TAHADHARI: Mlipuko wa kipindupindu Sumbawanga

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Wakazi wa mji wa Sumbawanga watakiwa kuchukua taadhari juu wa ugonjwa wa mlipuko wa Kipindupindu ili kuepukana na madhara ya ugonjwa huo.

Watu zaidi ya Sita wanaripotiwa kuwa na ugonjwa huo na wamefikishwa katika hospitali ya mkoa wa Sumbawanga kwajili ya matibabu.

Serikali ya mji huo wa Sumbawanga imewataka wakazi wote wa mji huo kuchukuwa taadhari juu ya ugonjwa huo kwa Kunawa mikono yao kabla ya kula chakula na baada ya kula na
kufanya usafi wa mazingira.

Pia wameaswa kuwakataza watoto wao kucheza katika mitaro ambayo haitiririshi maji machafu (inayotuamisha maji) na tahadhari zinginezo kujikinga na Ugonjwa huo uliopo hivi sasa Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa.
 
kipindupindu ni rafiki wa wachafu, haiitaji kuchukua taadhari bali kujijengea mazingira ya usafi kila wakati
 
Back
Top Bottom