Tahadhari ya mawimbi yaliyoko maeneo ya Ofisi za Azam Tazara kwa wenye gari zenye sensor

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Kwa yeyote anaetumia Gari isiyo nafunguo ya kawaida kwa maana zile zenye kutumia ki remote sensor kwa kuwasha gari na milango, unapoenda office za Azam Tazara hakikisha usizime gari yako mpaka ikibidi umalize shughuli zako mle ndani kama utaizima hiyo gari elewa kuwa haitowaka!

Kitakachofanyika utasukumwa na vijana waliopo eneo Hilo ambao ni wazoefu wa tatizo then gari itawekwa free na kusukumwa umbali wa mita kama 70 hivi au 100 huko ndio itawaka
Ushauri kama unakwenda pale Park gari yako umbali wa hata Mata Mia, na Pia hata ukiwa katika foleni ya kwenda mjini maeneo hayo sikushauri uzime gari( yaani hizi gari zakutumia start button/Remote control badala ya funguo)

Na Mwisho niwaombe uongozi wa Jengo hilo la Azam customer support kuangalia upya mfumo wa hiyo mionzi iliyotandazwa hapo kwani inaleta usumbufu mkubwa kwetu sisi wateja wenu ikizingatiwa hapo hakuna bango lolote linalotahadharisha mteja juu ya jambo Hilo.
 
Wazee wa mionzi kitaifa walione hili kabla ya janga kutokea
 
Back
Top Bottom