white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,561
- 13,753
Napenda kutoa tahadhari wa wasafiri watumiao barabar ya dsm to bk, kuna sehemu panitwa runazi zile samaki zinazouzwa pale nyingi si salama kwa binadamu, juzi nikiwa kwenye basi la OTA, mdada ambaye ni kondakta wa Bus hilo alinunua samaki mmoja na kuanza kula tukiwa safarini, e bwana tumefika maeneo ya ushirombo dada akaanza kulalamika kuumwa tumbo mala akaishiwa kabisa nguvu!! Na kuanza kutetemeka vibaya!! Ikabidi tumpeleke hadi hospital moja mjini kahama, vipimo vya awali ikaonekan kama kuna sumu ikabidi tumuache hapo sisi tuendele na safari ya kuja dar. Kwanza wale samaki wa kukaangwa nje huwa wanaonekana wameiva vizuri mno ila ndani ni Ni wabichi kabisa hivyo kuweni makini sana kwani kwa hali aliyokuwa nayo yule dada ilitutisha sana ikabidi sasa dreva awashe hazards, gari lilikuwa kama ambulance!!! Kumbe spidi 110 kwenye bus ni balaa!! Chukueni taadhari sana jamani.