Tahadhari: tuache kula mafuta ya alizeti la sivyo tutapofuka.

Kuna huyu mjasiriamali anayeitwa Mount Meru Petroleum, hii ndiyo biashara yake kuu Arusha na Singida, nami ni mmoja wa wateja wake. Kama kuna ukweli kwa hili jambo basi inatisha maana mafuta haya yamekuwa ndiyo option ya wengi kwa miaka hii.
 
Habari hizi zinaweza kuwa na ukweili - all in all najua kuna ujanja fulani unafanyika - unakuta kiwanda wanadai wanakamua mafuta ya alizeti lakini ukienda kununua mashuda hakuna- yapo kidogo mno ukulinganisha na mafuta yanayozalishwa. Wengine wansema wanacahngaya na mafuta fulani imported kama crude oil kwa shughuli za utengenezaji wa sabuni - sina uhakika lakini kuna jambo. Aliwahi kusema bwana mmoja anamjua mfanyakazi wa kiwanda kimoja Arusha alipopewa mafuta ya motisha aliyauza na kununua mafuta mengine dukani.

Najua moja tu jaribu kuwa makini na mafuta better hata yale yanayouzwa njiani ukutoka na kuingia Singida.
 
Kuna huyu mjasiriamali anayeitwa Mount Meru Petroleum, hii ndiyo biashara yake kuu Arusha na Singida, nami ni mmoja wa wateja wake. Kama kuna ukweli kwa hili jambo basi inatisha maana mafuta haya yamekuwa ndiyo option ya wengi kwa miaka hii.

Wakuu mashudu ya alizeti yanatumika sana kufanya mixing ya chakula cha kuku, sasa kama yanakamuliwa tena kwa kutumia hii kemikali basi hata hawa kuku tunaokula kila siku mitaani pamoja ya mayai ni hatari sana hasa kwa watoto wetu wapenda chips mayai / kuku.

Katika kila kilo 1000 za chakula cha kuku mashudu ya alzeti ni arround kilo 200. saa angalia ratio hiyo. Mashudu haya yamepanda ghafla na hayapatikani kwa urahisi, kilo ilikuwa sh 150 kwenye viwanda vya kukamulia alzeti ila sasa hivi ni zaidi ya sh 300. sasa sijui kama kuna connection yoyote kwamba wananunua kuyakamua tena. pia wafanyabiashara toka kenya wanayanunua kwa wingi sana na ndiyo wamefanya soko kupanda.

hatari if this is true.
 
Wataalam wa inteligency je ni kweli? isije kuwa ni mawazo ya mtu na story za vijiweni mnatuletea humu.
We unachekesha kweli, unafikiri intelijensia ipo kwaajili ya kukulinda wewe au? Ipo kwaajili ya kuhakikisha magamba wanatawala milele wananchi wanajilinda wenyewe
 
sasa tutaponea wapi!kila mahali shida tu
aya mtwambie wenzetu iyo alizeti pure nitaijuaje?
mana mie ndo mafuta yangu..olive oil bei imenishinda
 
