Tahadhari yatolewa juu ya ongezeko la maji Ziwa Victoria

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
external-content.duckduckgo.com.jpg

Bodi ya maji bonde la Ziwa Victoria imewatahadharisha watumiaji wa maji katika ziwa hilo wakiwemo wavuvi pamoja na watumiaji wa vyombo vya usafiri katika Ziwa Victoria juu ya athari zinazoweza kujitokeza kufuatia ongozeko la usawa wa maji ziwani humo kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

Tahadhari hiyo imetolewa na mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la Ziwa Victoria Mhandisi Florence Mahay ambapo amesema kuwa usawa wa maji katika ziwa hilo umeongezeka mpaka kufikia 1134.22 mamsl, ikiwa ni tofauti ya sentimeta tano ukilinganishwa na usawa wa juu zaidi kuwahi kufikiwa ambao ulikuwa 1134.27 kwa kipimo hicho kwa mwaka 1965.

Aidha Mhandisi Florence amesema kutokana na hali ya hewa katika bonde hilo kipindi cha masika huwa mwezi wa april mpaka mwezi mei hivyo kuna uwezekano wa usawa wa maji katika bonde hilo kuongezeka Zaidi.

Bodi ya maji bonde la Ziwa Victoria imekuwa ikifuatilia usawa wa maji wa Ziwa Victoria kwa muda wa takribani miaka 56 mpaka sasa kuanzia mwaka 1964 ambapo kumbukumbu ya taarifa za bodi hiyo zinaonyesha mwaka 2006 ndio mwaka uliokuwa na usawa wa chini kabisa kuwahi kufikiwa kwa kuwa na usawa wa 1131.87.

Chanzo: ITV
 
Hivi kuongezeka kwa maji kwenye water bodies kunaweza kusababisha madhala gani kwa binadamu especially watumiaji na wenye vyombo vya usafiri majini?
 
beth, Unfortunately, bad politics is now taking lead in every major sector in our country and this will exacerbate unsound effects of the community development total outcomes... Very bad..
 
Kweli kabisa.. Vibandari vidogo navyo vimefunikwa na maji. Mfano pale sweya karibu na ofisi ya mtaa
N.B pia magugu maji ni mengi sanaa na ni hatari kwa kuficha mamba na nyoka
 
Yakiongezeka maji kuna madhara yepi??watueleze mbali na majengo ya Malaika hotel kumezwa na ziwa,nini kitatokea
Uhaba wa samaki??
Ajali kwa vyombo vya ziwani??
Maji si yanapungua kuelekea Nile??
Mafuriko huko Ethiopia na Misri....


Everyday is Saturday.............. :cool:
 
Back
Top Bottom