Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,912
Napenda kuwatahadharisha vijana wa BAVICHA wanaopenda kuenda Dodoma(kama kweli dhamira hiyo ipo) kuwa makini na vijana wanaoambatana nao na hata wale watakaowakuta hapa Dodoma.Epukeni kabisa kuambatana na vijana msiowafahamu vizuri au kubeba vijana mradi tu wako teyari kwenda nanyi Dodoma.Bora mkaenda wachache waaminufu kuliko kundi kubwa lenye mamluku ndani yake.
Ninachokusudia kuwaonya vijana hawa wa BAVICHA ni uwezekano wa kujipenyeza mamluki/mapandikizi miongoni mwenu wenye silaha za jadi n.k, kwa lengo la kuonyesha mnapanga kufanya hujuma/uovu tofauti na ahadu yenu ya kutofanya mambo ya aina hiyo.
Mamluki hao wanaweza kabisa kujisalimisha na wakatoa maelezo ya kipropaganda kuwa walitumwa au walielekezwa kwenda Dodoma kufanya moja mbili tatu.Wanaweza hata kuwataja wasiohusika kwa lengo la kuwachafua.
Msisahau hii ni siasa na namalizia kwa kuwakumbusha msemo maarufu unaosema: "kwenye msafara wa mamba,hata kenge wamo."