Tahadhari kwa wamiliki wa magari: Ukiwa kwenye taa au foleni funga vioo, inasemekana kuna Vibaka wenye visu vikali wanapora pesa kimya kimya

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,249
21,345
Nimesikia kuna Clip inazunguka kwenye mitandao kwamba; Kuna aina mpya ya uporaji Kwa madreva wenye magari madogo wakiwa kwenye foleni au taa!
Mashuhuda wanasimulia kwamba Mwizi anapokuona umeshusha vioo, ukiwa peke ako kwenye foleni au taa (makutano junction)!

Anakuvizia Kama wapitavyo Machinga anajibana kama vile mshikaji huku mikono yake ikiwa ndani tayali anaanza kukutomasa Kwa kisu kikali sana huku akikuomba utoe Pesa zote umpe!

Inadaiwa style ya vibaka hao wanayotumia haiwezi kushitukiwa kirahisi na watu wanaokuzunguka kwasababu anakuja kama mshikaji, na akimaliza kukupora anakwambia "Siku ingine kwenye foleni au taa usiache kioo wazi"

Halafu anapokuaga anakuambia "NITAKUPIGIA TUONGEE VIZURI"
Ili kuwahadaa wanaokuzunguka waone kama no mtu na mshikaji wake!

Wanaume Kwa wanawake wengi wanasimulia kuporwa Kwa style hiyo mpya!
Mmoja anasadikiwa kuwepo maeneo ya taa za mnazi mmoja na pale BigBon

Hawajabahatika kupata PICHA yake lakini inadaiwa ni lijitu jeusi lenye sura ya kikauzu!

WITO;
  1. Polisi hususani Trafiki wanaongoza magari wasiruhusu wafanya biashara (machinga & ombaomba) kutembea kwenye foleni au taa
  2. Madreva wachukue tahadhari wapandishe vioo hasa wakiona wapo wenyewe.
  3. Ile sheria ya faini ya laki mbili Kwa mtu anaempa pesa ombaomba kwenye foleni iongezewe nguvu
NOTE; Sisi wenye ESCUDO Tutafte namna nyingine ya kujihami maana AC zetu ni za MAZABE!

NAMNA YA KUMKATA MTU HUYO

Wanaume Wa Dar; kama mkeo anafaham kuendesha mkabidhi aendeshe, halafu wewe jilaze siti ya nyuma kwenye foleni au taa mwambie mkeo ashushe vioo vya mbele tena kama ikiwezekana mwambie azuge kujipodoa na lips stick ili mwizi asogee, halafu ukisikia mazungumzo toka na panga Kwa mlango Wa nyuma usiulize na umuarest haraka iwekezekanavyo!

Mimi binafsi nimeaza operesheni hii tangu Jana sisubiri hadi Polisi waseme! Nitawapa mrejesho!
 
Akiniwekea bastola atafanikiwa kunipora lakini siyo kisu. Niko ndani ya gari halafu yeye yuko nje aingize mikono yenye kisu ndani nimpe nilichonacho? Nyasi zitawaka moto!
Hizo nyasi kwenye lami wakati huo utaziona wapi kakutaiti ikumbukwe kisu ni kidogo halafu kikali akigusa kidogo tu huna koromeo!
Au unazani kisu anakibeba begani kama shoka?
 
Hii inaonekana kama mzaha na kuwatania wanaume wa Dar ila kumbukeni kibaka au mwizi had nothing to loose akigundua hutacooperate anaweza akakisokomeza kisu ndani ya shingo, puani, jichoni ama mdomoni kabla hajakimbia. Unaweza usife ila ukabaki na majeraha makubwa!! Hapa cha muhimu ni kufunga vioo vya gari na kuchukua precautions zote! Silaha ni silaha, bunduki, panga, shoka, bisibisi, kisu na hata jiwe zinaweza kutumika na kuleta madhara ya kifo au majeraha makubwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea Kwa busara sana! Tushikamane kuwatafta waporaji hawa!
 
Huyo mwizi nae ana dalili ya uzembe😂😂mi uwezi niibia alafu uniage.
Nitakavyo deal naye, atajuta.
 
Wewe Mimi hapana akileta uduwanzi ndo nashuka kabisa.. kifuatacho taratibu za mwaliko wa msiba.

Hii inaonekana kama mzaha na kuwatania wanaume wa Dar ila kumbukeni kibaka au mwizi had nothing to loose akigundua hutacooperate anaweza akakisokomeza kisu ndani ya shingo, puani, jichoni ama mdomoni kabla hajakimbia. Unaweza usife ila ukabaki na majeraha makubwa!! Hapa cha muhimu ni kufunga vioo vya gari na kuchukua precautions zote! Silaha ni silaha, bunduki, panga, shoka, bisibisi, kisu na hata jiwe zinaweza kutumika na kuleta madhara ya kifo au majeraha makubwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom