Tahadhari uhaba wa Wahadhiri vyuo vya elimu ya Juu Tanzania

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,232
24,093
20 October 2021

Dar es Salaam.
Vyuo vikuu vya ndani vinakabiliwa na upungufu wa wahadhiri wenye sifa, kwa mujibu wa wakuu wa vyuo.

Siri hiyo imefichuliwa wakati wadau wa elimu wakieleza wasiwasi kuhusu ubora wa wahitimu hapa nchini.

Akizungumza katika mkutano ulioikutanisha Serikali, makamu wakuu wa vyuo na wadau muhimu wa elimu Dar es Salaam hivi karibuni, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka alisema shida hiyo bado haijashughulikiwa.

“Tumeshuhudia katika maeneo mengine wafanyakazi wakiajiriwa mara kwa mara, lakini inaonekana vyuo vikuu vimesahaulika kidogo. Tunaomba eneo hili pia likumbukwe,” alisema Profesa Kusiluka.

Akijibu ombi hilo, Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako aliiambia Mwananchi kuwa, changamoto hiyo inajulikana na kuna mfuko utakaotoa ufadhili wa masomo kwa wahadhiri 1,000 ili kuwawezesha kupata sifa za kufundisha vyuo kikuu.

“Hii ni moja ya hatua tunazochukua kuhakikisha elimu inayotolewa na vyuo vyetu ni bora, hivyo lazima tupate suluhisho kwa changamoto hizi,” alisema Profesa Ndalichako.
Katika miaka miwili iliyopita, takwimu za Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) zinaonyesha kuwa wafanyakazi wa vyuo vikuu wameongezeka kutoka 6,238 mwaka 2019 hadi 7,187 mwaka 2020.
Source : Tahadhari uhaba wa Wahadhiri vyuoni



Kutoka maktaba:

4 Jan 2019

Serikali: Uhaba wa wahadhiri (Wanataaluma) kwenye vyuo vya umma unashughulikiwa




Serikali imeeleza mkakati wake wa kuongeza idadi ya wahadhiri (wanataaluma) kwenye vyuo vikuu vya umma ili kukabiliana na uhaba wa wahadhiri kwenye vyuo hivyo unaotajwa kusababishwa na sera ya Serikali ya miaka ya 90 ya kusimamisha kuajiri wanataaluma.

Serikali imesema tayari imetenga Bilioni 4 kwa ajili ya kusomesha wahadhiri 68 walioko mafunzoni na wahadhiri wengine 32 wako njiani kuelekea mafunzoni.

Chanzo: Azam tv
 
Back
Top Bottom