Tahadhari, sio Kila boda Ni wa kumwamini na sio Kila abiria, Ni abiria kweli hasa nyakati za usiku, punguza Safari zisizo lazima usiku

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,903
Wakuu, Pamoja na kwamba boda boda Ni moja Kati ya ajira zinazowaokoa vijana wengi na kuwainua kiuchumi, Lakini baadhi yao aidha hawajui maana ya kujiajiri au wanatumika kuwahujumu maboda original, au sometimes wanakuwa na tamaa zisizo za msingi!!

Kuna binti mmoja kitaani hapa alinusulika kubakwa na boda nyakati za usiku, kaingia town late kidogo kutoka mji mmoja mitaa ya saa 6 night, kaita boda , wamekubaliana Bei, safari ikaanza, jamaa alivyofika mahali Kuna uwazi kdogo na majani , akasimamisha chuma yake , huyo binti kamuuliza kulikoni??

Jamaa akamwambia shuka kidogo, kisha from no where si akamnyan'ganya phone na noti kisha kampiga mtama, mara binti chini, jamaa akaanza kuforce kula mzigo kimazabe hku akimtishia ukipiga kelele nakuua!

Kabla jamaa hajaanza shughuli ghafla ukatokea mwanga mkali ikabidi mbakaji na jangili atimke, kumbe Ni boda TU naye alikua anarejea home akashangaa kuona boda katoka kwa speed afu bint yuko pale chini kandokando ya Barabara.

Kamuuliza kulikoni, ikabidi ampe full mkanda akshauri aliport Polisi!

Haya mambo yamezidi ndugu zangu, juzi Kati boda mmoja mida ya 11 alfajiri yuko harakati kakutana na mwana dada mmoja anajifanya msafiri kumbe ni chambo!!

Boda anampeleka sijui Nini kilitokea, umeokotwa mwili asubuhi jamaa kachinjwa shingoni, damu tupu zimezagaa chini na pikipiki haipo!!

Jamani jihadharini huko mliko!!
 
Ulifanikiwa kupata vitu alivyokupora huyo boda? Pole sana kwa kunusurika kubakwa, sijui ulishukuru Mungu au mwanga wa boda au boda aliyekuja?
 
download (1).jpeg

Moyo wa mtu ni kichaka huwezi jua huyu anania gani kwa kumuangalia tu usoni!!,unapofanya kazi huoni kazi unaona hiyo picha hapo juu!.. pesa inasifa ya kutafutwa ila kwa wachache baadhi huwa inawatafuta!.. maisha yetu sisi watu wa vipato vya chini ni kuitafuta pesa. Ni muhimu kuwa makini ila ngumu maana uhalifu si usiku tu hata mchana pia!.
Life is full of shit.
 
Hiyo ndo sababu lazima niwe na namba za simu za madereva wa bodaboda, Uber, na tax ninaowafahamu!! There's no WAY naweza kupanda bodaboda au taxi wakati wa usiku.

Only option kama nawakosa "madereva wangu" ni kupanda daladala, period!!
 
Ulifanikiwa kupata vitu alivyokupora huyo boda? Pole sana kwa kunusurika kubakwa, sijui ulishukuru Mungu au mwanga wa boda au boda aliyekuja?
Kwa mujibu wa shuhuda, aliambulia bag na kijimkoba ila pochi na phone jangili boda aliamsha navyo!!

Tumshukur Mungu kwa kumnusuru kubakwa, pengine HIV au Hepatitis ingemhusu huyo binti au mbakaji!!
 
Ingewekwa sheria madereva wa boda boda kuvaa reflector jackets zenye namba kubwa mgongoni. Ikiwa na namba za pikipik, kituo anachopack na jina kabisa. Ingesaidia kupunguza huu uhalifu.
 
Hii kazi ina majaribu sana.Ngoja niwape stori ya miaka 2 nyuma kuna wadada niliwapakia maeneo ya tegeta wanakwenda mashimoni (skanska kwa chini kidogo) sasa niliwapakia mshikaki ilikuwa ni usiku around saa 8 au 9 kipindi hicho nakesha sasa basi wakasema wamebanwa na mkojo nami nikatafuta eneo zuri nkawaambia haya kojoeni hapa nao wakasema twende tuu tutakojoa home sasa basi ile nawafikisha nyumbani kwao walipopanga wakaenda mbele ya taa kubwa ya nyumba wakavua nguo wote wakakojoa huku mimi wameniachia ma***ko nayakodolea macho walivyomaliza wakaja huku chupi zipo magotini wakaanza kunichezea nyimbo wakiwa uchi kabisa na kuniambia niwape elfu 10 niwale wote na chumba ni chao na kuhusu usalama wa boda wakasema unaisogeza hadi mlangoni alafu tunaacha mlango wazi ili uione aiseee niliwaza mengi sana kama ningekua nina tamaa ningetafuna wote ila nikawakatalia kwakua namuacha mkewangu kuja kukesha kwa ajili ya kutafuta pesa ila haya mengine hapana,hayo ndio majaribu niliyokutana nayo
 
