya self mastery inaruhusiwa. Hasa wale wanaohitaji ku aweken kundalini.
 
Asante sana mkuu kwa hii elimu maana imenisaidia mengi.

Hivi kuna madhara yoyote kama nikivuta marijuana wakati wa zoezi?
Napenda sana wakati wa hili zoezi nivute kwanza sijui kwanini

Dont. Usitumie kilevi cha aina yoyote katika meditation na hakikisha muda mrefu umepiga kama zaidi ya 3 hours hujatumia kilevi chochote.

Meditation inatumika kuiongoza akili. Sio tu kwenye msongo wa mawazo au stress bali hata katika addictions na mashikilio ya raha zitokanazo na vilevi katika kuitafuta furaha.
 
Kwa upande wangu mm navutaga kwanza kabla sijaanza na huwa inanipa utulivu wa kutosha nikiwa nafanya meditation.
Nb: nadhani hii unategemea na kichwa cha mtu, cha muhimu ni ku-practice na pale utakapoona inakupa utulivu zaidi basi shikilia hapo hapo

Hata mimi ndio hivo

Kwenye meditation kutumia kitu kama marijuana ilihali kikiwa kinakusaidia kufikia hali ya self mastery inaruhusiwa. Hasa wale wanaohitaji ku aweken kundalini.

Kufanya meditation kwa kilevi chochote ni kosa na haina progress yoyote. Naturally akili haiitaji substance kutoka nje yako ili uamke au kuamsha kundalini au chakras za kufunuliwa ufahamu. Naturally akili inaweza kufikia hekima ya juu bila kutumia substances yoyote kutoka nje.

Mojawapo ya lengo la meditation ni kujifunza kuidhibiti akili, kuongeza hekima, kuacha addictions na mazoea na pia lengo kuu ni kujifunza kuitafuta furaha bila kutumia milango ya ufahamu. Mara nyingi wanadamu tunatafuta furaha nje yetu kwa kutumia substances ambazo zinatufanya tuwe tegemezi ili kuipata hali fulani au raha fulani.

Meditation inakata hiyo mizizi na kukufunulia happiness within.
 
Kufanya meditation kwa kilevi chochote ni kosa na haina progress yoyote. Naturally akili haiitaji substance kutoka nje yako ili uamke au kuamsha kundalini au chakras za kufunuliwa ufahamu. Naturally akili inaweza kufikia hekima ya juu bila kutumia substances yoyote kutoka nje.

Mojawapo ya lengo la meditation ni kujifunza kuidhibiti akili, kuongeza hekima, kuacha addictions na mazoea na pia lengo kuu ni kujifunza kuitafuta furaha bila kutumia milango ya ufahamu. Mara nyingi wanadamu tunatafuta furaha nje yetu kwa kutumia substances ambazo zinatufanya tuwe tegemezi ili kuipata hali fulani au raha fulani.

Meditation inakata hiyo mizizi na kukufunulia happiness within.
Asante Mkuu,

Napenda kuuliza pia vipi kuhusu usaidizi wa music [kwa kutumia earphones], Je nako huko ni external influence. Maana mimi hua napata urahisi sana napoweka earphones.
 
Asante Mkuu,

Napenda kuuliza pia vipi kuhusu usaidizi wa music [kwa kutumia earphones], Je nako huko ni external influence. Maana mimi hua napata urahisi sana napoweka earphones.

Hapo kale takribani miaka 7000 iliyopita meditation ilikuwa inafanywa bila kutumia kifaa chochote cha mziki kwa sababu teknolojia haikwepo kama hivi sasa.

Aina ya music iliyokuwa inatumika katika meditation ilikuwa ni kengele ndogo ambayo ilikuwa inapigwa kwa utaratibu maalum na mtu anayefundishwa concentration anaelekeza akili yake kusikia sauti ya kengele ikipigwa na kufuata sauti yake mpaka inapoisha. Kengele inapigwa mara tatu wakati wa kuanza meditation na mara tatu wakati wa kumaliza meditation, ni kama kuandaa akili.

Hivi sasa mabadiliko ya technolojia na uwepo wa watu mbalimbali wanaojitokeza kufundisha meditation wanatoa CD au Audio guides na wengine wanauza kama sehemu ya biashara.

Kwa upande wa wanaofanya meditation toka miaka ya zamani, mpaka leo hawatumii muziki au chombo chochote katika kutumia kufanya meditation.

WHY? kwa sababu my dear friend, mind is a very tricky attribute. Muda mwingi milango yako ya ufahamu inafanya kazi. Macho, masikio, ulimi, pua, na ngozi kila saa tunavitumia kupata taarifa ya nini kinachoendelea nje yetu. Katika meditation una Switch Off milango ya ufahamu na kubakia na akili yako tu. Hii inakusaidia kuitambua nature ya akili yako na wewe binafsi na pia kutenganisha mazoea ya ku define happiness kutoka nje yako.

Hivyo kutumia audio music (relaxation music, new age music) bado hujafunga milango ya ufahamu (sikio) na sometimes kuna hali ya akili kutengeneza hali ya kufikirika kupitia music inayoplay background. Unaweza kulifahamu hilo ukiwa umejaribu kumeditate kwa muda mrefu na audio book.

SO: Njia nzuri fanya meditation bila support yoyote, funga milango ya ufahamu na hakikisha akili ipo timamu na haijaathiriwa na kilevi chochote. Face happiness within bila support kutoka nje yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom