Tahadhari kwa wapenda kula matunda wote, juweni kuna homa ya ini

kendy

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
224
500
Katika kula tunda,
kuna kuanza kwa kula denda,
kulamba chumvi,
kulamba dushe,
na hatimae kula tunda,
na katika kula tunda kuna kutoka jasho,
na mwisho kabisa kuna kumwaga majimaji kwa wote wawili.
Tangazo ni hili,
hivi sasa kuna homa ya INI,
hii huambukizwa kwa kugusana ama kuachiana majimaji yamtokayo mtu mweye wadududu wa homa ya ini,majimaji ya aina yeyote.
Tunashauriwa kupima na chanjo ipo,
inasemekana dawa wanazotumia wagonjwa wa homa ya ini ni dawa za HIV.
Wataalamu wa Afya watafafanua zaidi ,tuchukue tahadhari
asanteni kwa kunisikiliza.

MAELEZO YA WATAALAMU.

Ini ni kiungo muhimu sana ndani ya miili yetu, hufanya kazi zaidi ya 500 ; moja ya kazi ni kuchuja na kuondoa sumu kutoka kwenye damu.

Kutokana na sababu mbalimbali kama pombe iliyopita kiasi, sumu kwenye damu au maambukizi; ini hupata shida na kuvimba na kushindwa kufanya kazi vizuri. Hii hali huitwa HOMA YA INI au HEPATITIS.

Katika maeneo yetu, bara la Afrika maambukizi ya virusi wa Homa ya ini ndio sababu kuu ya shida kwenye ini. Virusi vya Homa ya ini vipo vya aina 5 (A,B,C,D,E).

Aina mbili za virusi (B na C ) ndio sababu kuu za ugonjwa wa homa ya ini na husambaa kupitia damu na majimaji ya mwili.

Homa ya ini ni sawa janga linaloua kimya kimya kulingana na takwimu za vifo za dunia inakadiriwa Kirusi cha homa ya ini aina ya B pekee huua watu 600,000 hivi kila mwaka.

Kwa wastani zaidi ya watu bilioni mbili, yaani, asilimia 33 hivi ya watu wote ulimwenguni, wameambukizwa virusi vya HBV, na wengi wao hupona baada ya miezi michache. Watu milioni 350 hivi huendelea kuwa na virusi hivyo mwilini, wengi huishi bila dalili na kuendelea kuambukiza watu wengine


NAMNA GANI UNAWEZA KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA HOMA YA INI (B NA C)…….?
Virusi vya homa ya ini B na C husambaa kupitia damu, shahawa au maji maji mengine ya mwili.
Virusi hivi vina uwezo wa kusambaa na kuambukiza mtu mara 100 zaidi ya virusi vya UKIMWI.
Njia hizi husambaza virusi hivi vya homa ya ini..:
  1. Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
    ➡Mama aliye na maambukizi ya Hepatitis B kumuambukiza mtoto wakati wa kujifungua, iwapo hamna juhudi za kitiba za kuzuia maambukizi kuna uwezekano hadi asilimia 90 kwa mama kumuambukiza mtoto.
  2. Kufanya mapenzi na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya homa ya ini
  3. Kuchangia vifaa vyenye ncha Kali kama sindano hasa kwa watumia madawa ya kulevya au wachora tattoo, miswaki
  4. Kuongezewa damu ambayo ina maambukizi ya homa ya ini.
Virusi vya homa ya ini vinaweza ishi nje ya mwili kwa muda mrefu…
Tafiti zinaonyesha virusi vya homa ya ini vinaweza ishi nje ya mwili hadi kwa muda wa siku 7, bado vikiwa na uwezo wa kuambukiza mtu. Tafiti zimeonyesha hata iliyokauka huwa na uwezo wa kuambukiza virusi hivi.

JINSI UNAVYOAMBUKIZWA:
Katika maeneo hatari zaidi duniani, Virusi vya Hepatitis B (HBV) kwa kawaida husambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine hususan nyakati za utotoni.
Kama ilivyo kwa Ukimwi, Virusi vya Homa ya Ini pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate, jasho na mwingiliano wowote ule wa damu.
Njia kuu za maambukizi :
-Kujamiana bila kinga
-Kunyonyana ndimi 'denda'
-Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua
-Kuchangia damu isiyo salama
-Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kuchangia miswaki
-kuchangia taulo na mwenye ugonjwa huo
-kubadilishana nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho.
Tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa virusi hivyo ni hatari kuliko hata vya Ukimwi kwa sababu vinaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu (yaani nje ya mfumo wa damu) kwa siku saba. Virusi vya Ukimwi (VVU) havina uwezo wa kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika moja.
Kutokana na usugu wa HBV, maana yake ni kwamba kama kirusi kipo kwenye ngozi, kitaendelea kuwa hai kwa siku saba na katika kipindi hicho mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya damu au jasho.
Kwa wastani kirusi cha HBV kikishaingia mwilini, hupevuka ndani ya siku 75, hata hivyo upo uwezekano wa kupevuka kati ya siku 30 hadi 180. Ndani ya siku 30 mpaka 60, mtu mwenye HBV anaweza kugundulika ikiwa atapimwa.
Mtu mwenye Homa ya Ini ana wastani mdogo wa kuishi kuliko mwenye Ukimwi. Kwa maana hiyo, mwenye maambukizi ya Virusi vya Homa ya Ini hufariki dunia haraka kuliko mwenye VVU.
DALILI ZA UGONJWA HUU:
Watu wengi hawaonyeshi dalili yoyote. Kwa maana hiyo mtu anaweza kuishi na HBV na kusababisha maambukizi kwa wengine bila kugundulika.
Hata hivyo, watu wengine husumbuliwa na homa kali na dalili ambazo hudumu kwa wiki kadhaa.
Dalili hizo ni:
-Uchovu
-Kichefuchefu
-Mwili kuwa dhaifu
-Homa kali
-Kupoteza hamu ya kula
-Kupungua uzito
-Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
-Macho na ngozi kuwa vya njano
-Mkojo mweusi
Kwa wagonjwa wengine, Virusi vya Hepatitis B hukua hadi kusababisha ini kuharibika kabisa (cirrhosis of the liver) au saratani ya ini (liver cancer).
KINGA:
-Chanjo
-Kutumia kinga wakati wa kujamiana
-Kuacha kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kutochangia miswaki
-Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
-Kutochangia damu isiyo salama
KUNDI LIPI NI HATARI ZAIDI?
Asilimia 80-90 ya watoto wachanga ambao huambukizwa katika kipindi cha mwaka wa kwanza tangu kuzaliwa, Homa ya Ini hukua mpaka kufikia kuwa sugu na hatimaye kifo.
Asilimia 30-50 ambao huambukizwa kabla ya kufikisha umri wa miaka sita, Hepatitis B hukua mpaka kuwa sugu na baadaye ni kifo.
Asilimia 90 ya watu wazima wanaopata HBV, virusi hivyo hutoweka ndani ya miezi sita. Yaani uimara wa ini husababisha virusi hivyo kupotea.
Asilimia tano kushuka chini ya watu wazima wanaopata maambukizi ya HBV, virusi hivyo vya Hepatitis B kugeuka sugu na hatimaye kifo.
Asilimia 15-25 ya watu wazima ambao walipata maambukizi utotoni na hatimaye Hepatitis B kuwa sugu, hufariki dunia kutokana na matokeo ya ini kuharibika kabisa au kwa saratani ya ini.
TIBA YAKE:
Mpaka sasa Homa ya Ini haina tiba, Ugonjwa huo ukishafikia kiwango cha ini kuharibika au kupata saratani ya ini, maana yake kinachofuata ni kifo.
SULUHISHO NA TIBA LISHE:
Kutokana na tatizo hili kuwa ni kubwa, tafiti zimefanyika na kupatikana tiba lishe ambazo zitafaa kutumiwa.
Tiba lishe hizi,
: Ni natural antibiotics ambazo husaidia kuua bacteria na virus , Lakini pia husaidia katika kuimarisha kinga ya mwili
.Pia husaidia katika kuondoa Maumivu na kuongeza uzalishaji wa seli katika mwili
. Huupa mwili nguvu
.Huongeza virutubisho katika mwili na kujenga afya bora ya mwili.
.Huongeza kinga ya mwili na kuondoa changamoto ya magonjwa nyemelezi.
Tiba lishe hizi zina vitamins mbalimbali, Madini mbalimbali, Virutubisho vitokanavyo na mbogamboga na matunda,Proteins,Amino acids na fiber
Virutubisho hivi ni muhimu sana katika kuimarisha kinga ya mwili.
Kwa elimu zaidi/ ushauri/ au upataji wa virutubisho hivyo wasiliana nasi kwa namba:
+255716789967
+255755928588
Tunapatikana
DAR ES SALAAM.
Lakini pia Ofisi zetu zipo pia Mikoani. (MBEYA,DODOMA,MWANZA NA ARUSHA.
WAWEZA JIUNGA KATIKA GROUP YETU YA WHATSAPP KWA ELIMU ZAIDI.
https://chat.whatsapp.com/JYvRmDFPKmi36KLWpFtS9d
Image may contain: food
 

kendy

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
224
500
Aisee magonjwa yametuzunguka hata hujui ujikinge na lipi.
Hebu fikiria unapomla denda au kuliwa denda na mgonjwa wa Homa ya INI,maana yake unawala wadudu kiulaiiiini,fikiria inaambukiza kwa jasho,vipi majimaji mengine?
 

Jang-Bogo

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
3,146
2,000
kumbe unayazungumzia matunda hayo ya kimasihara!!!!!!!!!!!!!!!
nikajua matunda like maembe (my favourites) yanasababisha haya maugonjwa ..

sisi watumiaji wa daladala sijui tutaponea wapi maana ikisha kula lundo tunavyomwagiana japo na tunagusana ngozi kwa ngozi nadhani Mungu itabidi ndio awe msimamizi wetu.maana hakuna namna.

hayo matundo mengine tunawaachia wenyewe maana umeonyesha na ubobezi wa kuyala kwa kutupa hints za procedure fuatwa.
ahahahahahahahaha
 

kendy

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
224
500
kumbe unayazungumzia matunda hayo ya kimasihara!!!!!!!!!!!!!!!
nikajua matunda like maembe (my favourites) yanasababisha haya maugonjwa ..

sisi watumiaji wa daladala sijui tutaponea wapi maana ikisha kula lundo tunavyomwagiana japo na tunagusana ngozi kwa ngozi nadhani Mungu itabidi ndio awe msimamizi wetu.maana hakuna namna.

hayo matundo mengine tunawaachia wenyewe maana umeonyesha na ubobezi wa kuyala kwa kutupa hints za procedure fuatwa.
ahahahahahahahaha
Kapime kama huna pata chanjo.kwa aliyenao ataanza dozi.Kula tunda kimasihara kuna raha yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom