Tahadhari: Mtandao wa tigo siyo salama, umeingiliwa na matapeli. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari: Mtandao wa tigo siyo salama, umeingiliwa na matapeli.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by fluphenazine, Apr 19, 2012.

 1. f

  fluphenazine Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&amp]Habari za sa hizi wanajf, Nimeona ni bora niwashirikishe hili jambo ambalo limenitokea mimi binafsi.[/FONT]
  [FONT=&amp]Siku ya J4 tarehe 17/04 around sa sita mchana nilipigiwa simu(0717183749) na mtu aliejiita customer care wa tigo lengo likiwa ni kurekebisha huduma za tigo pesa, Akataka nimpatie namba ya fomu ya usajili (inapatikana ukipiga *106#) pamoja najina langu sahihi. Nilikataa kumpatia hizo details badala yake akaenda kwa wakala wa tigo pesa (Namba ya wakala: 10295) akanitumia 1000/=(kwa wanaofahamu tigo pesa kuna message inarudi kwa aliyetuma ikikufahamisha hiyo pesa imepokelewa na nani kwa hiyo aliweza kupata jina langu kamili) [/FONT]
  [FONT=&amp]Mpaka hapo nikawa nimehisi kuna dalili za utapeli nikaamua kuhamisha pesa zote kwenye line ya mtu mwingine.[/FONT]
  [FONT=&amp]Ilipofika mida ya sa kumi kasoro nikashangaa simu yangu imeandika “sim card registration failed” nikajaribu kuiweka kwenye headset nyingine nikihisi labda headset yangu ina matatizo, pia huko nako iliandika hivyohivyo sim card registration failed. Nikajaribu kuipiga, nikagundua inapatikana na call inapokelewa lakini anaepokea hajibu kitu. Mpaka hapo nikajua yule tapeli tayari amefanikiwa kuwa na sim card yangu, Nikaamua kuwapiga 100 (customer care) ili nipatiwe msaada, badala yake waliniambia niende ofisi za customer care zilizopo karibu, ili tatizo langu lishughulikiwe. Nikawambia sa hizi ni jioni sitaweza kuwahi ofisi mpaka nifike nitakuta ofisi zimefungwa ,akaniambia niende kesho asubuhi, nikamjibu mimi nachotaka kwa wakati huu hiyo line aiblock isitumike mambo ya kurekebisha nitafanya kesho nikienda kwenye ofisi za customer care,akanijibu yeye hana access ya kublock line hiyo huduma inapatikana ofisi za customer care tu. Basi mpaka hapo nikaona hao wamekuwa helpless kwa tatizo langu. Nikaamua kwenda police kuripoti ili in case huyu jamaa akaamua kutumia line yangu kwa uhalifu mimi nisihusike.[/FONT]