Wanajamii nimesoma maelezo ya wachangiaji wengi nimeona kuna uelewa mdogo wa nini hasa kinafanyika katika utengenezaji wa mafuta ya kula. Mafuta ya kula yapo katika makundi kadhaa nitazumguzia kifupi mafuta yatokanayo na mgegu za mafuta, inaweza kuwa alizeti, ufuta, pamba, au mawese. Katika kundi hili kuna mbegu nyingi zaidi hata mbegu za mabonga zinaweza kutoa mafuta mazuri tu ila nimepanda hizo chache kwa kuwa inaelekea zinapatikana kwa wingi zaidi hapa nchini. Mbegu za ufuta na alizeti ni rahisi kutengeneza mafuta kwa kuwa zina tindikali kidogo zaidi wao wataalamu wanapenda kuita Free fat Acid(FFA). Kiwango kilichomo hakina madhara makubwa kwa mwanadamu kama ukitumia mafuta hayo bila ya kuweka dawa ya kuondoa tindikali Sodium Hydroxide. Dawa inatumika kuondoa tindikali hasa kwenye kama za pamba ambazo zina FFA nyingi mafuta ya pamba ni lazima yaondolwe FFA.
Ukiondoa hatua ya kuondoa FFA mafuta yanapitia hatua nyingi za utengenezaji. hatua ya mwanzo ni kukamua mbegu hiyo ili kupata mafuta ghafi, hatua hii mashine mbalimbali hutumika kwa kulingana na aina ya mbegu husika. Baada ya hapo hatua ya kuondoa FFA hufuata na hatua nyingine ni kuondoa rangi (bleaching) na hatua ya mwisho ni kuondoa harufu (deodorization). Hatua zote tatu zina umuhimu wake. Kama nilivyoeleza awali ni muhimu kuondoa FFA ili kulinda afya za walaji lakini vilevile katika hatua hii husani kwenye mafuta ya alizeti unapuguza kiwango fulani cha protini na kuongeza maisha ya mafuta katika maeneo ya mauzo (expiry Date) inakuwa ya mbele zaidi kuliko ambavyo ingekuwa bila kupitia hatua hiyo. Suala la rangi ni kuwa chakula kinapasa kiwe na rangi ya kuvutia, suala la harufu nadhani liko wazi.
Lakini ufundi mwingine wa kuzalisha mafuta kutokana na mashudu ufundi huo unaitwa desolventing yaani unaondoa mafuta yaliyobaki katika mashudu kwa kutumia kemikali ambayo yenyewe haichanganyiki na mafuta ila inaweza kuondoa mafuta katika usailia fulani. Kwa mfano ukitumia benzene kuondoa uchafu kwenye nguo, labda tuseme unataka kutoa girisi ukiweka benzene itaondoa hiyo girisi toka kwenye nguo lakini hiyo benzene inaweza kutenganishwa na girisi na benzene hiyo ikatumika tena. Ila kwa kuwa gharama za kufanya hivyo ghali basi haifanyiki.
Ufundi wa kutoa mafuta kutoka katika mashudu unahusisha matumizi ya kemikali ya hexane ambayo ikitumika katika mitambo kwa kuchanganya na mashudu mafuta yaliyobaki katika mashudu hujitenga na mashudu, na hivyo mafuta huendelea kutengenenzwa kama kama nilivyoeleza hapo juu.

Hexane iliyotumika huwa inakombolewa na kutumika tena kwa uzalishaji mwingine. Kwa ujumla hautua haina madhara ila ubora wa mafuta hayo ni tofauti kiasi na mafuta yanakamuliwa moja kwa moja ila hayana madhara ni mazuri kwa matumizi ya chakula. Uzalishaji wa mafuta ya mawese yana mafungu mawili, fungu la kwanza ni yale mafuta toka kwenye gamba la mbegu ya mawese ambapo kuna ufundi unaitwa fractional distallation hutumika ni kama uzalishaji wa mafuta toka katika visima vya mafuta, lakini hatua nyingine zinafanana. Kwa ufupi ethanol au methanol hazitumiki katika kuzalisha mafuta ya kula.
 
Mimi nimethibitisha kuwa hizi habari niza kweli cha kushangaza ni kuwa hii practice niya muda mrafu na pamoja na kuwa TZ tuna utitiri wa agencies (TFDA, TBS, MKEMIA, Maabara ya mifugo, Vyuo vikuu, TFNC na UWT) bado wananchi tunaendelea kulishwa sumu kwa gharama yetu wenyewe.
 
Miaka miwili iliyopita niliwahi kupashwa habari na whole seler wa mafuta ya alizeti jijini dsm kuwa madukani sasa kuna mafuta ya alizeti ya aina mbili.

Aina ya kwanza ni yale yalikamuliwa kwa njia ya kawaida - haya sina ugonvi nayo.
Aina ya pili ni mafuta yanayokamuliwa kutoka katika mashudu baada ya ukamuaji wa kawaida kumalizika - haya ndiyo shaka langu.

UKAMUAJI HUFANYIKAJE?

Mashudu ya alizeti humwagiwa ETHANOL kisa mafuta yaliyobaki ndani ya mashudu hujitenga.

Kutokana na biashara hii mashudu ya alizeti yamepanda bei kuliko kawaida. Nawashauri mtumie mawese ili musipofuke.

Mi nafikiri tahadhari ya kutokula peke yake haitoshi mkuu inabidi mamlaka ya chakula na TBS ifanye ufuatiliaji wa hali ya juu kubaini yalipo makampuni yanayofanya haya mambo ya uuaji. Ni kweli mashudu yamepanda sana kutoka elfu 10 hadi zaidi ya elfu 20 na pia yameadimika sana.
 
Back
Top Bottom