Tahadhari: Tutarajie hoja ya misaada ya mashoga kutumiwa kisanii kuwahadaa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari: Tutarajie hoja ya misaada ya mashoga kutumiwa kisanii kuwahadaa wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RMA, Nov 5, 2011.

 1. R

  RMA JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tayari serikali ya ccm iko mahututi. Ni ufisadi umewafikisha hapo walipo kiasi kwamba hawana hoja za kuwadanganya wananchi kuhusu ugumu wa maisha. Wananchi wanaelewa kinachoendelea. Lakini nionavyo mimi: Sasa watapata mahali pa kupumulia! Usanii wa kisiasa utatungwa ili kuwadanganya wananchi wasio na uelewa mpana kwamba ugumu wa maisha tulio nao ni kwa sababu ya kukataa kuruhusu ushoga ili tupate misaada! Subirini tu mtazisikia kauli za namna hiyo hivi karibuni.
   
 2. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Na kweli hawa wapuuzi wasio na haya wanaweza kuwadanganya wavivu wa kuchanganua mambo... Yaani mimi natamani misaada yote ingezuiwa ili tutie akili.
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hizo fikra zako za kipuuzi unazo wewe peke yako. Watu wanajua kwamba hakuna msaada uliositishwa na kama ulidhani kwamba msaada umesitishwa ili na wewe utafute kitu cha kuishutumu serikali basi fikiria upya!
   
 4. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  You are very right ......serikali ya JK imepata kuti la kujishika....itawajaza upepo karibuni....
   
 5. R

  RMA JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli unauma lakini habari ndo hiyo! Hata kama hakuna msaada uliositishwa, bado ccm itaibuka na kauli ya usanii wa uongo kwamba hali ngumu ya maisha ni kwa sababu ya kukataa misaada yenye masharti. Tofauti na hapo hebu semeni mtapumulia wapi.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,520
  Likes Received: 81,873
  Trophy Points: 280
  Hali zao sasa hivi ni mbaya sana. Wanaweza kuropoka lolote ili kuwahadaa Wananchi...Na kama ulivyosema wanaweza kabisa kulitumia hili ili kujiongezea umaarufu wasiokuwa nao.
   
Loading...