Tahadhari Maradhi: kwa Dada zetu wa nyumbani (Wasaidizi wa kazi za Nyumbani)

Gentlemen_

Member
Nov 24, 2019
45
125
Habari zenu wakuu,

Kichwa cha Habari kinaweza kisieleweke mpaka mtu atakaposoma ndani kwa Umakini na Utulivu.

Ki kawaida tuna kasumba ya kutafuta wasaidizi wa kazi za nyumbani kwa njia za kirahisi kama KUAGIZA ndugu na jamaa zetu wa vijijini.. au kubadilishana wafanyakazi hawa kutoka nyumba fulan kumuunganisha nyumba nyingine kuendelea kufanya kazi na kujitaftia kipato chake na familia yake inayomtegemea.

Tanzania utamaduni wa kuchunguza AFYA kwa mfanyakazi wa ndani hilo swala halipo. Hata baadhi ya ofisi huwa kitengo cha rasilimali watu huwa hawazingatii Uchunguzi wa AFYA kiundani hivyo kuajiri wafanyakazi wagonjwa.

Sina Maana kuwa watu wenye kasoro ktk Afya zao wasifanye kazi HAPANA.

nachomaanisha ni Aina Ya Ugonjwa alionao na Aina ya kazi na kundi la watu anao wahudumia..

Turudi kwenye Mada iliyonyooka.

Kuna Mfanyakazi (wa Kike) aliajiriwa na kufanya kazi kwa muda wa wiki mbili alijitahid kufanya kazi zote na kwa weledi ila Afya yake haikuw nzuri kivile..

Boss wa Mfanyakazi huyo hakupendezwa na kasoro zile za Kiafya (vipele, kukohoa na uchovu) ilibidi afunge safari ampeleke Hospital iliyo karibu na eneo wanalo Ishi.

Badaa ya kufika na kupima Vipimo iligundulika Binti ana Shida ya kiafya (UTI pamoja na UKIMWI na upungufu wa damu) hali hii ilimshtua Boss ukizingatia ana watoto wadogo pale nyumbani na ndie Dada wa kazi pekee anayewahudumia/ aliyewahudumia kwa wiki mbili.

Maswali yalikuja kichwani je, watoto hawatakuwa exposed na UTI? Je, Ukimwi?! Wamechangia mengi ukianzia Choo Mpk Sehemu ya Kulala ingawa Kisayansi Ukimwi hauambukizwi hivyo.

Niende Mbali zaidi:
Kuna baadhi ya Sisi wanaume huwa tunatamaa na Wadada wa kazi.. hujui katoka wapi.. kapitia yapi mpk kaja hapo kufanya kazi ila TAMAA zinatuzidi na kulala nao kimwili hali inayotufanya TUZOE MARADHI yasio na tiba.

Pendekezo langu ni kwamba

Hawa Watu wanaotusaidia Kazi za Nyumbani ni Vyema KUWAPIMA AFYA ZAO. Kwanza kabla ya kuwakabidhi majukumu rasmi. Itasaidia kusalimisha familia zetu, hasahasa Watoto na baadhi ya watu wazima wenye tamaa za kimwili.

Pia Kujua Afya ya mfanyakaz wako inasaidia hata Kumchagulia kazi za kufanya na za kutofanya Mfano mtu ana ALLERGY / Mzio wa Vumbi.. huwezi kumpa kazi zinazohusisha Vumbi kwa wingi. Au utamsaidia vifaa vinavyokinga VUMBI kupenya kirahisi ikiwa ni lazima aifanye hiyo kazi.

Niwatakie Afya Njema!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Emmanuel Robinson

Verified Member
May 29, 2013
1,164
2,000
Mimi ilinitokea amefika tu kesho yake kaumwa wife kumpeleka akachonga na dr ampime ukimwi kwa siri ile wanamtoa damu kwenye mshipa mkubwa akshituka mbona mnanitoa huko dr akazuga kuja kutoa majibu positive. Kesho yake tukamwondoa yaani ni mtihani mkubwa sana
 

Jane Lowassa

JF-Expert Member
May 10, 2016
2,049
2,000
Ujinga mtupu. It only exposes your ignorance regarding means of transmission of HIV. Yaani unamfukuza mtu kwasababu ametest positive with HIV na unaogopa asiwaambukize.
 

Emmanuel Robinson

Verified Member
May 29, 2013
1,164
2,000
Ujinga mtupu. It only exposes your ignorance regarding means of transmission of HIV. Yaani unamfukuza mtu kwasababu ametest positive with HIV na unaogopa asiwaambukize.
Wewe ndiye mpumbavu kabisa mtu kama huyo unamwacha amhudumie mtoto wa miezi minne mitano. Hebu tufichie upumbavu wako huko
 

Trayvess Daniel

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
437
1,000
Wewe ndiye mpumbavu kabisa mtu kama huyo unamwacha amhudumie mtoto wa miezi minne mitano. Hebu tufichie upumbavu wako huko
Kabisa... na hapo hujui tabia zake, what if siku akaamua tu kukukomoa makusudi kuambukiza watoto kwa tofauti za kibinadamu? Mimi nilimpata mmoja na hakumaliza wiki nilimrudisha walificha hawakusema lakini katika pekua nikakuta vidonge
 

Emmanuel Robinson

Verified Member
May 29, 2013
1,164
2,000
Kabisa... na hapo hujui tabia zake, what if siku akaamua tu kukukomoa makusudi kuambukiza watoto kwa tofauti za kibinadamu? Mimi nilimpata mmoja na hakumaliza wiki nilimrudisha walificha hawakusema lakini katika pekua nikakuta vidonge
Huyo ni mjinga tu humu kuna watoto ambao hawajui hujuma za hao wadada maana hawajawahi hata kukaa nao kuna mmoja aliwahi kuwapigisha mswaki wake ili kuwakomoa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom