Tahadhari: Teja akikuomba pesa mpatie, hachelewi kukusingizia unauza madawa

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
100,026
122,645
Wana jamii wote tahadhari kubwa sana ichukuliwe pale teja la madawa ya kulevya (maaruf "unga") litapokuja "kukupiga mzinga" (kukuomba pesa) hususan kama tulivyowazoea omba yao kubwa ni "Buku".

Usifanye ubahili wakati huu kwani ukimuudhi tu na akienda kusema wewe ndiye unamuuzia unga utajiunga na fiesta kule central police station.

Mpe hiyo "buku" na kama hauna japo kamkopee, maana wana hasira kwani ni lazima unga utakuwa adimu mitaani kwa trend hii ya bwana Makonda inavyoenda na arosto waliyonayo, mateja wanaweza kufanya lolote la ajabu.

Tahadhari sana. Hii siyo joke.
 
Aksante kwa tahadhari bi mkubwa, vipi ban imeisha lini?
 
Sasaaa
Hapana nimpe mtu buku kisa naogopa nisitajwe kua muuza unga?
Hapana kutajwa peke yake hakukamilishi ushahidi wa Mimi kufungwa jela kama muuza unga.

Ushahidi mkubwa unahitajika mpaka nitiwe hatiani sio teja kunitaja tu, ifahamike mateja hata mahakamani wanawajua kua wakiwa na alosto wanaweza sema lolote au kufanya lolote
 
Jela unaweza usifungwe lakini muda na rumande unaweza kuswekwa.

Bongo Bingo.
 
Siwezi kutoa pesa labda kama sijiamini ndio nitatoa .......

Si anipeleke uko tuone kama ataweza kunipa kesi ya kipuuzi hivyo.........
 
Wana jamii wote tahadhari kubwa sana ichukuliwe pale teja la madawa ya kulevya (maaruf "unga") litapokuja "kukupiga mzinga" (kukuomba pesa) hususan kama tulivyowazoea omba yao kubwa ni "Buku".

Usifanye ubahili wakati huu kwani ukimuudhi tu na akienda kusema wewe ndiye unamuuzia unga utajiunga na fiesta kule central police station.

Mpe hiyo "buku" na kama hauna japo kamkopee, maana wana hasira kwani ni lazima unga utakuwa adimu mitaani kwa trend hii ya bwana Makonda inavyoenda na arosto waliyonayo, mateja wanaweza kufanya lolote la ajabu.

Tahadhari sana. Hii siyo joke.
Zamani nilikuwa nakuona kama zuzu fulani na ushungi wako, lakini sasa nimekuvulia kofia. Kwa hiyo ushapanga dili na watoto wako ulioshindwa kuwalea wapite mitaani wakituomba buku na wewe ndio unakamata nafasi yako kutuandaa kutoa buku...hola!

Sitoi buku wala panya mawazo. Mwambie mwanao Dula hapa pagumu aje na maji
 
Hii ni tahadhari tu. Kutowa au kuto kutowa ni uamuzi wako.
 
Utajipotezea muda kwa "buku" tu, wakija wanakuchukuwa mpaka wajuwe huhusiki na umesingiziwa tum umeshapoteza mambo mengi.
Potelea mbali siwezi kuendekeza " ujinga" buku yenyewe usawa wa Magufuli huu sitoi nimesema sitoi waende huko Polisi wakaseme kama wanaweza.
 
Wana jamii wote tahadhari kubwa sana ichukuliwe pale teja la madawa ya kulevya (maaruf "unga") litapokuja "kukupiga mzinga" (kukuomba pesa) hususan kama tulivyowazoea omba yao kubwa ni "Buku".

Usifanye ubahili wakati huu kwani ukimuudhi tu na akienda kusema wewe ndiye unamuuzia unga utajiunga na fiesta kule central police station.

Mpe hiyo "buku" na kama hauna japo kamkopee, maana wana hasira kwani ni lazima unga utakuwa adimu mitaani kwa trend hii ya bwana Makonda inavyoenda na arosto waliyonayo, mateja wanaweza kufanya lolote la ajabu.

Tahadhari sana. Hii siyo joke.

FaizaFoxy , kwa lugha nyingine unaituhumu serikali kwamba inakusanya kusanya watu tu bila kufanya hata uchunguzi wa awali?

Kwamba kila mtu akitajwa hakuna intelijensia ya kuchunguza kama kuna sababu ya kumshikilia kwa uchunguzi zaidi?

Kwamba sasa jeshi letu liko katika ngazi ya sungusungu ambako mtu alikuwa akisemwa semwa tu tayari anahukumiwa na hata hukumu za vifo?

Haki itatendekaje katka jehsi la namna hii? Nini kifanyike?
 
Kwa sababu unaonekana kuwa na akili sawa na za teja nikuulize kuwa kwa mfano niko barabarani halafu hilo teja lako linaniomba hela nakataa kulipa litaenda polisi wapi ili linitaje kwa jina gani wakati limenikuta tu njiani wala halinijui?
 
Back
Top Bottom