Tahadhari kwa wanaume: Adaiwa kufa kwa kunywa viagra | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari kwa wanaume: Adaiwa kufa kwa kunywa viagra

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kapwani, Jun 2, 2010.

 1. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wana jamii forum wenzangu nathamini sana michango yenu na ninajua ina umuhimu mkubwa katika taifa letu....ngoja niwashauri tu jambo moja...mimi ni dada na si kaka tafadhalini tafadhalini epukeni vifo vya jinsi hii kama mambo hayaendi mrudie mola wako atayakamilisha busta busta inaua! kwani hamuwezi kuwa wapole tu kama mambo hayako sawa sana?
  na huyu dada aliyekuwa nae sijui alimuona akinywa hizo dawa? jamani kina dada wenzangu dume linapokunywa dawa, tena ana over dose au yeye ndiye aliemshauri aovadozi? huwezi kumshauri aaache? mmmmh duniani kuna mambo
  Mix with yours
  Adaiwa kufa kwa kunywa 'Viagra'
  Send to a friend Tuesday, 01 June 2010 23:24 0diggsdigg

  Moses Mashalla, Arusha

  MJI wa Arusha mwishoni mwa wiki ulizizima baada ya kutokea habari za kifo cha kutatanisha cha mkazi wa Levolosi, Omari Salim, 44, aliyefariki dunia wakati akipelekwa Hosptali ya Mt Meru baada ya kuzidiwa akiwa nyumba ya wageni na mpenzi wake.

  Tayari Jeshi la Polisi mjini hapa limeshathibitisha kutokea kwa tukio hilo, lililoibua maswali mengi kwa wakazi wa mjini hapa. Polisi imedai uchunguzi wa awali umebaini kifo cha marehemu huyo kimetokana na utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu za kiume.

  Polisi imezitaja dawa hizo kuwa ni aina ya Muco zilizokutwa ndani ya chumba alichokodi kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni.

  Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, Akili Mpwapwa aliiambia Mwananchi kuwa Mei 26 majira ya saa 8;30 Salim alimpigia simu mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la Caren Isaack, 20, ili wakutane. Alisema wote kwa pamoja walikubaliana na kwenda kukodi chumba katika nyumba ya kulala wageni ya Rhino.

  Alisema baada ya wapenzi hao kuwasili ndani ya chumba hicho, mpenzi wake alimwambia Salim kuwa wapande kitandani kwa lengo la kufanya mapenzi, lakini marehemu alilalamika kuwa alikuwa akijisikia vibaya na ndipo alipoomba kwenda bafuni kuoga.

  Kwa mujibu wa Mpwapwa, marehemu aliingia bafuni kuoga, lakini ghafla alitoka akiwa ameshika taulo mkononi huku akitetemeka, ndipo mpenzi wake alipopatwa na mshangao.

  Alidai kuwa kadiri muda ulivyokuwa ukienda, ndivyo hali ya Salim ilivyozidi kubadilika na ndipo akaamua kumbeba na kumweka kitandani na baadaye kumfunika shuka, lakini ghafla akaanza kutapika mfululizo.

  Kamanda Mpwapwa alifafanua ya kuwa Caren alilazimika kuomba msaada kwa mlinzi wa siku hiyo ndipo walipofanikiwa kumtoa chumbani na kukodi teksi kumuwahisha hospitalini, lakini akakata roho wakiwa wakiwa njiani.

  Alidai ya kuwa jeshi la polisi lilikuta vidonge mbalimbali vya dawa zinazosadikiwa kuwa ni za kuongeza nguvu za kiume zilizokuwa katika pakiti na kwamba huenda Salim alimeza vidonge hivyo kabla ya kushiriki ngono.

  Kamanda Mpwapwa alisema polisi wanamshikilia Caren kwa uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Na viagra yenyewe ndo iwe imenunuliwa pale Buguruni kwa mnyamani!
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  huko siiiikoooo
   
 4. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mama mia
   
 5. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heading siyo nzuri, wanaume wa jf ndo nanani sanaa, lbd ungesema "tahadhari kwa wanaume"
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Jun 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Hata General Sani Abacha naye alikufa kwa viagra akiwa na malaya wa kihindi aliyekuwa ameletwa kutoka India kwa ajili cha "Mzee."
   
 7. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasemekana hata baadhi ya watu maaarufu hapa TZ walikufa kwa viagra! hivi watumiaji wanakuwa wamepatwa na nini hata wanaamua kuongeza nguvu na viagra? nguvu imepungua ( ni kweli imepungua au kisaikolojia zaidi?...) au anataka kuonyesha umahiri zaidi na je hakunaga kipimo kiasi cha watu kuzidisha kila mara hado kufa....kama dozi ya ALU ni dawa nne kwa siku tatu,....viagra haina fomula?
  mix with yours
   
 8. PoliteMsemakweli

  PoliteMsemakweli Member

  #8
  Jun 6, 2010
  Joined: Nov 21, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Viagra nzuri ni hii: Usinywe pombe. kula chakula kizuri chenye mchanganyiko wa mboga za majani, matunda, nk. chukua muda kuongea na mpenzi wako mambo ya kufurahishana na hautakuwa na haja ya madawa kama viagra......
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Huyu si PakaJimmy? RIP
   
 10. Kijuso

  Kijuso Senior Member

  #10
  Jun 16, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 161
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Bwana Kichuguu wewe una ushahidi gani kuhusu huyo Sani Abacha kama alikufa na Viagra? Acha mdomo kama kitu hujui!!!!!TUPE USHAHIDI!!!!!!!!!!
   
 11. bona

  bona JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  hii kitu inamadhara na unaweza kufa kwa wale ambao hawana matatizo haya ila wanataka kuongeza cjui ni ktk mazingira ya ''kumkomesha'' mtu! uyo dada ni baamedi inaonekana jamaa alitaka kumkomesha labda kabla hawajaenda labda alimtia hasara sana kwa pombe za bei gari!
   
Loading...