Aisee mimi nikisikia mtu anabaka huwa napata hasira mno, unaweza kutongoza na kumaliza haja zako...ukiona gharama madada poa wamejaa huko hata 2000 unamaliza hizo haja zako...kwa nini umsababishie mwenzako mfadhaiko ikiwezekana umwambukize magonjwa yako au umtie kabisa mimba ambayo huwezi kuilea
 
Usiku yakikukuta umejitakia gest kibao lala ww dada unaripot usiku sasaba nakulima vboko kwanza
 
Hii kazi ina majaribu sana.Ngoja niwape stori ya miaka 2 nyuma kuna wadada niliwapakia maeneo ya tegeta wanakwenda mashimoni (skanska kwa chini kidogo) sasa niliwapakia mshikaki ilikuwa ni usiku around saa 8 au 9 kipindi hicho nakesha sasa basi wakasema wamebanwa na mkojo nami nikatafuta eneo zuri nkawaambia haya kojoeni hapa nao wakasema twende tuu tutakojoa home sasa basi ile nawafikisha nyumbani kwao walipopanga wakaenda mbele ya taa kubwa ya nyumba wakavua nguo wote wakakojoa huku mimi wameniachia ma***ko nayakodolea macho walivyomaliza wakaja huku chupi zipo magotini wakaanza kunichezea nyimbo wakiwa uchi kabisa na kuniambia niwape elfu 10 niwale wote na chumba ni chao na kuhusu usalama wa boda wakasema unaisogeza hadi mlangoni alafu tunaacha mlango wazi ili uione aiseee niliwaza mengi sana kama ningekua nina tamaa ningetafuna wote ila nikawakatalia kwakua namuacha mkewangu kuja kukesha kwa ajili ya kutafuta pesa ila haya mengine hapana,hayo ndio majaribu niliyokutana nayo
Daah! Pole mkuu, walikupa mshahara wako lakin??
 
we jamaa ni mzembe sana ingekuwa mimi nisingechomoka hapo
 
Wakuu, Pamoja na kwamba boda boda Ni moja Kati ya ajira zinazowaokoa vijana wengi na kuwainua kiuchumi, Lakini baadhi yao aidha hawajui maana ya kujiajiri au wanatumika kuwahujumu maboda original, au sometimes wanakuwa na tamaa zisizo za msingi!!

Kuna binti mmoja kitaani hapa alinusulika kubakwa na boda nyakati za usiku, kaingia town late kidogo kutoka mji mmoja mitaa ya saa 6 night, kaita boda , wamekubaliana Bei, safari ikaanza, jamaa alivyofika mahali Kuna uwazi kdogo na majani , akasimamisha chuma yake , huyo binti kamuuliza kulikoni??

Jamaa akamwambia shuka kidogo, kisha from no where si akamnyan'ganya phone na noti kisha kampiga mtama, mara binti chini, jamaa akaanza kuforce kula mzigo kimazabe hku akimtishia ukipiga kelele nakuua!

Kabla jamaa hajaanza shughuli ghafla ukatokea mwanga mkali ikabidi mbakaji na jangili atimke, kumbe Ni boda TU naye alikua anarejea home akashangaa kuona boda katoka kwa speed afu bint yuko pale chini kandokando ya Barabara.

Kamuuliza kulikoni, ikabidi ampe full mkanda akshauri aliport Polisi!

Haya mambo yamezidi ndugu zangu, juzi Kati boda mmoja mida ya 11 alfajiri yuko harakati kakutana na mwana dada mmoja anajifanya msafiri kumbe ni chambo!!

Boda anampeleka sijui Nini kilitokea, umeokotwa mwili asubuhi jamaa kachinjwa shingoni, damu tupu zimezagaa chini na pikipiki haipo!!

Jamani jihadharini huko mliko!!
Hata wenye magari pia,Mimi juzi narudi home na boda yangu mida ya saa sita usiku Kuna gari ilikuwa iko mbele yangu inaenda inasimama kama x4 alifanya hivyo,nampita ananipita,Basi akasimama gafla,nikampita,nyuma akaanza kupiga honi mfulilizo Kama anamfukuza muharibu ili watu waamke,nikaona duu,nikaingia uchochoroni akanipita akaondoka,Ila kumbukeni pia hata yule muuaji wa sinza aliyemuua yule mziba pancha pale aliienda na gari,uharifu haupo ndani ya chombo uko kwa mtu mwenyewe

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Tuna hitaji Neema ya MUNGU itawale katika maisha yetu.. Vijana wawe na hofu ya mungu, Vijana wawe wavumilivu, wasiwe na tamaaa. Mafanikio yanahitaji Muda.. Penda kazi yako na ithamini kazi yako
 
Kipindi hiki ni kigumu sana kwa rafiki zangu wapiga maji kupitiliza!! Ni HATARI.
Jitahidini sana msipite saa nne usiku, rudi nyumbani.
Kipindi hiki sio kwamba ni sababu ya shida ya pesa, hapana. Ni kama ugonjwa wa hali ya kuchanganyikiwa umeingia.
Na hii inatokana na watu wengi kukata tamaa, hawajui uelekeo!
Mmesikia kule Simiyu, mama kuchinja watoto wake mwenyewe (7&1.5yrs) na kisha yeye mwenyewe "kujichinja"
Reason: Alikuwa amerukwa akili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom