Tahadhari: 'Wamasai' eneo la maegesho la Mlimani City Mall | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari: 'Wamasai' eneo la maegesho la Mlimani City Mall

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SMU, Apr 20, 2011.

 1. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Tofauti na ilivyokuwa mwanzoni, katika siku za hivi karibuni nimeanza kuona wamasai (au pengine niseme vijana wa kiume waliovalia lubega!) wakizunguka huku na kule kutafuta wateja wa 'biashara zao' katika eneo la kuegeshea magari la Mlimani City Mall. Inawezekana pengine wamewekwa hapa kwa ajili ya ulinzi lakini wameamua kufanya biashara pia!

  Vijana hawa mara nyingi wanavizia mtu anapopaki na kuanza kuteremka kutoka kwenye gari au wakati mtu anaporejea kwenye gari lake kutaka kuondoka na hapo humfuata na kuanza kumshawishi kuhusiana na bidhaa wanazouza (aghalabu wanauza dawa za mitishamba).

  Lakini hivi majuzi nilistushwa na mmoja wao. Alinambia anauza laptop kwa bei poa! Hili lilinistua kwa sababu siyo la kawaida kwa aina hii ya wafanya biashara na hasa uzoefu wa kiusalama katika eneo la mlimani city. Sikutaka kuendelea kumsikiliza kwa sababu sikuwa na nia ya kununua laptop na pia sikupenda namna alivyonisogelea mlangoni mwa gari wakati nateremka.

  Si vibaya ndugu zangu mkachukua tahadhari zaidi juu ya mali zenu na pia usalama wenu mnapokwenda Mlimani City (hasa kwa magari). Kuna hatari nyingi naziona kwanza kwa wao kufanya biashara eneo hilo, namna wanavyofanya biashara (wanakuja mlangoni mwa gari kabisa) na pengine hata aina ya biashara wanayoifanya.
   
 2. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Duh! mlinzi wa kimasai na laptop ? hiyo itakuwa imeibiwa hapohapo.
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Na mimi nilihisi hivyo!
   
 4. D

  DURACEF JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  La kini pia kwanini wawa2mie walinzi wa kimasai katika eneo zuri na lenye hadhi kama hilo? wa2 wawe serious vinginevyo hali itakuwa mbaya sana.
   
 5. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Hao wamasai ni kikundi cha wezi wana dawa za kunusisha ukiwaentertain unazimika wanakukomba..ni wajanja sana wanatumia lubega kufool usigundue kuwa ni wajanja..na si wamasai tu pia kuna wahindi wanazunguka usiku na simu wanajifanya wanauza wamepata emergency kumbe wanauza mafake ya china
   
 6. U

  Uswe JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  sidhani kama ni walinzi wa mlc hawa wanaingia tu kutoka nnnje ila wamegeuza mlc kama kijiwe chao wanapiga bao na kuuza hapo hapo.

  lakizi waTZ tujilaumu wenyewe, kama tusingekua tunanunua vitu vye wizi hali hii ingepungua, laptop hata iwe nzuri kiasi gani kama huitumii haina value kwako, na ni wazi wengi wanaoziiba hawazitumii, ila kwa sababu waTZ tunanunua vitu vya wizi ndio maana tunaendelea kuibiwa

  Saidia kupunguza wizi, Acha kununua mali za wizi!
   
 7. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  bongo bongo dar es salaam!kila kitu ni hatari sasa hivi sijui tutafika wapi,hakuna kitu nakichukia kama unafika mahali unapark kabla ujashuka tayari kuna mtu mlangoni,huwanachukia ile mbaya
   
 8. n

  ngwini JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kaka tena wanakuwa kwenye gari lao hao wahindi,maana kuna cku natoka kwenye hle Atm ya nje ya Nmb naona gari linacmama mguuni na jamaa wa kihindi ananionyesha cmu anadai ana emergency anauza! Tuwe makini
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  asanteni,dah
   
 10. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  siku hizi mtu yeyote anaweza kuvaa kimasai, muwe makini mashuka yamejaa kila kona
   
 11. g

  gepema Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kwakweli tupo nyikani kama nchi maana kila mtu na kila kitu na lwake,sijui mwisho ni nini kama tukiendelea hivi
   
 12. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenifumbua macho,juzi kati kuna mhindi bonge fulani alitaka niuzia Nokia N97 kwa 170,000 bahati yangu sikuwa na cash,kumbe ningelizwa!!!
   
 13. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Pole Sugar wa ukweli...mjini hakuna mashamba
   
 14. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Mkuu ile ni kazi kabisa na wamejipanga,ni kama wale wanaospray vioo na kuvunja wanakuwa na gari wanaegesha ubavuni mwako halafu mmoja anakufuatilia unapoenda ili ukitaka a kurudi anawabeep wenzie
  wanafanya fasta kiasi hata walinzi hawastukii issueM
   
Loading...