Uchaguzi 2020 Tahadhari muhimu kwa CHADEMA na ACT Wazalendo

Ushauri mzuri,piakuna ushauri wa kigogo kashautoa!! Kabla ya kufika tar 28 inabidi makatibu na wenyeviti wa majimbo wa act/chadema wafatilie vituo hewa vyote! na pia lazima wawe na tallying center za kila kata-jimbo-mkoa(summation) ya mkoa ndio inaenda makao makuu ,hii itasaidia kujua jumla kuu ya vituo halali tu ,kisha mnafanya comparison ya kura na NEC katika ngazi ya jimbo ,zikienda tofauti tu na idadi halisi ,hapo inatakiwa ACT/Chadema waweke online matokeo yote nchi nzima ambayo ni halisi ,wakishaweka sisi tutajua cha kufanya!!

Kama NEC wakichakachua tunakinukisha kama GUINEA na NIGERIA.
Naam, huu Ni mpango mzuri Sana, 2015 CCM waliweka base Yao kule masaki bao la mkono, chadema ofisi Yao ikavamiwa na kuporwa vifaa vyao,

Kwa Sasa wajipange Tena kwa intelejensia kubwa maana hivyo vituo vya kujumlishia vya upinzani polisi na kitengo watavivamia na kuharibu kila kitu!!

Bora waweke vituo vingi fake ili kupoteza maboya,
Kila kitu kiwekwe mitandaoni!
Japo huenda internet ikazimwa siku hizo
 
...ccm akili zenu si za binadamu wa kawaida...
Kwa kweli. Hata mataifa mengine wanatushangaa
Screenshot_20200929-140107.jpg
 
Mawakala wa upinzani kwenye majimbo na kata pendwa siku ya uchaguzi watajikuta wanapata tatizo la tumbo kuharisha damu ( Tena ameoba)
 
Kuhusu vituo fake inabidi lifanyiwe umuhimu Sana, maana Kura feki nyingi Sana zitawekwa vituo fake, viongozi wote wa upinzani chadema/ Act wazalendo washirikiane Sana toka ngazi ya kitongoji,Kijiji,kata,tarafa na wilaya, ili kubaini vituo fake vyote, pia mawakala fake wa CCM maana Kuna sehem mawakala wanahitajika 500 CCM wameapisha mawakala 700 hao 200 wa kazi gani?

Pia lazima waandaliwe vijana/ watu kila maeneo kujiandaa kwa lolote muda wowote maana mawakala wanaweza fanyiwa Mambo ya hovyo na CCM au polisi
Ukipiga kura Linda kura by Sugu Mbeya 20/10/2020
 
Kuhusu vituo fake inabidi lifanyiwe umuhimu Sana, maana Kura feki nyingi Sana zitawekwa vituo fake, viongozi wote wa upinzani chadema/ Act wazalendo washirikiane Sana toka ngazi ya kitongoji, Kijiji, kata, tarafa na wilaya, ili kubaini vituo fake vyote, pia mawakala fake wa CCM maana Kuna sehem mawakala wanahitajika 500 CCM wameapisha mawakala 700 hao 200 wa kazi gani?

Pia lazima waandaliwe vijana/ watu kila maeneo kujiandaa kwa lolote muda wowote maana mawakala wanaweza fanyiwa Mambo ya hovyo na CCM au polisi
TEETH ndio wanaorganise kura feki ,Lissu aitishe press conference fasta kuihabarisha dunia uhuni unaoendelea wa Teeth kufeki uchaguzi mkuu.....Mwaka huu hakuna uhuni tena....Tutagawana ballot box na maturubai gazebo za NEC.
 
Kuelekea uchaguzi wa tarehe 28 naomba Chadema na ACT Wazalendo mchukue tahadhari muhimu

1) Kuhusu mawakala wenu, wajiamini, wawe makini na matukio yote, wawe wenye uzalendo maana pesa nyingi zitamwagwa siku hiyo. Pia wawahi mapema sana kabla ya saa moja maana mbinu chafu zinapangwa kutumika mapema sana asubuhi!

Pia washirikiane wote yaani wakala wa chadema na ACT- Wazalendo wawe kitu kimoja, hii itasaidia sana kupunguza mianya ya wizi.

Pia wasikubali kutolewa ndani ya kituo husika kwa sababu yoyote Ile!

2) Viongozi wakubwa wa Chadema na ACT Wazalendo kote bara na visiwani wawe makini Sana, tena sana maana mawasiliano yao yanafatiliwa, hivyo ikiwezekana kutumia njia mbadala ktk mawasiliano aubkubadili kabisa namba za simu, hii njia inatumika na kitengo ili kuzima mawasiliano na kuweza kuthibiti haki ya kutoa matokeo kwa wagombea hasa urais na ubunge.

3) Kuna uwezekano wa kuzima internet siku hiyo na zinazofuata, je mmejipangaje kukabiliana na hili? Pia mawasiliano yenu yakafungiwa hivyo vigumu kuwasiliana na kutoa updates mbalimbali, mjipange na kuchukua tahadhari muhimu zote!

4) Ulinzi na usalama wa wagombea wote urais, ubunge na udiwani. Hapa kuweni makini sana maana mipango yao ni kuwathibiti chini ya Ulinzi pindi tu muda wa kupiga Kura unapoisha saa 10, fanyeni mikakati makini na mathubuti ili kuepuka hii mitego, kuwa chini ya Ulinzi , kuporwa simu na kunyimwa haki ya kuonana hii ndo mipango iliyopo jikoni!

5) Himizeni watu wasiende mbali na vituo vyao vya kupigia Kura, maana kura feki zitaingizwa hivyo uwepo wa watu utasaidia sana kufatilia vitendo viovu vyote!

Mwisho, nawaomba kuweni watu wa vitendo, tumechoka uovu, kama jino basi iwe jino kwa jino!

Haki, Usawa na Amani ndo msingi wa uchaguzi huru!

Chagua Lissu, chagua Chadema, chagua ACT Wazalendo, chagua Maalim Seif!
Tuko pamoja
 
Back
Top Bottom