Tahadhari Kwa Wanaoomba Kazi

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Miaka miwili iliyopita kuna kampuni Fulani ilianzisha tovuti yake maalumu kwa ajili ya kutafutia vijana ajira na mambo mengine ya kazi , watu wengi walijiandikisha katika tovuti yao , wengi walituma na kuhifadhi vyeti vyao katika database ya tovuti hii , lakini ghafla baada ya muda tovuti hiyo ikafungwa bila sababu zozote zile na mwenye tovuti hiyo bado yuko mitaani anadunda .

Amechukuwa vyeti vya watu na mambo mengine binafsi ya watu kisha akaamua kufunga tovuti yake baada ya mwaka mmoja sina uhakika kwanini alifunga tovuti hiyo kwa sababu wale waliojiandikisha wakati huo hawakupewa taarifa zozote kuhusu kufungwa tovuti ile .

Je ilipofungwa taarifa na vyeti au mambo mengine ya wanachama waliyohifadhi katika data base hizo zitakuwa na usalama wowote zitakuwa mikononi mwa nani je zikitumiwa vibaya na wahalifu itakuwaje mambo yote hayo ?

Sasa kipindi cha wiki 2 zilizopita nimeona katika mitandao kadhaa watu wanalalamika wameona vyeti vyao ambavyo waliweka katika tovuti nyingine kwa wakati huo ziko kwingine bila wao kuwa na taarifa zozote kuhusu kuwepo kwa vyati vyao hapo

Pamoja na hayo kuna tatizo moja hawa wanaolalamika hawasemi haswa walipojisajili na kuacha cv zao na vyeti vyao wanabaki kulalamika kwahiyo ni ngumu kumnyooshea mtu kidogo kwamba wewe tovuti yako ina husika na hichi na kile .

Inabidi sasa wanaohusika na uangalizi wa tovuti au masuala ya biashara hizi kwa Tanzania wawe na sera au sheria Fulani kuhusu tovuti haswa kama hizi ambazo zinachukuwa mali na taarifa zingine za watu , huwezi kujua wengine wanaweza kuziuza kwa majangili wakaenda kutengeneza vyeti kama hivyo hivyo na kuviuza kwa watu wengine .

Hata wakati mwingine nimewahi kusoma magazeti fulani yakiwa na nafasi za kazi Fulani tena nyingi baada ya mwezi au miezi nafasi zile zile za ajira zinatangazwa tena na watu hao hao kwa anuani zile zile sasa najiuliza ina maana wakati ule hawajapata watu wa kuweza kufanya shuguli hizo mpaka wanarudia tena baada ya miezi 2 ? au ndio yale yale tunayoyaongelea kila siku ?

Binafsi nimepata hofu sana niliposikia hivi na kusoma habari hizi , nikajiuliza kwa nini nchi yetu haina sera au sheria zozote za mitandao zinazoweza kuwabana watu hawa na wengine wanaotoa nafasi za kazi za uwongo katika magazeti na vyombo vingine kisha wanachukuwa tu vyeti vya watu na kwenda kuvitumia kwa shuguli zambazo zinaendana kinyume na maadili ?
 
Shy,
wewe unawafahamu watz, ni wajanja kupita kiasi wao hawaoni hatari kufanya hivyo, pale wanapoona wenzao ni wahitaji basi nao hufanya wanavyojua, lakini hayo ni mawazo mfu,the only way wakati unascan cheti chako ni vema ukascan photocopy instead ya cheti halisia,
 
wengine wanakuambia tuma original katika application yako plus picha yako ya siku za karibuni inakuwaje hiyo
 
Sasa hapo ndipo huwa hapatoshi, kweli ni lazima utaingia mkenge, na kwa kuwa kazi unaitaka, heeeee!!!! basi utachachawa na mwishowe utajikuta umenasa, lakini vipi kama ukiwapa namba ya cell yako na ukawahimiza kama wataitaji orginal wakutafute?
 
Back
Top Bottom