Tahadhari kwa Wagombea Ubunge wa Chadema na ACT, Bara na Visiwani

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
842
2,467
Kuna jambo moja wengi wenu hamjaliweka akili au pengine kuliwazia.

Kwamba kama vyama vyenu vitalisimamia kwa nguvu zote suala la Tumehuru ya uchaguzi basi uchaguzi huu wa 2020 mnaenda kuunda serikali kwa Chadema huku bara na ACT kule Zanzibar.

Kwamba hatuwachagui kwa wingi ili muende ubungeni kufanya ujinga kama uliokuwa unafanywa na CCM kushangilia kila kiletwacho na serikali yao na kuunga mkono hata upuuzi.

Tutahakikisha sheria inabadilishwa ili wabunge wasiwe mawaziri kama ilivyo Kenya hivyo hakuna kujipendekeza ili kuteuliwa kuwa waziri. Hata ile katiba ya Warioba iliyo sema mbunge anaweza kuondolewa na wananchi wake kama yupoyupo tuu kama walivyo wabunge wengi wa sasa wa CCM.

Je kabla ya kuchukua fomu mmejiuliza hayo mtayaweza? Ujinga wa kuunga mkono kila jambo la serikali ya Chadema na ACT hamta kubaliana nao? Maana kama huwezi bora usichukue fomu kabisa, hatutaki akili za kiccm kabisa 2020-2025 maana ndio zimetufikisha hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bunge hili la sasa ni UTOPOLO kabisa japo ni Bunge la Vyama vingi...CCM mle Bungeni ni zero brain kabisa, bado najiuliza Bunge la 1990-1995 lililokuwa la Chama kimoja (CCM) mbona lilikuwa na wabunge mahiri?

Nakumbuka G-55 ya akina Njelu Kisaka na wengineo ilivyopeleka hoja Bungeni juu ya Serikali 3 ndani ya Muungano, enzi hizo PM ni Mzee John Samwel Malecela (Cigwiyemisi), ambaye alicheza fair play na Bunge likawaka moto.

Bila Baba wa Taifa, Mwl JK Nyerere "Mchonga" Leo hii Muungano ungekuwa wa Serikali 3...

CCM ya Leo wabunge wake wengi ni UTOPOLO chini ya Spika JYN....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tushirikiane Ku make sure Tumehuru inakuwepo ili yale tusiyo amini kutokea yatokee
Mkuu Mkongwe Mzoefu, kuna baadhi ya mabadiliko huwezi kuyafanya ukiwa nje ya mfumo rasmi. Hivyo mimi mwana jf mwenzenu nimeamua kuunga mkono juhudi, na kuleta mabadiliko from within.
Hivyo naomba support yenu kwenye hili ili nikifika humo ndio tuibadili Tume ya Uchaguzi sio iwe huru, Tume ni huru bali iwe Shirikishi.
Nimeamua Kustaafu Rasmi JF, Utangazaji na Uandishi wa Habari Baada ya Kuhudumu Miaka 30. Niko Free Kujiunga Siasa, Nimejiunga CCM na Nitagombea Ubunge - JamiiForums

P
 
Kama huamini hili itakuwa ngumu kuamini hata jina lako

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni vyema kuchagua chama kingine nje ya ccm kuongoza nchi, lakini ni ngumu kusema eti cdm wakichukua nchi hawataunga mkono kila kitu cha serikali kama ccm. Kama cdm karibia wote waliunga mkono ujio wa Lowassa waliyesema ni mchafu kwa zaidi ya miaka 7, leo utaamini vipi kuwa wanaweza kutokuunga mkono kila kitu cha serikali yao kama ccm?
 
Mkuu Mkongwe Mzoefu, kuna baadhi ya mabadiliko huwezi kuyafanya ukiwa nje ya mfumo rasmi. Hivyo mimi mwana jf mwenzenu nimeamua kuunga mkono juhudi, na kuleta mabadiliko from within.
Hivyo naomba support yenu kwenye hili ili nikifika humo ndio tuibadili Tume ya Uchaguzi sio iwe huru, Tume ni huru bali iwe Shirikishi.
Nimeamua Kustaafu Rasmi JF, Utangazaji na Uandishi wa Habari Baada ya Kuhudumu Miaka 30. Niko Free Kujiunga Siasa, Nimejiunga CCM na Nitagombea Ubunge - JamiiForums