  [FONT=&amp]Ile line haikuwa hewani kwa muda mrefu mpaka sa 4 kasoro usiku kwa sababu nilituma text nikaona imekuwa delivered mida hiyo. Nikaamua kumpigia simu, safari hii akawa hapokei tena anakata alaf anatuma text “ Nitumie message simu yangu mbovu”. Nikaamua kutuma text kumdanganya kwamba kuna pesa nataka nimtumie(500,000/=). Niliamua kufanya hivo ili kujenga mazingira ya kumkamata na aendelee kuwa hewani iwe kama ushahidi kwangu. Jamaa akachachawa akakubali, Nikamambia kwa vile ni usiku kesho asubuhi anikumbushe nisisahau kumrushia.[/FONT]
  [FONT=&amp]Ilipofika asubuhi jamaa akanitafuta sana kwa kubip na text kwa wingi. Nikamwabia asijali nipo njiani ndo naenda kwa wakala. Wakati huo mimi naenda tigo customer care office. Kabla cjafika akatuma text akitaka hiyo hela nisitume tena kwenye ile line(iliyokuwa line yangu) badala yake nitume kwenye namba ya wakala atakayonipatia. Nikajua hapo atakuwa amepata tatizo la password ya a/c yangu ya tigo pesa.Nikamkatalia hapo .Cha kushangaza zaidi baada ya muda akatuma tena text akaniambia haina shida nitume kwenye ile namba yangu, mpaka hapo nkajua tayari na password ya account ameshaweza kuipata. Wakati huo nilikuwa tayari nimeshafika customer care. Nilijieleza reception nikaelekezwa pa kwenda. Huyo mhudumu wa hapo customer care nilimweleza kila kitu mwanzo hadi hapo nilipofika na kwamba jamaa bado yupo hewani na tunachat naye ansubiri nimrushie pesa.[/FONT]
  [FONT=&amp] Tofauti na mategemeo yangu kwamba tigo wangetake any action kwa hawa matapeli ili wasiendelee na hii tabia, badala yake wakaniambia kama nikitaka nimkamate mwenyewe, Eti nimwambie huyo tapeli mtandao unasumbua tukutane sehemu nimpatie hizo pesa, nikiwa na askari polisi wamkamate . Wakaniambia wao option waliokuwa nayo ni kuiblack list number yangu ili isiwe rahisi mtu mwingine kuiswap tena. Basi mpaka hapo nikaona hawakuwa na nia ya dhati kuwakomesha hawa wezi, Nikaona bora wanirudishie line yangu nisiendelee kupoteza muda, mimi nimeplay part yangu kubwa mpaka hapo nilipofikia. Basi nikarudishiwa line yangu, Nikaenda kureset password ya tigopesa. [/FONT]
  [FONT=&amp]Leo huyu tapeli kanikosa mimi kesho anaweza kumliza mtu mwingine na pia haijulikani kashawaliza watu wangapi. Je kweli haya mambo ni ya kupuuzia? Pesa zenyewe siku hizi ngumu kupatikana.Cha kujiuliza zaidi huyu tapeli aliwezaje kuswap line yangu wakati mimi nipo hewani na kwa nini nisiulizwe? Huyo tapeli aliweza vipi kureset password yangu? Ninapata hisia kubwa kwamba hawa wezi wanasupport ndani ya tigo au wapo tigo kabisa. [/FONT]
  [FONT=&amp]Kwa hiyo kwa hali ilivyojionyesha MTANDAO WA TIGO SI SALAMA mtu akiwa na namba yako anaweza kuitengeneza upya line yako aka-access mpaka account ya tigo pesa. Ninaomba niishie hapo na poleni kwa kusoma habari hii ndefu.[/FONT]
  [FONT=&amp]Asanteni[/FONT]
   
 2. Y

  Yasser5 JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahsnte mkuu kwa kutujuza
   
 3. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Tatizo letu hapa TZ hatuna utamaduni wa kukamata waharifu kabla ya kumalizia uhalifu wao. Polisi wanaweza kabisa kukusaidia ila hawana muda kwa sababu mawasiliano yote ya simu yanayofanyika yanakuwa recorded na hayafutiki na wanaowasiliana wanaweza kujulikana maeneo walipo wakati wanawasiliana. TCRA wanaweza kuretreave chochote.
  Ingekuwa kesi yako ni kumtukana mke wa kiongozi wa Polisi au wa Serikali jamaa angekamatwa mara moja tu. Hiyo ndio bahati mbaya tuliyokuwa nayo hapa nchini kwetu.
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa.
   
 5. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  shukurani mkuu, iliyobaki tusambaze ujumbe. Tigo wenyewe kama wanaelekea kuzima vile!
   
 6. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Poleni sana
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Watakuwa ni wao wenyewe wanaofanya huo uhalifu. Tuwe makini...
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Customer care na customer support ni almost NIL kwa watoa huduma wetu.

  Kampuni za simu hazijali ukiwepo au usiwepo kwenye mitandao yao, wao wanavuna zza kutosha.

  Nililalamika zisitishwe sms za matangazo zinazonijia kutoka ZANTEL kila ninapotuma sms au kupiga au kupokea simu, wakaniambia niende ofisini kwao, nilipofika huko wakaniambia niandike barua kuhusu hilo, nikawauliza "kwani niliwaandika barua ya kuomba huduma hii"? jibu likawa ukitaka fanya hivyo "kama hutaki usitumie ZANTEL". Hii inaonesha ni vipi hizi kampuni zilivyo na kiburi. Hakuna moja yenye afadhali na mwenzake, kama si hili, lile.

  Naombea zije kampuni za uhakika zinazojua "customer care" ziwagaragaze hawa waliopo, wamesha vimbiwa.

