Tahadhari kwa viongozi wa chadema na wanachama wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari kwa viongozi wa chadema na wanachama wote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OPORO, May 7, 2012.

 1. O

  OPORO Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa CHADEMA,WANACHAMA NA WEPENZI wapenda mabadiliko,tupo katika nafasi nzuri sana ya kudai Tanzania Tunayotaka,tunaungwa mkono na watu wengi na tumekuwa tukipata msaada wa kila aina kutoka kwa jamii pana ya watanzania walio ndani na nje ya nchi,wote hawa wanafanya hayo kwa mapenzi mema waliyonayo kwa nchi yao,kuumia kwao kutoka na maisha tunayoishi katika taifa letu na uhitaji wao wa kubadilisha mfumo wa utawala uliopo ambao umeshindwa kumkomboa mtanzania na kumtoa katika lindi la umasikini.


  Pamoja na mazuri yote haya kwa jamii ya watanzania kwa CHADEMA,Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA wanaonekana kulewa sifa,ushabiki na baadhi yao kujikweza kabla ya kupata dola,umefika wakati ambapo baadhi ya wanafamilia wa viongozi kujitwalia mamlaka ya CHAMA na kutoa kalipio kwa viongozi halali wa CHADEMA ngazi ya Kata,Wilaya,Mkoa na kwa sasa inaanza kuwakumba baadhi ya viongozi wa Taifa.

  Nasema haya mapema ili viongozi wa CHADEMA,WANACHAMA NA WAPENZI tuchukue atua mapema ili tusije tukapewa dola na wananchi na tukajikuta wananchi wanajuta kuindoa CCM madarakani kutokana na matendo yetu kuzidi kuwakatisha tamaa.Viongozi,Wananchama na Wapenzi wa CHADEMA tuishi na kufanya harakati tujua na kujikumbusha kila siku kuwa kwa sababu ya kuwa mwanacham,shabiki au mkereketwa wa CHADEMA leo kuna watu:


  1. Wako gerezani kwa sababu ya CHADEMA
  2. Hawana ajira kwa sababu ya CHADEMA
  3. Ni Vilema kwa sababu ya CHADEMA
  4. Ndoa zimefarakana kwa sababu ya CHADEMA
  5. Wanabaguliwa makazini kwa sababu ya CHADEMA
  6. Wamefukuzwa kwenye nyumba za kupanga kwa sababu ya CHADEMA
  7. Wamefukuzwa vyuoni kwa sababu ya CHADEMA

  Je,katika mienendo,kauli,vitendo tunayotenda kama taasisi tunajua haya? na kama tunajua,tunayafanyia kazi kwa kiasi gani? Tunatambua idadi ya waandishi,wanaharakati,wanataaluma, wafanyakazi ,wanafunzi walioamua kuweka maisha yao rehani kwa ajili CHADEMA? Je,ni kwa kiasi gani uongozi wa CHADEMA unaelimisha secretariat ya CHAMA makao makuu kujua na kuishi maisha yanayotafsiri au kuhakisi ulisia huu.

  Viongozi wa CHADEMA taifa,Wananchama,Wapenzi na Wakereketwa,Tujiandae kwa ukweli katika kuikomboa nchi ili baadae tusije tukawaangusha watanzania.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Una mawazo mazuri ndugu.lakini jukumu hili silaviongozi pekeyao ni lakwetu pia.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kuwa mpambanaji maana yake ni kwamba uwe tayari kwa lolote.
  Kwa hayo unayoyasema kuwa kuna viongozi wa CHADEMA wamelewa madaraka sijui, unless una ushahidi wa kutosha.
  Chama chochote kama taasisi inaongozwa na watu wenye hulka na tabia tofauti. Sasa I don't think that it's right time kui judge chama kwa udhaifu wa mtu moja tena in personal circumstances.

  Ninachoamini ni kwamba CHADEMA kama chama cha siasa ni chama kinachoongozwa na watu wenye dhamira njema na Tanzania na Watanzania.
  Hiki chama kiko makini kuliko unavyodhani, maana akionekana kupe au mpumbavu yoyote anashughulikiwa pale pale hakuna kusubiri kesho.
  Ni kweli kwamba kuna baadhi ya watu wamepata matatizo kwa ajili ya CHADEMA, ambapo hata mimi ilinigharimu kwa namna moja ama nyingine. Hata hivyo mambo haya lazima yatokee, katika mapambano ya kudai haki na ukweli wapo watu watapoteza maisha, ajira, viungo vyao nk. na mapambano yanaendelea.

  Ninavyoona na nilivyohisi ni kwamba wewe si mpambanaji, na kama ni mpambanaji basi una ngozi nyepesi inayoweza kuchanwa hata na ka upepo.

  Au umetumwa humu kupima upepo wa makamanda.
   
 4. s

  step Senior Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu WAKEREKETWA/WAFURUKUTWA haya ni maneno aka mipasho ya CCM haitumikagi na wana CHADEMA.
   
 5. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama CHADEMA ndo walisababisha hao watu wapatane na hayo yaliyo wakuta
  Labda useme kwakuwa wapo chadema basi watu wengine wanaamua kufanya Hivyo
  Na hao waliofarakanisha Ndoa zao Sidhani kama Chadema imefarakanisha Ndoa ya Mtu
  Bali ni walo wawili walichokana tu wakaamua kutafuta Sababu, na Walio vunjika Miguu ni
  Askali wa selikali yenu ndo walifanya hivyo na si Chadema,

  Mbona unapotosha jamii wewe?
   
 6. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tupo vitani mkuu, hayo yote yanatokea kwa kuwa wenye dola hawataki mabadiliko, ukiwa Mtanganyika kama mimi uwe radhi kwa lolote mpaka tutakapoikomboa nchi yetu mikononi mwa mafisi wanaifisidi. Hatuwezi ku-retreat mpaka tu-win war, tayari tushawin battle kadhaa, hivyo wewe kama upo nasi watie moyo hao ndugu kwamba bado safari inaendelea na mengi yatatiokea ilhasi tunapambana. Chadema sio ya viongozi wa taifa ila ya Watanganyika wote.
   
 7. M

  MTK JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Good food for thought; wenye masikio wasikilize hoja hiyo tusije ikwa kama kumuondoa mkoloni mweupe ukamwingiza mkoloni mweusi; hasara tupu the revolution will be still born. tahadhari kabla ya hatari.
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ningependa uongee kwa kutuwekea ushahidi zaidi si propaganda
   
Loading...