Tahadhari: Usiruhusu askari wa usalama barabarani kuandika namba yako ya leseni

Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,853
1,521
Salaam jf.

Kwa wale madereva wa jiji la Dar wenye magari binafsi au ya ofisi, usikubali kutoa namba zako za leseni pale askari wa usalama barabarani anapozihitaji namba zako kwa muundo wa kutaka umtajie na yeye azinakiri kwa karamu katika karatasi au wewe uziandike katika karatasi halafu umpatie.

Kufanya hivyo utajikuta siku moja ukilia kilio cha kubweka kama mbwa. Kuna fashoni siku hizi imeingia kwa maaskari wa usalama barabarani ukimpatia nambari yako ya leseni anakaanayo na anasave kama namba phonebook, siku akijisikia kukupigia ili akujulie hari yako unakutana na missed call za madeni kama zote.

Sasa unaanza kushangaa mbona nadaiwa kama laki hivi! Halafu ukitolewa lisiti ya deni unakutwa mzee mzima ulikamatwa tarehe fulani kwa nambari T ZZZ 999 ukichungulia nambari za gari unakuta ni semi trailer mercedes benz mashine ya kijerumani.

Sasa unaanza kushangaa lini uliendesha mercedes wakati wewe upo na passo miaka nenda rudi. Ukikamatwa na trafiki akiomba leseni mpe kama anataka kukagua au kukupiga faini.

TII SHERIA BILA SHURUTI.
 
Ameeleweka sema utakuwa na kichwa kikubwa hivyo kizito


You might be true kwamba nina kichwa kizito a.k.a slow learner.

Sasa wewe akili kubwa hebu naomba unieleweshe in brief... amemaanisha nini ?

Na ukishindwa kuclarify vizuri, basi wewe ni mpumbavu & lofa.

-Kaveli-
 
You might be true kwamba nina kichwa kizito a.k.a slow learner.

Sasa wewe akili kubwa hebu naomba unieleweshe in brief... amemaanisha nini ?

Na ukishindwa kuclarify vizuri, basi wewe ni mpumbavu & lofa.

-Kaveli-
By the way kama wewe huishi Dar itakuwa ni vigumu kuelewa hii maada .maana Dar tumetangulia mbele kidogo kuhusu mambo ya kuandikiwa faini za makosa ya trafic
 
Labda nifafanue vizuri. Hizi mashine za risiti za faini, siku hizi matrafiki wanaandika hata kama yupo kwake sio lazima awe na gari barabarani, yeye akiwa na namba ya leseni yoyote ile anaweza kukubambikizia kosa (haya kwa maaskari wasio watiifu)
 
Ilishamkuta jamaa yangu. Hili ni baa halisi kabisa. Baada ya kukataa kumpa ya kubrashia viatu, Cheupe alinakili namba ya leseni na gari. Akamchapa tatu za fasta kimya kimya.

Kuja kukuta deni 170k baada ya malimbikizo ya fine. Hatuna mfumo wa kujitetea kwa issues kama hizi....

Driver beware
 
Mi yangu tulibadirishana na boss akanipa gari niendeshe... mi nikampa leseni yangu anitunzie....maisha rahis sana
 
Back
Top Bottom