TAHADHARI: Waziri Wa Afya Ummy Mwalimu ashauri Watanzania waache utaratibu wa kusalimiana na kukumbatiana

Nadhani tatizo tulilonalo kwa sasa si la kusalimiana kwa mikono na kukumbatiana. Tatizo lililopo ni je tumejipanga vipi kuzuia kuingia kwa virusi hivyo hapa Tanzania? Je tunazo maabara za kuthibitisha pasi na shaka kwamba mgonjwa husika anayo au hana maradhi hayo tena kwa muda mfupi. Je tunaweza kuzuia kuingia kwa maradhi hayo katika mipaka yetu au katika viwanja vyetu vya ndege. Je tunavyo vifaa vya kuwatambua wasafiri ambao wamekwisha athirika na gonjwa hili katika vituo vya kuingia nchini? Hayo ndio masuala ya kuzungumzia kwa sasa. Ukianza kuzungumzia kusalimiana kwa mikono na kukumbatiana moja kwa moja unakuwa unazungumzia njia za kujikinga ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa ambao tayari upo. Kwa sasa bado conovirus haijatufikia, hivyo tujikite zaidi katika kuzuia uingiaji wake hapa nchini kwetu.
 
Back
Top Bottom