Tahadharini na wafanyakazi wa ndani,H/G! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadharini na wafanyakazi wa ndani,H/G!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by LiverpoolFC, Jul 17, 2012.

 1. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ninaishi Arusha mtaa wa Ilkiurei,Mfanyakazi mmoja wa ndani hapa mtaani kwangu amekamtwa usiku wa leo majira ya saa saba na dk 40 akiwanga ndani ya nyumba anayofanya kazi kama H/G!

  Alikamatwa akiwa kama alivyozaliwa toka tumboni mwa mamaye na akiwa ameshafungua kila mlango wa vyumba na hata baadhi ya watu wakikoroma bila ya kujijua kama vyumba vyao vimefunguliwaje.

  Na baada ya zoezi lake hilo kwa H/G huyo halijaisha,na ndipo Mama mwenye nyumba akawa amezinduka na kukuta chumba chake kiko wazi na ndipo akaanza zoezi la kutaka kujua nani amefungua,Na alipoukaribia chumba pili nayo wazi,kwenda kwa watoto nako kiko wazi na kuangalia mlango kuu nalo lipo wazi na ndipo alipoangalia sebuleni akaona mtu yuko uchi wa mnyama na kumhamki ni mfanyakazi wake wa ndani!

  Na ndipo Mama akaanza mayowe na watu wengine wakadamka na hawakuamini walipomwona anayetenda haya yote ni mfanyakazi wa ndani!

  H/G huyo alianza kubwabwaja kwa kuropoka kwa lugha mbalimbali ya kwmb yeye ni anatumika kuzimu na ndipo yowe zilizidi na hata majirani wakatokeza na nipo Mpaka mafuta wa MUNGU aliyekuwa jirani akadamka na kushusha Neno la MUNGU na akivunja nguvu ya mwovu shetani na ndipo huyo mfanyakazi akaendelea kusema mengi na baadae akazimia na mpaka natoka majira ya saa tisa alikuwa hajazinduka tu na hbr nilizopata muda si mrefu ni kwmb amezinduka na yule mpaka mafuta wa MUNGU amerudi pale na akaimarisha Neno lake Mungu katika makazi hayo ambao watu walikuwa wamepungukiwa na Neno la Mungu!

  TAHADHARI:

  Ndg zanguni tuweni makini sana na wafanyakazi wa nyumbani kwn wengi wao wamezidi kuwa ni mawakala wa kuzimu na hasa kwa upande wa watoto wa kike na sijajua ni kwnn haya yanawakumba wao sana!

  Huyo mtoto ameongea mengi sana kuhusu wanavyotumika ktk ulimwengu wa nguvu za giza.

  Ni hayo tu yaliyojiri night hii hapa mtaani kwangu na nikapenda niwajuze wadau wa JF!

  Nawasilisha!
   
 2. Little Angel

  Little Angel JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mh,inatisha sana,Mungu atusaidie maana kwa macho ya kibinadamu huwezi jua isipokuwa kwa nguvu za Mungu tu.

  poleni sana,sasa ikawaje kuna yoyote mabaya yenye madhara amekwishawafanyia so far?
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hawa ma-HG ni janga kwa kweli....
   
 4. l

  lasix JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Dah inaogopesha hasa ukizingatia hawa watu tunawahitaji majumbani mwetu na huwezi kumgundua kwa kumwangalia.ni jambo zito hasa kwa sisi wenye watoto wadogo
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli ameng'ang'ana ya kwmb ndiyo kazi yake ktk anga hii anayoishi.

  Ameongea mengi sana hasa akisimamia anavyotumika nyakati yote hapo kuzimu na hata anavyosababisha ajali na kuua watu wasio na hatia kwani kule wanapoishi wanakunywaga damu za watu kila siku.

  Asubuhi amepumzika ila mtumishi huyu wa Mungu amedamkia naye hapa akimwaga injili balaa na hata huyo H/G ameshatadharisha kitambo ya kwmb hawaogopi chochote zaidi ya wokovu tu!

  Ntarudi na mengi aliyoyasema kwani hakika tusipokuwa na Imani tutadidimizwa na mwovu shetani!
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,208
  Likes Received: 3,773
  Trophy Points: 280
  Poleni sana!
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  mahouse girlni headache jamani....... Ukimpata mzuri unashukuru...

  Halafu hata uwape nini kazi bure....
   
 8. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Yani wanakatisha tamaa jamani!
  Nafikiri ungekuwepo leo umwone alivyo huyo dada hakika utakata tamaa kbs ya kuwatumia hata nyumbani!
   
 9. N

  Nndu wa Selote JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 341
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Ndugu Liverpool,

  Hii taarifa yako inaonekana ina mapungufu makubwa-kama ya kutunga vile!!! Je housegirl zaidi ya kukutwa akiwa uchi sebuleni alikuwa akifanya nini? Nina maana ni kitu gani kilifanya wenye nyumba waseme anawanga? Je, haiwezekani kwamba alikuwa kwenye ndoto? Suala la kuwa uchi inawezekana alilala bila nguo na alioanza kuota akaamka na kutoka kama alivyokutwa. Je ni madhara gani aliyoleta zaidi ya hadithi za milango kukutwa wazi? Je kukutwa kwa huyo Housegirl ambaye mwandishi wa habari hii hautueleza hata hicho alichokuwa akibwabwaja, inatosha kutuambia tujiadhari na wasichana wa kazi za ndani????
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Thankx Best!
   
