TAHADHARI kwa wana ChitChat wote

Status
Not open for further replies.

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,873
Kila jukwaa lina watu ambao wanakuwa ni members ‘zaidi ya wengine' tokana na mapenzi ya kila member. Katika majukwaa yote hili la CC limekithiri tabia za uchochezi na undumilakuwili kwa members husika. Member anakuwa na ID zaidi ya moja kwa malengo ya kuchezea akili za members wenzie wa hili Jukwaa.

TAHADHARI:

Kwa member yeyote mwenye ID zaidi ya moja na zote akataka kuzitumia ChitChat kwa kutaka kuwa nazo active kwa sababu zozote zile, hizo IDs zitaunganishwa mara moja!

Kwa mwanachama yeyote yule atakayehisi kuna member ana ID zaidi ya moja kwa lengo la kuwavuruga, TAFADHALI taarifa itolewe mara moja kwa njia ya kubofya kitufe cha "Report Abuse" ama kwa PM kwenda kwa Invisible ama Moderator ama wote. Epuka kuvunja sheria kwa kufanya name calling kwenye thread husika, utafungiwa pasipo sababu!

ChitChat imekuwa ikitumika kama njia ya kutafuta wachumba, kuunganisha marafiki, na kukuza ujamaa kati ya baadhi ya members. Na hapohapo imekuwa ikitumika vibaya na baadhi ya waharibifu; kubeza, kejeli, sanifu na kuchezea akili za watu. Hili hatutalivumilia, lengo letu kuwaanzishia uwanja huu halikuwa kuwavuruga!

Zoezi la kufuta huo usanii wa kuwa na ID zaidi ya moja kwa ajili ya kujikosha na nyingine kwa ajili ya kuponda na kusababisha ukosefu wa amani limeshaanza kufanywa mara moja na baadhi ya IDs zimekuwa merged.

Wana ChitChat, hili jukwaa linaweza kuonekana ni sehemu ya mzaha na lisilo na tija! Hii sio sahihi. Kila mahala katika jamii panahitaji sehemu ambayo ni ‘Stress free zone' kama ilivyokuwa awali na kama itakavyokuwa kuanzia sasa ambapo lipo na uangalizi wa karibu. Tutajiepusha na ban lakini itapobidi, tutatembeza ban kwakuwa tutakuwa tumelazimika!

Ni muhimu, mtambue kuwa tunaheshimu privacy zenu na iwapo mkapata threats au PM za kutilia mashaka wasisite ku-report kwetu nasi tutachukua hatua haraka sana. EPUKA ku-paste PM ya mtu katika public forums, itakuzawadia ban kwakuwa ni nje ya sheria za JF!

NOTE: Hakuna moderator hata mmoja anayeweza kujigamba, kupiga mkwara kupitia PM wala kukupigia simu kukutishia kwa namna yoyote ile, mods wetu wamefunzwa uvumilivu na kuheshimu privacy za watu na hivyo yeyote atayekuja kwako akijigamba kuwa moderator wa JF tafadhali tufahamishe mara moja!

Nawatakia Chit Chatting njema…
 
Invisible naomba kuuliza, maana ya "name calling" ni ipi haswa? unamaanisha mentioning(like what i just did to your name) au quoting au kuandika jina la ID ya mtu kwenye post???

Hapana, soma sheria za JF:

JamiiForums Rules

Kuna vipengele hivi:

1 - Flaming, Bashing, and Trolling:
Hate posts and personal attacks will not be tolerated on the boards. Treat others on these message boards as you would expect them to treat you. Posting topics specifically designed to provoke a negative response from someone (aka trolling) is also asked to be avoided.

2 - Profanity:
Profanity is not tolerated in the board, some words will be censored, also there is to be no name calling, linking two/more display names or a display name with a real name, doing so will give you a warning, and then a ban if you continue.
Mbili hizi zimekuwa zikivunjwa makusudi, si jambo la kufurahisha
 
Tumekusoma mkuu, tena kuna wimbi la watu wameibuka kwa lengo la kuhakikisha wanaharibu hali ya hewa humu na baadae kujisifia kuwa wao ni kiboko ya wana chit chat, mfano ni ndugu C.T.U na kuna mwingine nimemuona leo anajiita @antchitchat, nimekuwa na wasiwasi nae pia, tunashukuru kwa mwongozo wako mkuu na kutukumbusha maana uwepo wa hili jukwaa kwa wale tuliokuwa tunalifikiria ndivyo sivyo.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante kwa maelezo mazuri mkuu Invisible, lakini mimi bado nina oni moja. Ili kupunguza haka kautaratibu ka kuwa na ID mbili, swala la ban lazima litazamwe upya. wakati mwingine ban zinasababisha ID nyinginyingi humu.Halafu wengine wanakula ban za kionevu kwa nini asifungue ID nyingine?Ujue kukaa 2 good weeks bila kutimba humu ni shughuli pevu.

Ban iwe adhabu ya mwisho baada ya maonyo mengine kupita.

Naomba kuwasilisha.
 
Hili la id zaidi ya moja labda litolewe ufafanuzi
je ni haramu chit chat tu?
au hata kwingine mfani mmu?
na ni wakati gani id zaidi ya moja ni sawa?

Mkuu The Boss, zingatia maelezo haya chini. Jibu lako lipo hapo.

Kila jukwaa lina watu ambao wanakuwa ni members ‘zaidi ya wengine' tokana na mapenzi ya kila member. Katika majukwaa yote hili la CC limekithiri tabia za uchochezi na undumilakuwili kwa members husika. Member anakuwa na ID zaidi ya moja kwa malengo ya kuchezea akili za members wenzie wa hili Jukwaa.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
112 Reactions
Reply
Back
Top Bottom