Tahadhari kwa serikali, machafuko huwa hayaji kwa kupiga kengele. Huanza polepole. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari kwa serikali, machafuko huwa hayaji kwa kupiga kengele. Huanza polepole.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Feb 8, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Machafuko yangekuwa na utaratibu wa kupiga vingo'ola yanapoanza kutokea nchi zilizowahi kukumbwa na ghasia zingekuwa na uwezo wa kujihami mapema. Lakini machafuko huanza polepole japo huwa na dalili ambazo watawala huwa wakizipuuza. Chanzo kikuu cha machafuko ni kero. Kwa mfano, serikali inadharau na kufanya mzaha kuhusu kero na adha kubwa ya wananchi wapatayo kutokana na mgomo wa madaktari. Tahadhari tu kwa serikali, Watanzania wamejaaliwa vipaji vya upole na uvumilivu. Lakini hali ikizidi kuwa mbaya wanaweza kubadilika na kuleta matatizo makubwa. Nyoka aina ya moma unaweza kumkanyaga mara nyingi asikudhuru kwa kuwa ni mpole, lakini akiamua kukugonga mwili wako utaoza mpaka utakapotokwa na uhai. Watawala wetu tafakarini kwa kina migomo hii ya madaktari, msije tafuta mchawi baadaye.
   
Loading...