Jindal Singh
JF-Expert Member
- Sep 9, 2015
- 1,853
- 1,521
Salaam jf.
Kwa wale madereva wa jiji la Dar wenye magari binafsi au ya ofisi, usikubali kutoa namba zako za leseni pale askari wa usalama barabarani anapozihitaji namba zako kwa muundo wa kutaka umtajie na yeye azinakiri kwa karamu katika karatasi au wewe uziandike katika karatasi halafu umpatie.
Kufanya hivyo utajikuta siku moja ukilia kilio cha kubweka kama mbwa. Kuna fashoni siku hizi imeingia kwa maaskari wa usalama barabarani ukimpatia nambari yako ya leseni anakaanayo na anasave kama namba phonebook, siku akijisikia kukupigia ili akujulie hari yako unakutana na missed call za madeni kama zote.
Sasa unaanza kushangaa mbona nadaiwa kama laki hivi! Halafu ukitolewa lisiti ya deni unakutwa mzee mzima ulikamatwa tarehe fulani kwa nambari T ZZZ 999 ukichungulia nambari za gari unakuta ni semi trailer mercedes benz mashine ya kijerumani.
Sasa unaanza kushangaa lini uliendesha mercedes wakati wewe upo na passo miaka nenda rudi. Ukikamatwa na trafiki akiomba leseni mpe kama anataka kukagua au kukupiga faini.
TII SHERIA BILA SHURUTI.