Tingitane
Senior Member
- Apr 18, 2012
- 116
- 130
Habari wakuu,
Kuna tatizo la heart failure kwa wanawake wanaojifungua nafikiri tatizo hili linasababisha vifo vya kina mama wengi sana lakini sijui kama mimi ndio nilikuwa silijua au wengi pia hatulifahamu na kwanini elimu juu ya tatizo hili haitolewi wakati wa clinic kwa kinamama.
Iko hivi mwishoni mwa mwezi January kuna rafiki yetu alijaaliwa mtoto sasa tukaamua kwa pamoja tukamtembelee na kumpa hongera kwa kujaaliwa mtoto, hivyo tulienda kama kikundi cha washikaji kwa umoja wetu.
Wakati mazungumzo yanaendelea ndio rafiki zetu waliamua kutuweka wazi kuhusu tatizo lililompata mama wakati anajifungua kuwa kuna maji huwa yanaingia kwenye mapafu pamoja na moyo jambo ambalo lilipelekea moyo kushindwa kufanya kazi vizuri na kujisIkia mchovu sana na kushindwa kupumua akawa anahisi ni uchovu tu wa kujifungua lakini kadri muda ulivyozidi kwenda hali ikazidi kuwa mbaya ndipo alipolazimika kuchukua hatua ya kumpigia Daktari pale Aga Khan kwani ndpko alipojifungulia alipomuelezea Daktari kuhusu hali anayojisikia akamjibu hebu acha unachokifanya uje hapa hospital mara moja.
Dr. hakutaka kumshtua sana lakini baada ya kupata ahueni ndipo alipomwambia ukweli kuwa hali aliyokuwa nayo ni hatari sana na mapigo ya moyo yakishafika chini ya 50 hata moyo wasingeweza kuupump tena ndio ingekuwa mwisho wake.
Washukuriwe Madaktari wa Aga Khan kwa kufaulu kuokoa maisha ya rafiki yetu ijapokuwa amepewa masharti mengi sana ikiwa hakuna kuzaa tena, akafunge tu kizazi na hakuna kutumia uzazi wa mpango wa aina yoyote na hakuna kunyonyesha mtoto (Na tatizo lilitokea ndani ya siku mbili baada ya kujifungua).
Sasa sababu kubwa sana ya mimi kuja hapa katika hili jukwaa ni kutaka watu wengi zaidi wafahamu kuhusu "heart failure during delivery" kwani nimegundua wengi sana wanapoteza maisha pasipo kujua na naomba kama kwenye hili jukwaa kuna Daktari ambaye anaweza kuelezea hili tatizo kwa upana zaidi atusaidie na kama pia kuna uwezekano wa kushare huu ujumbe kwa namna yoyote ili wengi wafahamu naamini wengi wataokolewa.
Ahsante.