Tahadhari kwa wale ambao watoto wenu wanasoma shule ambazo wanapelekwa na School Bus | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari kwa wale ambao watoto wenu wanasoma shule ambazo wanapelekwa na School Bus

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by everybody, Mar 29, 2012.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu, jana nimepata habari ya kusikitisha sana. Kama tunavyojua wakazi wengi wa Dar es Salaam and i think mikoa mingine pia tunapeleka watoto wetu shule ambazo zina school bus kwa ajili ya kurahisisha usafiri. Sasa jana kuna mzazi ambaye mtoto wake alichukuliwa na school basi kama kawaida ila wakiwa njiani kilichotokea ni kwamba mtoto yule akiwa ndani ya basi alikanya sahemu ambayo nafikiri bati la basi lilikua limeoza na kilichotokea ni yule mtoto kudumbukia ndani na kwa vile dereva hakulitambua hilo kwa haraka, aliendelea kuendesha gari na yule mtoto alikanyagwa. It is so SAD.

  Ushauri wangu ni kuwa sisi kama wazazi tuchukue hatua ya kukagua magari haya yanayowapeleka shule na kuwarudisha nyumbani watoto wetu kuona kama yana ubora unaotakiwa. Kwa kweli inauma sana mtoto wako ameondoka nyumbani salama ila kwa sababu ya tamaa za wenye hizo school basi hawatumii hela kufanyia marekebisho magari yao, mwanao anarudi nyumbani kama taarifa ya kifo.

  Lets be proactive on this.

  Nawasilisha.
   
 2. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Its so sad,I see!!!
  This is Africa,hakuna gari mbovu,unakuta gari imebaki mabati tu lakini bado ipo barabarani na hesabu zinapelekwa!!
  Chumvi ikishaharibika utaitia nini ili ifae tena?!!!
   
 3. c

  collezione JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Duh,... Nimesikitika sana

  Any way kaka, sio ma_school basi tu. Hata mabasi yetu ya kusafiria yote yameoza...

  Ndo maana nasema na nitarudia kusema. hizi ajali za barabarani, nyingi ni za kujitakia...

  Ila kwa kuwa waTanzania ni wamcha Mungu sana... Utawasikia watu eti "mapenzi ya Mungu"
  Mimi naomba tusiwe tunamuingiza Mungu kwenye huu ushetani wa uzembe.. Tuwe tunasema kwa mapenzi shetani..(Kwasababu hakuna Mungu anayependa watu kufa kizembe hivyo)
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ukweli mabasi mengi yanayobeba watoto wa shule ni mabovu mno. Mabasi mengine utafikiri yametolewa kwenye mabanda ya makumbusho (museum).
   
 5. M

  Mitowo Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jesus christ, mungu wangu so sad, jaman nimesiktka sana, kwel kuna haja ya kufanya ukaguz wa haya magari na ukilikuta bovu unatoa taarifa polisi, ni wapi imetokea hyo issue na shule gani?
   
 6. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 60
  Inasikitisha sana, wazazi inabidi tuwe makini sana na kila jambo tunalowafanyia watoto wetu na uangalizi wa kutosha unahitajika kwa watoto wakati wote jamani. Nawapa pole sana ndugu wa huyo mtoto, namuomba Mungu mwenye uwezo mweza wa yote awatulize na kuwapa faraja kwenye kipindi hiki kigumu, katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti anayeishi na kutawala milele Amin.
   
 7. m

  mgadafi Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapana na trafic wanachangia izi ajali nimewahi kuna hiace school bus imebeba watoto zaid ya 35 yani kwa sababu ni watoto ndio hawana haki ya kurilax?then unakuta shchool bus nyingi hazina kondactor watoto haohao ndio wanajifungulia milango.mwisg.o wa yote madreva wa school basi ni waroho wana tabia ya kuyapekuwa mabegi ya watoto na kuwalia icho kdg wanachokwenda nacho shule.211]Inasikitisha sana, wazazi inabidi tuwe makini sana na kila jambo tunalowafanyia watoto wetu na uangalizi wa kutosha unahitajika kwa watoto wakati wote jamani. Nawapa pole sana ndugu wa huyo mtoto, namuomba Mungu mwenye uwezo mweza wa yote awatulize na kuwapa faraja kwenye kipindi hiki kigumu, katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti anayeishi na kutawala milele Amin.[/QUOTE]
   
 8. +255

  +255 JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,910
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Walikuwa wanacheza na mwenzake akadondoka kupitia dirishani na sio kama ilivyotangazwa manake wamelikagua gari na hawakukuta sehemu iliyotoboka kwa ndani...Habari toka polisi
   
 9. m

  mzawahalisi JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  kutokuwajibika, Rushwa, kuchukulia poa, na ushikaji ndio unatugharimu watanzania.

  Pole mtoto kizazi chetu cha hobelehobela kimekutoa duniani.
   
 10. n

  ng'wandu JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kuna tatizo kubwa la usimamizi katika mabasi yanayobeba wanafunzi. Dereva na konda wanabehave kama vile wamebeba abiria wa kawaida bila kujali kuwa wale ni watoto wadogo. Iweje konda yuko hapo ndani, watoto wacheze mpaka wadondoke?

