TAHADHARI: Waziri Wa Afya Ummy Mwalimu ashauri Watanzania waache utaratibu wa kusalimiana na kukumbatiana

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,755
2,000
“Katika kipindi hiki cha tishio la virusi vya corona nawataka Wananchi wajizuie kabisa kupeana mikono.

kukumbatiana na kupeana mabusu, najua ni ngumu hii kwa Watanzania lakini tujitahidi ili kujiepusha na kuwaepusha wenzetu na maambukizi”- WAZIRI UMMY

“Njia kuu za kuambukizana corona zinatoka kwenye majimaji, kwahiyo unavyombusu, kumkumbatia au kumshika mkono mwenzio unamuweka kwenye hatari.

na kama utampa mkono haraka kanawe maji, kwa kipindi hiki tusalimiane hata kwa ishara na usipopewa mkono usinune” -WAZIRI UMMY MWALIMU
1582975399657.png

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
1,670
2,000
Kwenye mwendokas kule ni zaid ya kukumbatiana kule ni nyama kwa nyama na madungadunga aka gropers ule usafir ni janga lingine nadhan william gates alikua sahihi kusema hii ngoma ikitimba africa itakua massacre God forbid
 
Percy

JF-Expert Member
Jul 21, 2014
5,209
2,000
Sasa kwenye mwendokasi watu wanagusanisha nyama kwa nyama, mtu shazi, tutapona kweli? Alafu kauli yake inaonyesha mzigo ushaingia TZ wachache sana watamuelewa. Ngoja nkanunue Mask mapemaa.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
2,830
2,000
“Katika kipindi hiki cha tishio la virusi vya corona nawataka Wananchi wajizuie kabisa kupeana mikono.

kukumbatiana na kupeana mabusu, najua ni ngumu hii kwa Watanzania lakini tujitahidi ili kujiepusha na kuwaepusha wenzetu na maambukizi”- WAZIRI UMMY

“Njia kuu za kuambukizana corona zinatoka kwenye majimaji, kwahiyo unavyombusu, kumkumbatia au kumshika mkono mwenzio unamuweka kwenye hatari.

na kama utampa mkono haraka kanawe maji, kwa kipindi hiki tusalimiane hata kwa ishara na usipopewa mkono usinune” -WAZIRI UMMY MWALIMU

Sent using Jamii Forums mobile app
Huku ni jiji mwambafy tu. Hakuna ajuaye fika unasambaa vipi.

It is just a matter of time. Si kwenye dala dala wala magogoni. Ule muda wa kutuvuruga ni sasa. Kina Azory, na wengine huruma ilitutoka. Sasa zamu yetu sasa. Malipo yote ni hapa hapa.

God forgive us.
 
Top Bottom