Tahadhari majangiri National Parks Tz, wajeda wa JWTZ wamekabidhiwa rungu

kinganola

Senior Member
Aug 16, 2011
117
30
Nashukuru sana serikali kwa kuamua kuwakabidhi JWTZ wakawashughulikie Majangiri, dawa yao imepatikana. Askari wanyama pori na maofisa wao, walikuwa wanakula dili na hawa majangili,tunayajua hayo.

Wakitaka hata meno ya Tembo, kwanza wanawatafuta hawa wahusika, wanawahonga then wanaingia mbugani na wanapewa hadi uelekeo upi waende kufanya huo ufirauni wao, wale waliongia bila kuwahonga, ndio huwa mnajidai mnawasaka, kwendeni huko, ndio maana mmetajirika na kuwekeza mali za mamilioni huku mijini.

Sasa Wa Jeda JWTZ hawahongeki kizembe, mkijipendekeza tu mmekwisha, watawafanya bucha nawambia, mmetumalizia wanyama wetu, inasikitisha mlimuua hadi faru anayejulikana dunia nzima na alipelekwa Sauzi akakulie huko, amerudi mmemuuwa pamoja na kufungiwa kifaa cha GPS.
 
Wasiwasi wangu hata hao JWTZ wataathirika na huo mkumbo, hakuna mtanzania asie na njaa bwana na wala hakuna mwenye uchungu na mali za Tanzania.
 
wasiwasi wangu hata hao jwtz wataathirika na huo mkumbo, hakuna mtanzania asie na njaa bwana na wala hakuna mwenye uchungu na mali za Tanzania.
hata mimi huo ndio wasiwasi wangu....hakuna asiyependa hela....hivi ile ishu ya yule faru iliishia wapi? kwa anayejua tafadhali
 
Unajua, ili uweze kuhonga, lazima utumie muda/wa kutosha kutengeneza network, mpaka waje wajipange, cha moto watakuwa wamekiona, Hawa jamaa hawajuagi cha protocal wala kesi mahakamani, wanamaliza wenyewe, nini kitaendelea, mimi sijui, ila watakao naswa,shauri yao.
 
wasiwasi wangu hata hao jwtz wataathirika na huo mkumbo, hakuna mtanzania asie na njaa bwana na wala hakuna mwenye uchungu na mali za Tanzania.

hayo ni kweli kabisa hata wao muda si muda mambo yatarudi pale pale mfano kuna eneo la kati ya mikumi na kidatu huwa kuna kikosi maeneo hayo na mara nyingi huwa kuna matukio ya magari kuvamiwa na kuporwa, watu husema ni wao huwa wanahusika sana na vitendo hivyo na pale kwa wanaoijua hiyo njia huwa si salama kabisa kupita hasa kuanzi saa 2 uck ni hatari sana.
 
Hata wakae macomandoo wa Obama kazi bure, waarabu na wazungu wanawapakia wanyama mchana kweupee si bora watanzania nao wanufaike hata kimaskini
 
Wajeda watawapiga sana warina asali na wawindaji wenyeji hasa wa mitego ya nguchiro na digidigi. Isitoshe kwenye maeneo waliyopewa wazungu na waarabu huko hawatii pua, ambako kuna hadi viwanja vya ndege maalum. Kubwa zaidi wanyama wetu na maliasili zetu zinapitia ktk viwanja vyetu vya ndege tunavyovijua bayana. Kifupi hawana jipya hao wajeda. Wanajua wanapoanzia na kuishia.

Ovyo kabisa mipango yetu jamani... Looh!
 
unajua,kuna sheria ya uuzwaji wanyama pori hai,sasa hawa mabwana wanatumia mwanya huu,any way hiyo siyo ishu,sasa hivyo viwanja vya ndege vilivyopo porini,nani anavi monitor?,mbona kama tunaibiwa kweupe?,na hawa jamaa ukiwakuta,wanavibali na ukijichanganya,wanakupa za chembe,wanapanda flight,wanasepa.
 
Hii nchi imelaanika badala ya kufikiria njia za kuokoa rasilimali za taifa mnampelekea ulaji zaidi S.h.i.m.b.o hahahaha sikio la kufa
 
Kama ni kweli basi nayo ni hatua, ila kama mnavyosema kila mtanzania sasa haaminiki sababu ni kiongozi mkuu / viongozi wakuu kujihusisha na wizi,rushwa na ukwapuaji kuanzia kura hadi raslimali, sasa nani aache??????!!!!!!! Watu wenye hofu ya MUNGU pekee yao.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hata hao JW wana njaa sasa yakitokea mapambano ndo utasikia. Selous game reserve kuna wasomali wanawinda swala wanauza nyama uarabun. Serikali legelege.
 
wasiwasi wangu hata hao jwtz wataathirika na huo mkumbo, hakuna mtanzania asie na njaa bwana na wala hakuna mwenye uchungu na mali za Tanzania.

Sijui ni bahati mbaya ama nzuri lakini zamani raia walikuwa wazalendo kutokana na imani kuwa hali ni ngumu kwa wote so let us be faithfull; maana viongoi walipodokoa nyama jikoni hapo siku za nyuma kabla hazijatengwa jikoni watoto walikua hawapati habari na hata walipokuwa wanakula maharage monday to monday waliona ni sawa tu kwani waliamini siku moja itakuwa YES! lakini siku hizi kutokana na technology na evolution kwenye ICT basi huwezi danganya mtu story za uzalendo wakati wakubwa wanakomba mboga jikoni. Ni vigumu kwa raia wakawaida kuvumilia kutunza mali ya pamoja huku kikiwa na mifano ya wakubwa kukwapua mabilioni ya public funds bila kuchukuliwa hatua zozote zaidi ya kusafishwa na kamati za uchunguzi.

Itapofika hatua kila mtu akataka ku exercize muscles zake apate kula naye ndiyo tutajua Somalia was once a gud nationa; Mungu epusha hii balaa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom