Tahadhari: Kwa waendesha Boda boda na watumiaji mkoani Kilimanjaro

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,204
15,198
Salaam Wakuu,
Tujitwike kwenye mada.

Kama wote tunavyojua kuwa hiki ni kipindi cha mvua katika maeneo mengi ya nchi yetu na maeneo mengine duniani. Mvua ni nyingi na Mungu ashukuriwe kwa baraka zake.


Sehemu kubwa ya mkoa wa Kilimanjaro haswa Marangu,Uru,West Kilimanjaro na maeneo mengineo udongo wake una asili ya utifutifu hivyo huwepo na utelezi kipindi cha mvua.

Usafiri kwa kutumia pikipiki (boda boda) imezoeleka Sana miongoni mwa Watanzania wengi hivyo hutumika Mara nyingi Sana.
Katika kipindi hiki cha mvua,tope huwa jingi Sana na ardhi huteleza.
Usafiri wa bodaboda huwa si rafiki Sana katika kipindi hichi.

Miinuko huteleza kupita kiasi. Waadhirika wakubwa ni watumiaji wa bodaboda.

Hivyo,nawashauri watumiaji wa usafiri huu mpunguze na angalau tafuteni njia mbadala ikiwepo hata kutembea kwa miguu(kama uendako si mbali) na usafiri wa daladala.

Utafika salama kuliko kujitoa ufahamu. Kukiwa hakuna jinsi,tafuta pikipiki ambayo magurudumu (tyre) yake hayajaisha au hayaelekei kuisha na breki ziwe za uhakika.
Umsisitize dereva aendeshe kwa mwendo wa kawaida kabisa na zile speed zao zipungue kabisa kipindi hiki cha mvua.

Chukua tahadhari na kila la kheri.

NB: Ni kwa watumiaji wa barabara ambazo siyo katika kiwango cha lami.
 
Asante, pia waambie wakati huu wa mvua viroba si rafiki wa kuendesha bodaboda kutoka mijohoroni hadi kule juu SANGO
 
Kwa maoni yangu mimi huu ushauri ulipaswa kuwa wa nchi nzima, sasa sijui kwa nini umechagua Kilimanjaro peke yake
 
Asante, pia waambie wakati huu wa mvua viroba si rafiki wa kuendesha bodaboda kutoka mijohoroni hadi kule juu SANGO
Haswaaa Mkuu. Viroba siyo vya kuvigusa wakati huh,japo wanadai huleta joto katika kipindi cha baridi.
 
Kwa maoni yangu mimi huu ushauri ulipaswa kuwa wa nchi nzima, sasa sijui kwa nini umechagua Kilimanjaro peke yake
Mkuu,ni kweli ungepaswa kuwa wa Tanzania nzima ila mm nimeuchagua mkoa wa Kilimanjaro kwa sababu ndo nina uzoefu nao.
 
Back
Top Bottom