Tahadhari kwa Serikali ya CCM, Mungu hajalala

Nawatahadharisha tu, mateso wanayoyapitia watu wa Mungu, kuonewa, kupigwa, kudhulumiwa...mnadhani Mungu amelala na hayaoni mateso wanayopata watu wake?

Tuoneeni tu!! Ila mjue Mungu mtenda haki hajalala.
Bavicha wamesema wakati wa kuonewa umeisha, sasa wewe unasema tuoneeni tu!
 
Ccm wanadhani kwasababu watz wengi ni wanyonge basi wanaweza kuwafanya lolote.

Wanasahau kuwa Mwenye kulipa kisasi ni Mungu Mwenyezi pekee!

Mioyo ya wanyonge itaendelea kusikitika na kunung'unika kimya kimya, ila Mungu wa Yakobo atalitukuza Jina lake.
 
Mungu mpenda haki huitazama mioyo na sio maneno yatokayo vinywani........

Vinywani mwa wanasiasa kumejaa maneno ya busara na na unyenyekevu Lakini mioyo yao imejaa usheitwani na ufedhuli wa hali ya juu.....

Ndio hao hao wanaokula viapo bungeni huku wameshika vitabu vya Mungu na upande wa pili wanatenda matendo yanayowaangamiza wengine......
Na wanafikiri huyu Mungu Amelala
 
"Mnyapara wa barabara" yuko kazini, hasikii la yeyote isipokuwa DAB. Eti asema anawapigania 'wanyonge' hata kwa kubomoa Nyumba za hao 'wanyonge'!

Mbaya zaidi mnyapara anafanya udhalimu huku akishangiliwa na wengi ambao amefanikiwa kuwashikia akili ilhali ni wawakilishi wa wananchi!

Hili nalo litapita!
Na Mungu mtoa Haki atatenda.
 
Hayo unayasema wewe na wengine humu tunajadili hali halisi. Wanyonge wanaodaiwa kutetewa huku wakiumizwa wengi wao hawana itikadi yoyote. Toka lini MUNGU akawa na chama. Twasema hivi MUNGU ndiye mtetezi wa wanyonge iko siku wote tutalithibitisha hilo.

Hili nalo litapita!
Litadhibitishwa...
 
"Mnyapara wa barabara" yuko kazini, hasikii la yeyote isipokuwa DAB. Eti asema anawapigania 'wanyonge' hata kwa kubomoa Nyumba za hao 'wanyonge'!

Mbaya zaidi mnyapara anafanya udhalimu huku akishangiliwa na wengi ambao amefanikiwa kuwashikia akili ilhali ni wawakilishi wa wananchi!

Hili nalo litapita!
Hivi mwanza vip kuna sehemu kabomoa? Maana nikikumbuka alicho kisema nadhan dodoa hawakumchagua
 
Ccm wanadhani kwasababu watz wengi ni wanyonge basi wanaweza kuwafanya lolote.

Wanasahau kuwa Mwenye kulipa kisasi ni Mungu Mwenyezi pekee!

Mioyo ya wanyonge itaendelea kusikitika na kunung'unika kimya kimya, ila Mungu wa Yakobo atalitukuza Jina lake.
Amen!!
 
Mungu mpenda haki huitazama mioyo na sio maneno yatokayo vinywani........

Vinywani mwa wanasiasa kumejaa maneno ya busara na na unyenyekevu Lakini mioyo yao imejaa usheitwani na ufedhuli wa hali ya juu.....

Ndio hao hao wanaokula viapo bungeni huku wameshika vitabu vya Mungu na upande wa pili wanatenda matendo yanayowaangamiza wengine......
Wanamuektia Baba Mungu!
 
Nawatahadharisha tu, mateso wanayoyapitia watu wa Mungu, kuonewa, kupigwa, kudhulumiwa...mnadhani Mungu amelala na hayaoni mateso wanayopata watu wake?

Tuoneeni tu!! Ila mjue Mungu mtenda haki hajalala.

Mkuu japo nakubaliana na wewe lakini pia naona si vyema kumwachia MUNGU kila kitu ilhali yatokanayo leo ni matunda ya kazi na maamuzi ya binadamu..
Yaani tukosee sisi alafu tumbebeshe MUNGU lawama zote..
Tunapomuomba MUNGU yatupasa kuamka, kupambana na kudai haki za msingi..!
 
Ni kweli mkuu
 
Back
Top Bottom