 11. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Watu wengi huwa nyanyapaa watumishi hawa,
  na kuwafanya second class citizen.
  Kuna wenye nyumba ambao huwageuza nyumba ndogo,
  tena kwa kuwabaka.
  Huwafanyisha kazi masaa 24.
  Hakuna mikataba,
  siku zote hupunjwa ujira.
   
 12. sister

  sister JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,026
  Likes Received: 3,932
  Trophy Points: 280
  kuna nyumba fulani walikuwa wanalishwa nyama za watu bila kujua..........siku moja yule mama akamleta mchungaji nyumbani kwake H/G wacha apandishe na kuanza kutoa siri.

  mimi nadhani ukimpata tu H/G unamwitia mchungaji au unampeleka kanisani akaombewe mana ni hatari................na tuwe na utaratibu wa kusali usiku majumbani kwetu na kama unaweza mwagia nyumba yako kwa maji ya baraka kabla ya kulala unapita kila chumba unamwagia maji ya baraka na kusali.
   
 13. sister

  sister JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,026
  Likes Received: 3,932
  Trophy Points: 280
  ni kweli baadhi ya familia zinatesa H/G tena sa nyingine mama ndo anakuwa mtesaji mkuu.........
  watu wanathamini chakula........H/G anakula mabaki ya chakula, anafua nguo za watu wote nyumba nzima.........kazi zote anafanya yeye wakati hyo familia ina watoto wakubwa ambao wote wanaweza kujifulia nguo zao na kufanya kazi za nyumbani.

  nasi tujitahidi kuwapenda H/G ishi naye kama ndugu mana ameshika dhamana ya uhai wetu majumbani.........kumbuka yeye anaandaa chakula anaweza kuwawekea sumu mkafa wote.
   
 14. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red mpaka mwili wangu umetetemeka.Unaweza kusifia nyama ya leo tamu sana, kumbe bonge la maiti ya ajali.Eeeh Mungu tusaidie!
   
 15. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Yuko MH mmoja aliwahi kuwa waziri enzi za Mwalimu,
  Ma HG wake wote ambao ni 5 amewasomesha mpaka kidato cha 6

  Si hivyo,
  Enzi hizo miaka ya 90 alikuwa akiwapa Tsh25,000 wakati wengine wakilipa 2000.
  Zaidi ya hapo alihakikisha kila mwezi anaweka 10,000 ili akifanya kazi miaka 3 mfululizo anaanza shule kama binti yake.

  Watu wengi walimwona falla mkubwa.

  Leo hii wale Ma HG wana kazi zao nzuri kabisa,
  huenda kwake wakati wa likizo,
  Ni bint zake nao wanamwona ni baba yao.

  Mabinti 4 ni Wahehe 1 ni mrangi

  inataka moyo lakini.
   
 16. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Nndu wa Selote!
  Pole sana kama unaona ina mapungufu na inaweza ikawa wewe mwenyewe una mapungufu ya uelewa kwn karibia member wote wamenisoma vema kbs.

  Wewe pekee ndio umekuwa tofauti nao na ni dhahiri kbs ya kwmb napata hofu na uelewa wako!

  Hv wewe siyo mmoja ya wanafamilia ya Selote wale ninaowajua kweli?

  Pole sana! H/G ameongea kana kwmb ungekuwepo na una familia usingetamani hw wafanyakazi!
   
 17. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Nimeipenda hii!
   
 18. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kwa uwezo wetu wa kibinadamu siyo rahisi kujua mapema tabia ya HG.Kumshirikisha Mungu ni jambo muhimu sana na isichukuliwe kwamba ma-HG wote ni wabaya maana hizo ni tabia binafsi za mtu mwenyewe,ndiyo maana unaweza pata mwenye tabia za kichawi kama huyo,mwongo,mwizi,malaya au mzuri mwenye tabia ya kuigwa.
   
 19. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Nundu wa Selote ana point.
  Kuna kitu inaitwa sleep Walk ni ugonjwa.

  Mtu anaamka usiku,
  anafungua jokofu,
  anachua misosi anapasha moto,
  anakaa na kula,
  hali yupo usingizini.

  Ukimshitua unaweza kumpeleka katika shock,
  na brain ikashindwa kufanya kazi vizuri kwa muda.

  Kitaalamu ugonjwa upo.

  Hata hivyo sipingi madai kwamba,
  ana nguvu nyingine kutoka katika dunia ya roho.

   
 20. pinkmousse

  pinkmousse JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni case ya tatu naisikia kutoka Arusha, dada yangu anaishi huko jirani zake wawili wamekutwa na issue kama hizo mwezi uliopita,mmoja baada ya kuombewa ameamua kuondoka kwa sababu anasema hiyo nyumba wanasali sana na kusikiliza safina radio kila wakati hawezi kuishi mazingira hayo.
   
Loading...