Tahadhari kwa watu wanaonunua viwanja au mashamba Kibaha hasa kata ya Visiga

J33

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
1,552
1,512
Nimeona nianzishe uzi huu ili kuwasaidia watu wanaotaka kununua naeneo au viwanja hapa Kibaha. Kuna magenge ya na tapeli ambao wanatafuta wateja Dar na kuwaleta kuwauzia mashamba ya watu wengine na mbaya zaidi wanauza mashamba hayo kwa watu zaidi ya mmoja(yani unauziwa leo na kesho eneo hilo hilo anauziwa mtu mwingine).

Mbinu kubwa wanayotumia ni kuuza kwa bei ndogo sana ili kuvutia wateja. Wamejipanga vizuri na ukiwakuta wanakuwa na viongozi fake pamoja na mihuri yote ya serikali na wakati mwingine wanaweza kukuletea hata bibi mzee sana aonekane ndio mwenye shamba ili kuwaaminisha wateja.

Wana kesi nyingi police lakini mara zote wanunuzi ndio wanaoumia kwa sababu wanauzia watu wengi kwa pamoja kwa hiyo migogoro mikubwa inabaki kwa wanunuzi ambao nao baadae hujikuta eneo sio la kwao wote.

USHAURI. Ukinunua eneo huku hakikisha anayesimamia uandikishwaji ni mtendaji wa Serikali kwa kuangalia vitambulisho vyake, Pili hakikisha baada ya kukagua eneo maandaishi na makabidhiano ya pesa yanafanyika ndani ya Ofisi ya Serikali ya mtaa.

Mwisho kwa wale wenye mashamba tayari hakikisha unajenga hata kibanda na muda wote shamba au kiwacha kinasafishwa na kulimwa hata Mihogo.
 
Back
Top Bottom