TAHADHARI: Wagonjwa wa akili 150-250 wanapokelewa Mirembe kila siku

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,323
7,963
Idadi hiyo imetajwa katika Idara ya Huduma za Nje ambapo kati yao, Wagonjwa 30 hadi 70 hupewa Matibabu na kuondoka huku Wagonjwa 9 hadi 15 wakilazwa.

Daktari wa Vyanzo vya Akili, Veronica Lyimo amesema tatizo hilo linazidi kukua nchini na asilimia kubwa ya Wagonjwa hukutwa na sababu za Kibaoloja, Saikolojia na Kijamii.

Akitolea ufafanuzi amesema sababu za Kibaolojia zinahusisha Magonjwa ya Akili ya Kurithi pamoja na Kifafa na sababu za Kisaikolojia zikichangiwa na Malezi Mabovu kwenye jamii ikiwemo Matumizi ya Vilevi, Msongo wa Mawazo na Dawa za Kulevya.

========================

Hospitali ya Taifa ya Afya ya akili Mirembe jijini Dodoma, inapokea wastani wa wagonjwa wa akili 150 hadi 250 kwa siku kwa ajili ya matibabu.

Idadi hiyo imetajwa kuwa katika kitengo cha huduma za nje ambapo kati ya wagonjwa hao, wagonjwa 30 hadi 70 hupewa matibabu na wagonjwa tisa hadi 15 hulazwa. Taarifa hiyo imeelezwa leo Alhamisi, Oktoba 6, 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dk Paul Lawala wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea wiki ya maadhimisho ya afya ya akili jijini hapa.

Dk Paul amesema kutokana na kuongezeka kwa matukio ya kikatili na mauaji kwenye jamii, yanadhihirisha kukua kwa tatizo la akili ambayo husababishwa na sababu mbalimbali. Kwa upande wake, Daktari wa vyanzo vya akili Veronica Lyimo amesema asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo hukutwa na sababu za kibaiolojia, saikolojia na kijamii.

“Tukizungumzia sababu za kibaiolojia hapa unazitaja sababu za magonjwa ya akili ya kurithi na magonjwa ya ndani kama kifafa. Lakini kwa sababu za kisaikolojia ni malezi mabovu ambapo katika jamii kukiwa na sababu za makundi yasiyo rafiki, matumizi ya pombe, msongo wa mawazo na matumizi ya madawa ya kulevya,” amesema.

MWANANCHI
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom