Tahadhari kwa Vyombo vya Dola: Wiki ijayo ina matukio makubwa mawili Ujio wa Lissu na Msiba

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Ni dhahiri Vyombo vingi duniani kuanzia leo hadi wiki ijayo vitaelekeza antenna zao Tanzania, kwa vile kuna matukio makubwa mawili, moja ni la ujio wa Tundu Lissu unaosubiriwa kwa hamu na wa Tanzania wengi na jingine ni tukio la msiba mkubwa wa aliyekuwa Rais wa Tanzania.

Chonde chonde, Serikali na Vyombo vya Dola hatutaki mtuongezee majonzi mengine, hasa kuhusiana na mapokezi ya kiongozi mkuu wa Chadema na mtia nia wa ugombea urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Lolote litakalotokea baya litauthibitishia umma kuwa yote yaliyokuwa yanasemwa kuhusu Lissu ni ya kweli.

Msiba huwa hauji kwa bahati mbaya, ni mpango wa Mungu ili kufikisha ujumbe anaotaka.
 
Back
Top Bottom