Tahadhari: Mlio kwenye ujenzi kuweni makini na mafundi

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,896
36,213
Habari za wakti huu wanajamii wenzangu.....

Bila shaka kuna ndugu zangu wapo kwenye ujenzi au kuna wengine wapo kwenye mipango ya kuanza ujenzi hivi karibuni....kama ilivyo kawaida kuwa katika kipindi cha ujenzi lazima tutawahitaji mafundi kwa namna moja au nyingine......

Sasa shida ipo kwa hawa ndugu zetu tunaowapa kazi ya kutujengea vibanda vyetu....wakati wewe unapiga hesabu za kuwahi kumaliza kibanda chako ili uhamie kwako uepukane na lawama za wenye nyumba yeye ndio anapiga mahesabu ya kutajirikia humo humo kwenye ujenzi wako.....

Bila shaka kila mtu mwenye kutarajia kuanza ujenzi lazima kutakuwa kuna makadirio aliyojiwekea......lakini wengi wao waliowakabidhi hizo site mafundi wamejikuta wakitumia bajeti mara mbili ya ile waliokadiria kutokana na wizi au utapeli wa hawa mafundi....

Angalizo usikubali kwenda kununua vifaa katika duka atakalo kuelekeza au ile siku mliyopanga kwenda kununua wewe ghairisha....nenda siku nyingine au kama ikiwezekana kama umepaelewa vizuri mtume mtu akaulizie bei kwanza.....

Nimewahi kushuhudia mtu mmoja anauziwa kitu cha elfu kumi....kwa shilingi elfu ishirini na tano.......kinachofuata hapo ni mwenye duka baadae kumtumia chake fundi au baadae fundi kwenda kuchukua mzigo wake huku wakikucheka ujinga........

Ndugu zangu mlio kwenye ujenzi muwe macho.....

NB; samahani kama nimemkwaza mtu kwenye uzi huu....lakini sikuwa na jinsi......
 
Tatizo watu wengi hawana muda au ujuzi wakujua ni vitu gani vinahitajika kwa shughuli gani.

Hivyo mwisho wa siku huishia kuwaamini mafundi au ndugu zao kwenda kuwafanyia manunuzi ya mahitaji yao.
 
Kweli mkuu mimi mwenyewe huwa nashangaa kabisa.....yaani anashindwa hata kufanya window shoping ya vifaa atakavyovihitaji kwenye ujenzi wake.....yaani mtu mpaka anapigwa cha juu hadi elfu kumi mtu hashtuki tu....
 
Jambo lingine ni sisi wenyewe kuaminishana kwamba ujenzi ni mgumu/gharama hasahasa pale kwenye umaliziaji (finishing) hivyo mtu anapopewa bei za juu kwakuwa kashaaminishwa hivyo anakubali tu.
 
Kweli mkuu mimi mwenyewe huwa nashangaa kabisa.....yaani anashindwa hata kufanya window shoping ya vifaa atakavyovihitaji kwenye ujenzi wake.....yaani mtu mpaka anapigwa cha juu hadi elfu kumi mtu hashtuki tu....
Hela yenyewe kapiga tu huko bandarini/tra unafikiri ana uchungu hata bei ikipandishwa mara mbili? Hela usipoitolea jasho wala huijali ukiambiwa bei unatoa tu bila kuhoji.
 
Habari za wakti huu wanajamii wenzangu.....

Bila shaka kuna ndugu zangu wapo kwenye ujenzi au kuna wengine wapo kwenye mipango ya kuanza ujenzi hivi karibuni....kama ilivyo kawaida kuwa katika kipindi cha ujenzi lazima tutawahitaji mafundi kwa namna moja au nyingine......

Sasa shida ipo kwa hawa ndugu zetu tunaowapa kazi ya kutujengea vibanda vyetu....wakati wewe unapiga hesabu za kuwahi kumaliza kibanda chako ili uhamie kwako uepukane na lawama za wenye nyumba yeye ndio anapiga mahesabu ya kutajirikia humo humo kwenye ujenzi wako.....

Bila shaka kila mtu mwenye kutarajia kuanza ujenzi lazima kutakuwa kuna makadirio aliyojiwekea......lakini wengi wao waliowakabidhi hizo site mafundi wamejikuta wakitumia bajeti mara mbili ya ile waliokadiria kutokana na wizi au utapeli wa hawa mafundi....

Angalizo usikubali kwenda kununua vifaa katika duka atakalo kuelekeza au ile siku mliyopanga kwenda kununua wewe ghairisha....nenda siku nyingine au kama ikiwezekana kama umepaelewa vizuri mtume mtu akaulizie bei kwanza.....

Nimewahi kushuhudia mtu mmoja anauziwa kitu cha elfu kumi....kwa shilingi elfu ishirini na tano.......kinachofuata hapo ni mwenye duka baadae kumtumia chake fundi au baadae fundi kwenda kuchukua mzigo wake huku wakikucheka ujinga........

Ndugu zangu mlio kwenye ujenzi muwe macho.....

