TAHADHARI: Kuweni waangalifu na mtu aitwaye LINDA MATIAS kwa watumiao Facebook

webondo

JF-Expert Member
Apr 29, 2012
1,713
382
Habari zenu ndugu zangu.
Naamini wengi ambao tunatumia JF huenda tukawa tunatumia Facebook pia, sasa kwa wale wanaotumia hii social media tafadharini sana kuweni makini na huyu mtu anayejiita LINDA MATIAS. Huyu mtu anapatikana Facebook kwa hilo jina ingawa haifahamiki hasa kama ni Mwanamke kweli au Mwanaume. Anafanya kazi ya kutapeli hasa wanaume. Huwa anaanza kwa kuku-add watu wenye majina ya kiume kwa kutuma "friend request" then baada ya hapo anaanza kuwatongoza au kuanzisha maongezi ya kuwataka kimapenzi. Baada ya hapo anadanganya anataka muonane, kisha anadanganya kuwa hana nauli ili atumiwe nauli afike mahala ulipo, mimi ni mmoja ya watu ambao aliniomba urafiki, means niko katika friends list yake, nikashangaa napigiwa simu na watu watatu tofauti ambao ni rafiki zangu kuniuliza kama namfahamu huyo Linda Matias "nikawajibu simjui ila aliniomba urafiki nikamkubalia means yuko katika orodha ya marafiki zangu" kila mmoja kwa wakati wake akaniambia kuwa amepigwa na huyo mtu, yaani wote wametapeliwa. Waliniuliza kwakuwa wananiona orodha yake pia "mutual friend" ingawa aliponipigia simu rafiki yangu wa pili nikamfahamisha kuwa awe makini na huyo mtu kwanikuna mtu mwingine pia amenipigia. Alipopiga simu mtu wa tatu naye nikamweleza hivyo, nikajua ohhhh kumbe huenda anafanya huo mchezo kwa watu wengi.

Huyo mtu huwa ana-pretend kuwa yeye ni mwanafunzi wa chuo (Mzumbe) anasoma law, lakini hao marafiki zangu wote walishawahi kuongea naye sauti ilikuwa ya mwanamke kweli. Ingawa wanahisi pengine akama ni mtu ambaye yuko hapa dsm au pengine anashirikiana na wanaume. Yeye ukiangalia katika orodha ya marafiki zake almost wote ni wanaume. Nadhani anafanya hivyo akijua itakuwa rahisi kuwanasa wanaume.

Poleni wale ambao mmepigwa na huyo mtu.
 
Kuna mwanamke (au mwanamme sijui) yumo humu JF nasema mwanamke kwa avatar yake na maelezo yake, siku moja alileta nyuzi ya kuwa amechoka kuishi na bwanake kwa mateso aliyoyapata na anataka kuondoka, katika kumpa ushauri kwenye jamvi la wazi, akani pm, na kuanza kunishinikiza nimpe nauli aondoke. Nikamwambia, "koma" kwani nilikupeleka mimi huko? hajani pm tena.

Kuweni makini si fb tu, hawa matapeli hata humu wamo.
 
Mkomage kutongozwa na wanawake. Tena msiowajua. Inachekesha kweli mtu atake muonane yeye hafu akuombe nauli.
 
Hv mwanaume rijali na mwenye akili timamu unaweza tongoza mtu usiemuona? acha waliwe wanaofikiria ngono kila wakati
 
Huu utapeli kwenye hizi social netwaork sasa ni too much kwakweli. Kutongozana kwingi. Naona dunia inafika mwisho sasa
 
duh,kweli.ila fb kunawatapeli wengi sana tu.watu kibao wamelizwa either kutapeliwa pesa na wengine wamekumbwa na majambazi ya mapenzi yaliyoiteka fb.so guys bora kuwa makini maana huwezi jua na wakati mwingine wanatumia very straregic ways kufanikisha,mie kunamtu namfahamu kabisa anahiyo tabia anajidai anfanya kazi abroad kumbe yupo maswa tena vijijini na elimu yake ya kuungaunga.
 
Kuna mwanamke (au mwanamme sijui) yumo humu JF nasema mwanamke kwa avatar yake na maelezo yake, siku moja alileta nyuzi ya kuwa amechoka kuishi na bwanake kwa mateso aliyoyapata na anataka kuondoka, katika kumpa ushauri kwenye jamvi la wazi, akani pm, na kuanza kunishinikiza nimpe nauli aondoke. Nikamwambia, "koma" kwani nilikupeleka mimi huko? hajani pm tena.

Kuweni makini si fb tu, hawa matapeli hata humu wamo.
Pole sana mkuu! Wako wengi sana hawa watu! Kufanya kazi hawataki wao wanapenda kutapeli tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom