Tahadhari: Kwa watafuta ajira usijaribu kuomba wala kufanya kazi hospitali hizi jijini Mwanza

Wakuja waje

Member
Nov 14, 2020
24
75
Habarini wanajukwaa

Naomba nijikite kwenye mada yangu.

Pengine kutokana na ukosefu wa ajira,kama mtanzania mwenzenu ambae kwa nyakati tofauti nimewahi kuwa katika mkoa wa Mwanza kikazi kama mkaguzi wa maswala ya afya,nimekutana na kisanga cha ubabaishaji na usumbufu kwa baadhi ya hospital za watu binafsi mkoani humo.

Natoa tahadhari ya kwamba ukiomba kazi katika hospital hizi tambua unajitolea la sivyo utapata msongo wa mawazo!

1. HURUMIA WATOTO HOSPITAL
Hospital hii ipo mtaa wa kilelu-Mabatini.

Ni hospital nzuri yenye miundombinu ya kisasa.

Hii hawalipi kabisa mishahara, ukiajiriwa watakubali kiasi chochote cha mshahara ukibahatika utalipwa nusu au awamu moja baada ya hapo hesabu maumivu.

Mabingwa wa kubadili wafanyakazi maana hakuna mtu huvumilia usumbufu, matokeo yake hospital hii imekimbiwa na wagonjwa na iko kwenye mwelekeo wa kujifia.

Hakuna mfanyakazi mwenye mkataba.

2. ALJUMAA HEALTH CENTRE MWANZA
Kituo kidogo katikati ya soko kuu la mwanza la zamani kwenye jengo la msikiti wa Ijumaa.

Hospital ina miundombinu bora sana....iko equipped vizuri sana,inazo mashine za kisasa na vifaa bora sana nadiriki kusema moja ya hospital yenye vitu vizuri sana iko kwenye top 3 ya hospital zenye vifaa vya kisasa kwa mkoa huo.

Pamoja na sifa nzuri nilizotaja hapo juu,kituo hiki kina shida ya uongozi.

Kila kukicha wanabadili wafanyakazi na mshahara ni mpaka maombi,inachukua zaidi ya miezi 2 au 3 wafanyakazi kulipwa

Kazi ya kituo hiki sio guarantee ni kama vibarua tu

Hakuna mfanyakazi mwenye mkataba kama utakuta mkataba ni ubabaishaji tu

Wafanyakazi kituo hiki hawana likizo wala day off!

Iko kwenye mwelekeo wa kujifia.

3. UHURU HOSPITAL
Ipo mtaa wa uhuru karibu na mtaa maarufu wa mlango mmoja.

Moja ya hospital bora sana mwanza ikiwa na miundombinu safi na ya kisasa.

Shida kubwa ni uongozi na mmiliki kua mbabaishaji

Inabadili wafanyakazi kama mvua na mishahara haieleweki wafanyakazi njaa kali

Sio sehemu salama kwa mtafuta ajira

Iko kwenye uelekeo mbaya kama mmiliki wake hatabadirika.

Mikataba hakuna

4. SALAAMAN HEALTH CENTRE MWANZA
Ipo mtaa wa mission karibu na njia panda ya bugando jirani na msikiti wa wahindi ule mweupe.

Kituo kizuri kiasi chake.

Kina tatazo la uongozi

Wanafukuza wafanyakazi kila kukicha, kufanya kazi kituo hiki unatakiwa uwe mvumilivu kuliko uvumilivu wa AYUBU!

Mshahara wanatoa nusu nusu, mfano leo utapewa laki kesho laki 2 baada ya wiki watamalizia

Hawatoi mkataba na wanafukuza na haupati haki yako popote

Usumbufu kwa wafanyakazi umepelekea kukosa wateja.

Mwelekeo wake ni kujifia.

5. STAR MED CARE
Ni dispensary ipo mtaa wa mabatini kama unaelekea shule ya msingi mabatini.

Uongozi ndio changamoto,hali inayopelekea kazi kuharibika matokeo yake kukosa mishahara.

Hizi ni baadhi ya hospital sumbufu sana na si salama sana kwa mtafuta ajira.

Usiku mwema!
 
KuSagiana kunguni
Sema inabidi warekebishe mifumo ya uongozi ...unamfanyishaje mtu kazi siku 60 au 90 hujamlipa ili hali wewe unaingaiza huo ni unyonyaji na ukoloni tulioupiga vita...kama hujawahi kucheleweshewa mshahara huwezi kujua uchungu wake...hospitali ni moja ya biashara zinazoingiza kwa sana pesa...maana faida ya dawa moja ukimuuzia mgonjwa ni kama mara tatu ya bei uliyonunulia hizi private zinapiga pesa ya kutosha...bado ma surgery,bado ma charge ya kulaza wagonjwa....yaani huku kwenye biashara ya afya ni hela kwa hela mzee haiwezekani ukashindwa kulipa wafanya kazi kwa siku 30.
 
