Tahadhari ya COVID--19,Mtaani watu hawachukui tahadhari yoyote huku vifaa vya kunawia vimewekwa ili kuhadaa mamlaka

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,857
49,553
Poleni na harakati za kukabiliana na Covid19

Kusema ukweli hali ya maisha mitaani hasa huku niliko,i mean mkoani hakuna tahadhari yoyote ya maana watu wanachukua,mikusanyiko iko palepale na shughuli zinaenda kana kwamba hakuna hatari yoyote.

Vifaa vya kusafisha mikono vimewekwa na watu ili kuhadaa mamlaka wasilipe faini,mara nyingi havina maji na hata vikiwa na maji watu hawanawi yaani kiufupi kuna kupuuzia na kuchoka kwa watu.Hata wenye mamlaka kama serikali haitoi msisitizo wowote na kufanya doria ,vyomba vya manispaa vimewekwa maeneo kadhaa kama masoko nk lakini hakuna wa kumsisitiza mtu anawe,hivyo hivyo na kwa wafanyabiashara.

Kwa kweli covid 19 ni ana tu spare tu vinginevyo.........!! Shime serikali ikazie watu kuchukua tahadhari kwa kufanya doria na ambush za mara kwa mara na ikiwezekana wawatoze faini watu au watoa huduma kama maduka nk wasiowasisitiza wateja kunawa..Kwa ugonjwa wa mlipuko kama huu haina maana kwa watu wachache kuchukua tahadhari wakati wengine hawachukui tahadhari yoyote inakuwa ni kupoteza mta,italeta maana kama tu kila mtu atatimiza wajibu wake la sivyo serikali ilazimishe watu kufuata taratibu zilizowekwa kama kwingine.

Tuacheni mzaha jamani Covid 19 ni noma sana
 
Back
Top Bottom