Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Habari,
Mzani ukisoma pungufu ya kilo tatu na ushee.
Kwa wale wakaazi wa Dar ambao hupata kitoweo chao kwenye bucha za Mwenge kuanzia leo mtakapoona huu uzi kuweni makini. Wauzaji wa nyama bucha zile wamekuwa wakiwauzia nyama pungufu wateja kutokana na kilograms unazonunua.
Mimi nimekuwa mhanga wa wizi huu zaidi ya MARA 11 kwa muda tofauti tofauti nikitumia Bucha tatu za Mkulima na za pembeni kulia na kushoto kwa mkulima.
Mara ya kwanza kilo 10 walinipiga kilo 2.5
Mara ya pili kwa kilo 12 wakapiga 3.
Mara baada ya hapo nikajenga urafiki na muuza samaki duka la mwisho kama unakunja kona ya msikitini, kila nikinunua nyama naenda kwake kuhakiki na mara zote nakuta nimepigwa nyama.
Uzuri ukiwambia nipe nyama yangu wala hawabishi wala kukataa wanakurekebishia fasta.
Jana nimepigwa nusu kilo nikaona sio vibaya niwambie wenzangu.
Waziri Mwigulu Nchemba , RC Paul Makonda, W. J. Malecela mfikishie swahiba wako ujumbe huu, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni najua upo humu, naomba ufuatilie huu wizi wa hawa jamaa.