Habarini wanajukwaa.

Naomba nijikite kwenye mada yangu.

Pengine kutokana na ukosefu wa ajira,kama mtanzania mwenzenu ambae kwa nyakati tofauti nimewahi kuwa katika mkoa wa Mwanza kikazi kama mkaguzi wa maswala ya afya,nimekutana na kisanga cha ubabaishaji na usumbufu kwa baadhi ya hospital za watu binafsi mkoani humo.

Natoa tahadhari ya kwamba ukiomba kazi katika hospital hizi tambua unajitolea la sivyo utapata msongo wa mawazo!

1.HURUMIA WATOTO HOSPITAL

Hospital hii ipo mtaa wa kilelu-Mabatini.

Ni hospital nzuri yenye miundombinu ya kisasa.

Hii hawalipi kabisa mishahara,ukiajiriwa watakubali kiasi chochote cha mshahara ukibahatika utalipwa nusu au awamu moja baada ya hapo hesabu maumivu.

Mabingwa wa kubadili wafanyakazi maana hakuna mtu huvumilia usumbufu,matokeo yake hospital hii imekimbiwa na wagonjwa na iko kwenye mwelekeo wa kujifia.

Hakuna mfanyakazi mwenye mkataba

2.ALJUMAA HEALTH CENTRE MWANZA

Kituo kidogo katikati ya soko kuu la mwanza la zamani kwenye jengo la msikiti wa Ijumaa.

Hospital ina miundombinu bora sana....iko equipped vizuri sana,inazo mashine za kisasa na vifaa bora sana nadiriki kusema moja ya hospital yenye vitu vizuri sana iko kwenye top 3 ya hospital zenye vifaa vya kisasa kwa mkoa huo.

Pamoja na sifa nzuri nilizotaja hapo juu,kituo hiki kina shida ya uongozi.

Kila kukicha wanabadili wafanyakazi na mshahara ni mpaka maombi,inachukua zaidi ya miezi 2 au 3 wafanyakazi kulipwa

Kazi ya kituo hiki sio guarantee ni kama vibarua tu

Hakuna mfanyakazi mwenye mkataba kama utakuta mkataba ni ubabaishaji tu

Wafanyakazi kituo hiki hawana likizo wala day off!

Iko kwenye mwelekeo wa kujifia.

3.UHURU HOSPITAL

Ipo mtaa wa uhuru karibu na mtaa maarufu wa mlango mmoja.

Moja ya hospital bora sana mwanza ikiwa na miundombinu safi na ya kisasa.

Shida kubwa ni uongozi na mmiliki kua mbabaishaji

Inabadili wafanyakazi kama mvua na mishahara haieleweki wafanyakazi njaa kali

Sio sehemu salama kwa mtafuta ajira

Iko kwenye uelekeo mbaya kama mmiliki wake hatabadirika.

Mikataba hakuna

4.SALAAMAN HEALTH CENTRE MWANZA

Ipo mtaa wa mission karibu na njia panda ya bugando jirani na msikiti wa wahindi ule mweupe.

Kituo kizuri kiasi chake.

Kina tatazo la uongozi

Wanafukuza wafanyakazi kila kukicha,kufanya kazi kituo hiki unatakiwa uwe mvumilivu kuliko uvumilivu wa AYUBU!

Mshahara wanatoa nusu nusu,mfano leo utapewa laki kesho laki 2 baada ya wiki watamalizia

Hawatoi mkataba na wanafukuza na haupati haki yako popote

Usumbufu kwa wafanyakazi umepelekea kukosa wateja.

Mwelekeo wake ni kujifia.

5.STAR MED CARE

Ni dispensary ipo mtaa wa mabatini kama unaelekea shule ya msingi mabatini.

Uongozi ndio changamoto,hali inayopelekea kazi kuharibika matokeo yake kukosa mishahara.

Hizi ni baadhi ya hospital sumbufu sana na si salama sana kwa mtafuta ajira.

Usiku mwema!
Kwahiyo kwa Kukosa Kwako Ajira Kote huko ndiyo kwa Hasira zako umeamua uje JamiiForums Kuwachafua?

Yaani inaingia Akilini kweli Wewe Mtu Mmoja uyajue Mapungufu yao ( hizi Taasisi / Zahanati / Hospitali ) zote halafu Serikali yenye Mkono mrefu kupitia Wizara na Taasisi zake Nyeti wasijue?

Inaonyesha una Majungu na Mswahili.
 
Ameshasema yeye ni mkaguzi!
 
Back
Top Bottom