  Fikiri!
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kweli kabisa na watakuwa wanawajua vizuri tu ila wanakula nao kwanini isiwe voda au airtel kazi ipo..
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  Hao tigo wenyewe ndio mijizi
   
 11. ALLEX

  ALLEX JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 2,046
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  kweli kabisa hata mimi nilisha patwa na maswahiba hayo. Nilipo kwenda tigo wakaniambia ni mtengeneza line alikosea na kuswap kwa mteja mwingine ni wezi tu hao tena wana saidiwa na hawa wabwana wadogo walioanza kazi juzi wanataka mafanikio ya haraka haraka..
   
 12. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,858
  Trophy Points: 280
  wizi huo haupo tigo tu ni karibia mitandao yote. tena kali kuliko zote ni hii unakwenda kwenye kibanda kutuma hela kumbe yule mtu kachakachua anajua mwenyewe hivyo anatumia code ya mtu mwingine unapoomba kutuma anaingiza hela kabisa na sms unaipata kumbe siyo kweli kuna jinsi wanafanya kwa kutuma sms tu na delivery report inakujia kwa staili ileile ya kutuma hela. ukiondoka tu wao wanasepa kumbe yule uliyemtumia hajapata wamekupiga changa la macho.

  mwanzo sikuamini ila yalipomtokea mfanyakazi mwenzetu ndipo nilijua kumbe hawa ni wezi. chunga sana hela za kwenye simu ni risk sana.

  na je hii ya nmb mobile, najua mtakuwa hamjaiskia ila uwe macho sana ukimtumia tu hela kwa njia ya cardless unajiwekea uwezo wa 90% kuibiwa kama unayemtumia ni mjanja
   
 13. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  tatizo wahusika wanachukulia kama jambo dogo kumbe linaweza kuwaharibia kibiashara
   
 14. D

  Dan Geoff P Member

  #14
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 25
  Tigo customer care hawajajua majukumu yao katika kuboresha huduma na kumpa kipaumbele mteja wake,,inawezekanaje matatizo kama hayo wayachukulie kizembe zembe tu bila kuchukua hatua stahiki kwa wahusika...binafsi nina imani kubwa kuwa wahusika wa hilo tukio ni wahudumu wenyewe wa tigo kwa sababu wao ndio wenye access na account ya mtu,,inawezekanaje mpaka password ya tigo pesa iwe imebadilishwa? Ni nani anayeweza kufanya hvo kama sio mhudumu wa kampuni...tiGo a boring network in Tanzania.
   
 15. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Du pole sana umenitisha ndiyo nilikuwa naelekea kwa wakala niweke kalaki na nusu cha kutuza ac.
   
 16. D

  Dan Geoff P Member

  #16
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 25
  Ha haaa umenifurahisha sana kurunzi...hako kalaki bora ukakachimbia chini tu kuliko kakaliwa na matapeli.
   
 17. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Tunashukuru kwa taarifa. Lakini hapo kwenye nyekundu umechemsha. Wizi huu upo mitandao yote ya SIMU na BENKI. Yaani hiyo ya tigo cha mtoto. Kuna watu wamelizwa mamilioni kwenye NMB MOBILE.Mind your words
   
 18. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mimi kuna kipindi nilikuwa naweka pesa kibao kwenye akaunti yangu ya Simu, kwasasa nimejiwekea utaratibu pesa zote zinakaa benki kwenye line vinakaa vihela mbuzi kama elfu50 ili kunisaidia kununua vocha na in case napigwa vimizinga vidogodogo au luku inaisha ghafla
   
 19. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,044
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180

  Naomba elimu zaidi juu ya hii kwani hilo ndilo kimbilio langu kwa sasa kutuma pesa kijijini kwetu
   
 20. hope 2

  hope 2 Senior Member

  #20
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, maelezo yako yako wazi na hatua zote ulizochukua umeziweka wazi.
  nakushauri nenda TCRA kutoa malalamiko yako hayo, kama una mda wafungulie kesi Tigo, naamini utashinda na utapata mshiko wako vizuri tu.

  ninachofahamu ni kwamba, hamna mtu anayeweza kufanya SIM swap kama sio muajiriwa wa tigo. na kama namba yako ilifanyiwa swap, kumbukumbu za transaction iliyofanyika zinakuepo na kampuni inaweza kuona wazi kwamba ni nani alifanya huo upuuzi.
   
Loading...