  Nilishashududia kwa macho yangu mtoto wa kama miaka miwili hivi akidondoka kutoka ndani ya school bus hapo kinondoni manyanya, konda akashuka na kumuokota, sikujua kama yule mtoto aliumia au la. Kwa rehema za Mungu kuliko hakuna gari jingine karibu ambalo lingeliweza kumkanya mtoto yule.

  Kuna dereva wa school bus moja alikuwa anakuja kumchukua mtoto wangu nyumbani, alikuwa rough sana hata majirani walianza kunung'unika, believe me ilikuwa sababu mojawapo iliyonifanya nimhamishe mtoto wangu, hasa baada ya gari hili kupata likiwa limebeba wanafunzi.

  Nafikiri sis wazazi ambao tunalipa hela nyingi kwa ajili ya usafiri wa watoto wetu sasa tuamke na kuchukua hatua. Tuangalie ubora wa magari na hao wafanyakazi ndani ya magari hayo
   
 11. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Aisee.....inasikitisha sana iwe ni kwa kutumbukia chini au kuruka dirishani kama ambavyo taarifa zilivyo hapo juu, huu ni uzembe wa hali ya juu watoto hawakuwa na mwangalizi ndani ya gari, kazi ilikuwa ni nini na kwa nini asiangalie kama gari lake halina mazingira hatarishi kwa watoto ambao wanahitaji ungalizi wa hali juu. kama ni kutoboka je dereva huyo hafanyi ukaguzi wa gari na kugundua ubovu unaoweza kuleta madhara kwa abiria, chombo chenyewe, na yeye mwenyewe kabla hajaanza kazi yake? oohh... maswali yanazidi kunijia bial majibu.
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  yeuwiiiiii jamani nimeumia moyo sana, sijui mzazi wa huyo mtoto ameumiaje nafsi yake! MUNGU AMPE UVUMILIVU na km wazazi hatutaamka watoto wetu watamalizwa,
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  inamana hakuna usimamizi wowote hadi mtoto acheze hadi atoke dirishani akanyagwe afe wakati gari linatembea !!
   
 14. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,697
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  Kama kawaida yetu ya kureact on issues. Utaona wiki hii magari mabovu yatakamatwa na kukaguliwa ila ikiisha wiki mbili tunasahau tunarudia tulikotoka. Wapi ukaguzi wa siti belt..tumeshasahau.
   
 15. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,697
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  Hii issue inakuwa tatizo hasa pale wamiliki na wadau wakubwa wa vyombo vya usafiri wanatoka huko huko Sumtra na Vyombo vya Usalama ie Polisi.. Huwezi kujikamata na kujikagua mwenyewe..
   
 16. m

  mariavictima Senior Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo hivyo tu, madereva na makondakta wengi wanawanyanyasa watoto kijinsia hasa wale wanaobaki nao wa mwisho kwenye gari. Kuna mzazi alishuhudia mtoto wake akiwa na mbegu za kiume kwenye nguo zake. Alipoulizwa na mzazi akasema eti kondakta alimpakata. Wazazi pigeni kauli mbiu ya kuwa na madada kwenye school bus. Shule zote ziige mfano wa St. Aloysius girls Primary iliyoko Mbezi Beach - Makonde.
   
 17. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,697
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  Last week nilipita mitaa ya Arusha nikakuta daladala kioo cha nyumba kimevunjika chote kiasi cha gari kuwa wazi nyuma, lakini bado linapakia abiria na lina pita barabarani mbele ya trafic. Nilisahau kuangalia jina la mmiliki coz katika hali ya kawaida haiwezekani
   
 18. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #18
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha sana,pia wenye mashule wawe makini kwani hawa madereva wanowapa
  kuendesha hizi school bus wengi walikuwa wa daladala,utakuta dereva na kijana wake
  wote wako mbele kwenye basi watoto wako nyuma peke yao,hivyo ni rahisi kuumizana,
  maana hawana mtu wa kuwaangalia.
   
 19. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  nina wasiwasi na hapo kwenye red, watu wanaomcha Mungu wanathamini maisha lakini kiukweli Watanzania hatuthamni maisha. Chunguza hili na utagundua! Na sio ajabu kukuta kuwa mifumo karibia yote ya maisha ni hatarishi kwa binadamu lakini tumekaa na hakuna tunachofanya!
  Kiukweli hii ni ajali ya kusikitisha sana na inakuwa ngumu hata kueleza mkasa huu. Poleni sana

   
 20. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Duh inauma sana hii kiukweli hali ni mbaya sana,binafsi navyoona magari kwa mfano gari la kariakoo-kimara likichoka wanabadilisha route linakwenda labda kimara-bonyokwa(kimara juu) likichakaa hawana pa kulipeleka ss ndo hapo inakuja idea ya kulipeleka kuwa school bus hebu niambieni litakuwa kwenye hali ipi??me nimeshaona mengi tu ma school bus ya mtindo huu na wazazi tunalipa hela nyingi!Polisi ss wana wajibu wa kukagua ubora wa mabasi wa watoto wa shule yote vyinginevyo tutakuja kujutia baadae!wazazi pia tuliangalie hili!
   
Loading...