Livanga
JF-Expert Member
- Apr 15, 2010
- 469
- 148
Leo asubuhi mzungu mwenye uzoefu na Tanzania aliwasili JKN international Airport akitokea Zanzibar, akaingia kwenye taxi mojawapo ya Taxi za pale air port zenye mstari wa kijani lakini badala yake aliishia kutekwa ndani ya taxi hiyo.
Baada ya kama dakika 30 kwenye taxi wanaume watatu waliingia kwa taxi (hii inaonekana ilikuwa imepangwa kikamilifu) na wakaanza kumzungusha mjini kwa kutumia ATM card yake kuchukua hela kweny bank mbalimbali.
Walimwambia kuwa wao ni wasomali ingawa walikuwa wanaonge kiswahili kizuri sana. Walikuwa ovyo au hawakuwa katika hali ya ustaarabu na walimtishia kwanza kabla hawajaanza mchakato wao, wakamwambia utakuwa salama kama utashirikiana nasi na yeye alitekeleza kama walivyotaka.
kwa mategemea walimuuliza alitaka kushushwa wapi na alipowajibu walimshusha jengo moja kabla ya ofisini kwake, wakamrudishia computer yake na kumwambia "tunajua wewe ni mmarekani kwahiyo unaishi kwa kutegemea computer!" Na alipowaambia kuwa ataweza kuwatrace kwa kutumia iphone yake nayo pia wakamrudishia.
Hawakumfanya lolote la kumuumiza mwili lakini kijasho kilikuwa kimemtoka. KWa sasa yuko kituo cha polisi anaandika maelezo.
Ndugu watanzania wenzangu tunapoelekea mwisho wa mwaka kuweni makini sana na pale airport kama dereva taxi humjui bora umwite unayemjua aje kukuchukua.