Tahadhari: Namna bora ya kutizama na kulinda "image"ya CHADEMA mbele ya umma

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
43,080
2,000
Wadau,huu ni mtizamo na mawaza yangu juu ya namna gani tunapaswa kutizima na hatimae tuweze kulinda image ya chadema.Mtizamo wangu huu ni matokeo ya mvutano unaoendelea ndani ya chama chetu ingawa kinawahusu watu wachache tu ambao tunaweza kuwapuuza ila ni lazima tuchukue tahadhari kwani inawezakana ikatokeo kesho mgogoro kama huu ukaibuka tena na safari hii ukawa mkubwa kuliko tunvyoweza kufikiria.

Kitu kikubwa kinachoathiri siasa za vyama vya upinzani hapa nchini ni watu wachache(individuals) kuwa na nguvu au umaarufu kuliko chama chenyewe.Inasikitisha sana kuoana inafikia hatua only some few individuals ndani ya chama ndio wana-define integrity na popularity ya chama.Hizo sifa mbili, kwa maoni yangu, ndio kwa kiasi kikubwa zinatumika sana ku-determine image ya chama mbele ya umma.

Msingi wa mawazo haya ni kuwa kuna watu wachache ambao wakijitoa ndani ya chama fulani, basi hata umaarufu na kuaminika kwa chama hicho mbele ya jamii kuna athirika kwa kiasi kikubwa na inaweza hata kuathiri chama husika katika chaguzi mbali mbali.Hii ni hatari sana kwa chama kinachokua na kujiimarisha kwa lengo la kushika dola.Tukubali
tukatae, chadema ni kimojawapo na ndio maana mnaona kuna watu wachache wanaolengwa kuchafuliwa kwasababu wahusika(wapinzani)wanaamini fulani akihujumiwa basi na chama kizima kimehujumiwa.Huu ni ukweli ndugu zangu tuukubali ingawa ni mchungu.Binafsi sipendi kabisa hali hii.

Njia pekee tunayoweza kukifanya chama kama chama kisimame chenyewe bila kutegemea nguvu ya indivuduals ni kuwa na msimamo thabiti wa kusimamia sheria na kanuni za chama bila kubagua.Hapa nina maana kwamba chama siku zote hakitasita kumchukulia hatua za kinidhamu mwanachama yoyote yule bila kujali wadhifa wake ndani ya chama pale tuhuma zinazomhusu kuthibitika kuwa ni za kweli.Na iwe ni mwiko kupuuza tuhuma kisa zinamhusu mtu fulani.Tuhuma zote zichunguzwe na ukweli uwekwe hadharani.

Faida ya hatua hii ni kuwa umma utajenga imani kuwa ndani ya chadema hakuna ubabaishaji na kuwa ukiwa mbabaishaji basi huna nafasi ndani ya chama.Hali hii itakifanya chama kijibebe chenyewe na hivyo kujiuza mbele ya umma.

Mwisho,tufikie hatu kuwa umaarufu wa mtu mmoja mmoja(individuals) uwe ni jambo la ziada tu ila umaarufu na sifa ya chama ndio uwe msingi wa chama kukubalika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom