Tahadhari, manunuzi ya bidhaa kwenye mitandao! Kuwa makini yasije yakakukuta makubwa

Quarteman

Senior Member
Jul 31, 2016
129
169
Kama kichwa cha habari kinavyosema!

Jamani hii mitandao inayouza vitu online kama zoom, kupatana, kikuu, jumia, Kariakoo Mall na hata hapa JF twapaswa kuwa makini sana pale ununuapo bidhaa hasa simu, na bidhaa nyingine zinazofanana na hizo!

Ipo hivi, nilipigiwa simu na rafiki yangu hivi majuzi akanijulisha rafiki yetu mmoja kashikiliwa kwenye kituo fulani cha polisi na anatuhumiwa kwa wizi hivyo tukamdhamini. Kwa kweli nilishtuka kwa namjua rafiki yetu hana hizo tabia za wizi.

Basi nikafika kituoni na jamaa zangu wengine tukafanya michakato yote jamaa akatoka!

Turudi kwenye kisa chenyewe kilichomletea zengwe.

Mwaka jana huyu aliyewekwa ndani alikuwa na shida ya simu basi akashauriwa aingie online anaweza kupata simu anayoitaka kwa bei nafauu kiasi na akaletewa hadi alipo!

Kweli jamaa akaingia kwenye moja ya mitandao inayouza vitu online na kufanikiwa kupata simu aliyoitaka kwa bei poa tu, akaweka oda baada ya kuridhika na bei, baada ya siku kadhaa akaletewa mzigo hadi alipokuwa na biashara ikaishia hapo!

Akaedelea kutumia simu yake kwa miezi kadhaa, sasa hivi juzi ndio akajikuta chini ya vyombo vya usalama kwamba anamiliki simu ya wizi, na kwamba katika tukio hilo kuna vitu vingine viliibwa ikiwemo pc, aina nyingine tofauti za simu, na pesa!

Kwa bahati mbaya kidogo hakupewa risiti maana ile simu ilikuwa ni second hand na muuzaji alivyodaiwa risiti hakuitoa lakini mnunuaji huyu akaridhika tu(kama ilivyo kwa watu wengi kutochukulia maanani swala la risiti).

Ila kwa bahati ni kwamba chati za muuzaji jamaa alizitunza kuanzia wanakubaliana hadi analetewa mzigo, pengine huenda zikamsaidia huyu jamaa.

Kwa sasa bado upelelelezi unaendelea tunasubiri matokeo!

Lakini vile vile baada ya hili tukio kutokea nilipata taarifa kuwa pale kituoni kuna kesi zinazofanana na huyu rafiki yetu za kununua simu kwenye mtandao na kuzitumia kisha baada ya muda wakakamatwa kwa case hizo!

Hivyo hii mitando ni mizuri lakini kuna watu wasio waaminifu kabisa, tuwe makini!

Mimi huwa ni mdau wa kununua bidhaa online lakini kwa sasa hii mitandao ya kibongo inaelekea kuna wengi wameumia!

Nawasilisha.
 
Hii trick kwa second hand ipo sana, nunua kwa trusted sellers online apps kama Tunzaa na Swahilies
 
Alinunua kwa kupitia mtandao gani?
Mi nameazoea ya kununua toka 2020 , na bidhaa nakuta ikiwa mpya na imefungashwa vizuri.

Au alitumia wauzaji wa Instagram
 
Alinunua kwa kupitia mtandao gani?
Mi nameazoea ya kununua toka 2020 , na bidhaa nakuta ikiwa mpya na imefungashwa vizuri.

Au alitumia wauzaji wa Instagram

Soma vizuri, siyo instagram boss!

Kuna hii mitandao,zoom, jumia, kariakoo mall, kupatana n.k!

Ni mtandao ambao una app kabisa kati ya hiyo niliyoitaja!

Na ujue kwenye hii mitandao kuna bidhaa used, so aliona used akaona inamfaa akatoa oda akaletewa mzigo, akakagua akalipa baada ya kuridhika!

Na hili linafanyika na wengi tu!
 
Hii trick kwa second hand ipo sana, nunua kwa trusted sellers online apps kama Tunzaa na Swahilies

Tatizo mkuu si wote wanajua namna ya kifahamu trusted sellers app! Hizi app au sites zinazojulikana na wachache kwamba si trusted zinapata wateja pia!

Wapo wauzaji wanaotangaza bidhaa zao kote kote wanajua kwenye app flan ni trusted wanakuwa waaminifu huko, na upande mwingine wanajua kuna mianya ya kupiga so huko hawakosi wa kumpiga!
 
Back
Top Bottom