P

Utafanya nini Paskali, mtu mwenye uwezo wa kufanya mabadiliko ya mfumo anaonekana tu, lakini sio ww Paskali. Ni nani alikuambia ukiwa ndani ya mfumo ndio unaweza kuleta mabadiliko? Kama unatafuta ulaji tafuta kwa gia nyingine, sio hiyo ya kuwa mbunge eti ulete mabadiliko. Mama Tibaijuka amezeekea bungeni na alikuwa waziri kabisa, jana analia kama mtoto aliyenyimwa nguo mpya ya siku kuu, eti sheria ya kusikilizwa haikufanyiwa kazi, hivyo kawaachia wengine waifanyie! Sifa yako kubwa Paskali ww ni mrefu, lakini sio ya mtu mwenye msimamo. Hivyo huna lolote unaloweza kwenda kubadilisha ukiwa bungeni, zaidi ya kuwakarimu wabunge wakike weupe.
 
Kuna jambo moja wengi wenu hamjaliweka akili au pengine kuliwazia.

Kwamba kama vyama vyenu vitalisimamia kwa nguvu zote suala la Tumehuru ya uchaguzi basi uchaguzi huu wa 2020 mnaenda kuunda serikali kwa Chadema huku bara na ACT kule Zanzibar.

Kwamba hatuwachagui kwa wingi ili muende ubungeni kufanya ujinga kama uliokuwa unafanywa na CCM kushangilia kila kiletwacho na serikali yao na kuunga mkono hata upuuzi.

Tutahakikisha sheria inabadilishwa ili wabunge wasiwe mawaziri kama ilivyo Kenya hivyo hakuna kujipendekeza ili kuteuliwa kuwa waziri. Hata ile katiba ya Warioba iliyo sema mbunge anaweza kuondolewa na wananchi wake kama yupoyupo tuu kama walivyo wabunge wengi wa sasa wa CCM.

Je kabla ya kuchukua fomu mmejiuliza hayo mtayaweza? Ujinga wa kuunga mkono kila jambo la serikali ya Chadema na ACT hamta kubaliana nao? Maana kama huwezi bora usichukue fomu kabisa, hatutaki akili za kiccm kabisa 2020-2025 maana ndio zimetufikisha hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
Wosia mzuri huo,so kwa wabunge wa CDM & ACT Wazalendo pekee.Siyo kazi ya mbunge kuitetea serikali Bali kuisimamia.Hawa wote waliopoteza mwelekeo tuwapige chini bila kupoteza muda.
 
Bunge hili la sasa ni UTOPOLO kabisa japo ni Bunge la Vyama vingi...CCM mle Bungeni ni zero brain kabisa, bado najiuliza Bunge la 1990-1995 lililokuwa la Chama kimoja (CCM) mbona lilikuwa na wabunge mahiri?

Nakumbuka G-55 ya akina Njelu Kisaka na wengineo ilivyopeleka hoja Bungeni juu ya Serikali 3 ndani ya Muungano, enzi hizo PM ni Mzee John Samwel Malecela (Cigwiyemisi), ambaye alicheza fair play na Bunge likawaka moto.

Bila Baba wa Taifa, Mwl JK Nyerere "Mchonga" Leo hii Muungano ungekuwa wa Serikali 3...

CCM ya Leo wabunge wake wengi ni UTOPOLO chini ya Spika JYN....

Sent using Jamii Forums mobile app

Kweli bunge letu asa hivi ni UTOPOLO, tunalibatiza jina Bunge-utopolo
 
Ni vyema kuchagua chama kingine nje ya ccm kuongoza nchi, lakini ni ngumu kusema eti cdm wakichukua nchi hawataunga mkono kila kitu cha serikali kama ccm. Kama cdm karibia wote waliunga mkono ujio wa Lowassa waliyesema ni mchafu kwa zaidi ya miaka 7, leo utaamini vipi kuwa wanaweza kutokuunga mkono kila kitu cha serikali yao kama ccm?
Bado tuu hujaamini kuwa ujio na uondokaji wa Lowassa umeleta somo zito kwa Chadema?
Uchaguzi za chama Decemba mwaka Jana zimeonyesha wazi kuwa somo la yaliyotokea limewaingia na kujitambua.
Hata hivyo hoja hapa ni kutoa tahadhari kwa watakao gombea kujitambua wajibu wao na kuwa tofauti na CCM
 
Back
Top Bottom