NB; samahani kama nimemkwaza mtu kwenye uzi huu....lakini sikuwa na jinsi......
Ndugu yangu Ufundi ni Fani za watu akiamua kukuoiga hutoki acha kabisa.....Tena afadhali umpe Uhuru atakuonea huruma lkn akishtukia unaBANA utaumia sana ni ushauri tu
 
Ukiwa makini mbona freshi....sema walio na ujenzi wengi ni wale ma mwinyi...unakuta anamaliza miezi hatii mguu site....
 
Kweli mkuu mimi mwenyewe huwa nashangaa kabisa.....yaani anashindwa hata kufanya window shoping ya vifaa atakavyovihitaji kwenye ujenzi wake.....yaani mtu mpaka anapigwa cha juu hadi elfu kumi mtu hashtuki tu....
Ndugu yangu hakuna kwa kukimbilia, ukienda kununua mwenyewe wanazidisha mahitaji ya vitu ili vibaki wakauze kwa mjenzi au kulekule dukani ulikonunua.
 
Ni kweli, ila watu wanaojenga baadhi wamegundua mafundi wanaochelewesha kumaliza nyumba. watu wako tayari kugaramia mafundi kutoa mkoa 1 mpka kwenda mwingine wanajuwa kazi yao iliyowafikisha hapo watapiga kazi vizuri sana na kumaliza kwa wakati kuliko kuwapa kazi mafundi wa ilo eneo watakusumbua sana.
 
Adha kubwa nikuwa hawa jamaa huwa wana underestimate kazi ilikukuvuta uwape kazi ,kazi ikianza unaanzakuona gharama zinapanda oh unajuwa pale tulikosea kdg tuongeze material na bei ya ujenzi inaongezeka, mbaya zaidi kama ulimpa kazi kwa kutumia fomula ya percentage
 
KikulachoChako
Bro umenena ukweli mtupu nakumbuka nilipokuwa namjengea bi mother nilikwenda na fundi dukani kufika pale bahati nzuri mwenye duka tumekulia pamoja. Kitu nilichoulizia alinipunguzia bei akaniuzia kwa rahisi basi yule fundi akamfata mwenye duka akataka apewe hela ya kumleta mteja mwenye duka akamwambia yule ni kama mdogo wangu huoni hata bei niliomuuzia ya chini sana. Yule fundi alikasirika sana
 
Hivi unafikiri kujua bidhaa gani inapatikana wapi na kwa bei gani ni kazi rahisi?! Yaan umzungushe mtu juani hivi hivi kweli?! Hiko cha juu ni halali yao, hutaki nenda kazunguke mwenyewe upigwe bei Mara tatu yake ya hiyo anataja fundi
 
ujenzi ni shida!fundi anajenga ya kwake kutoka kwenye nyumba yako anayokujengea!
 
Hela yenyewe kapiga tu huko bandarini/tra unafikiri ana uchungu hata bei ikipandishwa mara mbili? Hela usipoitolea jasho wala huijali ukiambiwa bei unatoa tu bila kuhoji.
Kweli mkuu hela uliyoitafuta kwa jasho lako lazima uwe makini kwa kila senti inayotoka.....na huo ndio utaratibu wa kula kwa jasho.....

Alafu kibaya zaidi wakati wewe unajibana hata kunywa lager fundi mdio anakuwa anaongoza kufungua vizibo huko bar kwa kupitia ujenzi wako.......
 
Ukiwa makini mbona freshi....sema walio na ujenzi wengi ni wale ma mwinyi...unakuta anamaliza miezi hatii mguu site....
Hapana kaka akiamua kukuumiza Atakuumiza tu kutokana na kz zangu nakwambia hiyo kwa kumaanisha ujue wakati mwingine fundi anapoona hueleweki anakukomoa tu....mimi nadhani Ukiamua kujenga kwanza sivibaya kujua gharama halisi manake itasaidia kupunguza wizi lkn haitaondoa wizi kwa Fundi alidhamiria kukupiga
 
Hebu nipe experience yako fundi anakuibiaje maanake sasa hivi nipo kwenye finishing na huwa hajengi bila mimi kuwepo,naenda site jumamosi na jumapili tu tunajenga tulichopanga kikiisha au kikibaki site inafungwa kila mtu anaendelea na mambo yake mpaka weekend inayofuata. Nanunua kila kitu mwenyewe kutoka maduka ninayotaka mimi na quality ya vitu ninavyotaka mimi.
 
Suala la uaminifu kwenye maeneo ya kazi kwa watanzania wengi ni tatizo kubwa siyo dogo. Hapa wengi watawasema mafundi vibaya lakini ukifanya sensa ya hawa katika kazi zao utashangaa huko ni wapiga dili kupita kawaida.

Hata hivyo tupo mafundi wazuri, waaminifu na wenye maadili katika kazi. Na hata kazi zingine wapo. Tupo radhi kudhalauriwa na kuonekana wajinga kuliko kupoteza uaminifu na uadilifu.

Tunachekwa sana lakini hatuna mpango wa kuacha uaminifu. Uaminifu unalipa, unajenga heshima, unalinda utu na kuinua taifa.
 
Back
Top Bottom