Tahadhari ukienda kununua gari show room kuwa makini sana

Hadithi yako ni kama yangu.
Nakumbuka mwaka fulani hivi majuzi nilinunua simu ya mkononi.
Ilikua ni Samsung Galaxy s6 edge. Nilinunua kwa sh 370,000.
Nilikaa nayo miezi mitano ndipo nilipofuatwa na askari kuwa ile simu ni ya wizi. Askari hao walikuja pamoja na yule dada aliyeniuzia. Tukaenda mpaka Osterbay kuandika maelezo.
Sikurudishiwa hata cent tano

Nilichogundua ni kuwa yule dada anashirikiana na wale jamaa kutapeli watu.
Yeye anauza alafu baada ya muda wanaifuata simu yao. Kwakua hakuna mauziano halali ya simu za mkononi, basi unakosa cha kujitetea
Duh!
 
Daah polee sana mkuu,nmejifunza kupitia wewe,Kamwe sitanunua kifaa chichote (used) chenye thamani kutoka mikononi mwa mtu!Hasa hizo Simu ,gari n.k
 
pole sana mkuu
showroom nyingi mjini magumashi mengi
sjui ule mpango wakuzihamishiaga kigamboni uliishiaga wapi
mi naonaga bora kuagiza tu mwenyewe either befoward tradecarview au sbt
 
Wenye showroom wamekutapeli lakini wewe kutaja hiyo showroom kwa jina hutaki. Je? Tukisema huu ni umbea tunakosea?
Au tukisema kuwa hajatapeliwa bali yeye nimpinzani wa mwenye hiyo showroom anataka kumuharibia mwenzie biashara tutakuwa tunakosea? Anachoficha ficha ni nini?
 
Au tukisema kuwa hajatapeliwa bali yeye nimpinzani wa mwenye hiyo showroom anataka kumuharibia mwenzie biashara tutakuwa tunakosea? Anachoficha ficha ni nini?
Baelezee ndugu yangu. Huyu hauzi mwenzie anauza anamletea kauzibe
 
Hivi kwa sasa gari show room unaweza kufika milioni tano? Msimu huu wa korosho sitaki kufanya kosa. Nitakuja huko Daesalamu mwenyewe
 
Pole Sana mkuu, zinaitwa yards hizo zinazouza used cars, show rooms wanauza gari mpya.
 
Ni Bora niishi bila gari kuliko kununua kwa mtu mweusi wa hapa Bongo au showroom za hapa Tanzania....watanzania matapeli sana na ushirikina hapo hapo plus lawama kibao, hapo ulienda kununua gari na haukuwa tapeli......siku zote nitabaki kutomuamini binadamu. Baadae wanasema maisha magumu na kazi hakuna wakati wamefungua ofisi kuzuga tu....ndani yake wanafanya utoporo mtupu.
Na sisi raia tubadilike, tufanye biashara na Kampuni kubwa kwa usalama wa kipato chetu, watu kama befoward au SBT sidhani kama ukanjanja huu ungetokea.
 
USHAURI WANGU MTU YEYOTE ANAETAKA KUNUNUA GARI AAGIZE MWENYEWE KUTOKA JAPAN ACHANA NA JANJA JANJA YA HAPA BONGO SJUI SHOWROOM SJUI GARI YA MKONONI KWA MTU( GARI YA KUMVUA MTU) AU GARI MTU KASHINDWA KITU FULANI ANAIUZA ILI APATE HELA ACHANA NA HIZO SHORTCUT, HAKUNAGA UZITO KUSUBIRIA GARI MWEZI MZIMA KUTOKA JAPAN. KUNA ADVANTAGES NYINGI KULIKO HASARA UTAKAZO PATA KUHANGAIKA NA GARI ILIYOTEMBEA KWENYE ARDHI YA BONGO ILIYO NA MATATIZO KILA SEHEMU. PLS SHIKA USHAURI WANGU USINUNUE GARI YA MBONGO.
Tatizo pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom