Elections 2010 Tahadhari-vijana acheni vitambulisho vya kupigia kura majumbani

KIDUNDULIMA

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
966
537
nawashauri vijana kote nchini hasa kwenye majimbo ambako CCM hawapui, waviache vitambulisho vya kupigia kura majumbani badala ya kutembea navyo. Hii ni kwa sababu katika maeneo hayo vijana wanakamatwa kamatwa ovyo na kuswekwa ndani. Na ukiwa ndani vifaa huachwa counter na kama kuna kitambulisho ni rahisi kwa polisi kukificha ili upoteze haki yako ya kupiga kura. Kijana kama huna kitambulisho zaidi ya cha mpiga kura bora ukachukue barua toka serikali ya mtaa ndo utembee nayo kama kitambulisho la sivyo tutapoteza wapiga kura wengi vijana kutokana na kamata kamata ya polisi. Si mmeshasikia Arusha na Mwanza jinsi vijana wanavyoswekwa ndani? Huo ni mwanzo majimbo mengine yatafuata.
 
Hili ni angalizo zuri haswa tukizingatia Mama Salma amesikika akilalama na vijana ndiyo wanataka kuivunja ndoa yake kwa kutomchagua mzee wake.......... JK
 
Lakini pia wawe macho maana kama mkeo ni sisi m au mmeo ni sisi m atakuibia na kukificha hadi 1.11.
Nashauri kama mmeo na mkeo ni sisi m chukua shahada yake ifiche hadi tarehe 1.11 ili asipige kura kuharibu matokeo yetu.
 
sasa hii ni mbinu chafu...........sisi sio wachafu bana, tutawashinda kihalali kabisa!
 
Kuna moja alikuwa ananisogelea kubaini kama nina shahada na kama nitapiga kura. Kwa sababu najua umafia wake, nikahamisha kila kitu. Huko nilikoweka bora panya washerehekee, ila Oct 31 nitakong'oli penyewe
 
sasa hii ni mbinu chafu...........sisi sio wachafu bana, tutawashinda kihalali kabisa!

CCM wakikabwa koo hakuna uhalali. Kumbuka walishajifunza Kenya, Zambia, na Malawi kuwa ni gharama kubwa kwa chama kilichopo madarakani kupoteza uchaguzi mana hakitapata nafasi ya kurudi tena madarakani.
 
Usalama wa taifa wamesha anza kutafuta ushindi kwa waajili wao!:blah:
 
Back
Top Bottom