TAHADHARI: Kuna matapeli! Fuata taratibu hizi...

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,873
Wakuu,

Penye wengi, pana mengi pia. Jukwaa hili pamoja na kuwa na matangazo mengi, lakini wengine ni matapeli wakubwa sana. Tafadhali, tulishatoa angalizo na tunasisitiza tena:

Mnapoamua kufanya biashara yoyote nje au ndani ya JF bila kutushirikisha msiilaumu JF.

Tunafahamu kuna ambao mmeshalizwa, tafadhali tufahamisheni ili tuweze kuwaanika (tutaanzisha thread maalum kwa ajili ya hili).

Nisisitize, IWENI MAKINI NA MATAPELI!
 
Ninaungana na anayesema kwamba ID za matapeli zitangazwe. lakini pia nafikiri haitatosha. Itapendeza kama tutakwenda mbali zaidi, kwa wale waliotapeliwa kuleta majina kamili ya hao matapeli. Ili baada ya kuwa na ushahidi wa kutosha, majina kamili pamoja na ID zao yatundikwe hapa. Hilo litasaidia si tu wanachama wa JF, bali pia na raia wengine wa mtaani ambao huwa wanatembelea mitandao ya kijamii.
 
wazo hilo zuri sana.maana wengine utapeli uraiani wanauleta na humu.haifai jamani.
 
Ninaungana na anayesema kwamba ID za matapeli zitangazwe. lakini pia nafikiri haitatosha. Itapendeza kama tutakwenda mbali zaidi, kwa wale waliotapeliwa kuleta majina kamili. Ili baada ya kuwa na ushahidi wa kutosha, majina yao kamili yatundikwe hapa. Hilo litasaidia si tu wanachama wa JF, bali pia na raia wengine wa mtaani ambao huwa wanatembelea mitandao ya kijamii.

Labda kutundika majina ya hao matapeli, sidhani kama yule aliyetapeliwa atathubutu kuja kuweka bayana hapa kwamba ametapeliwa kutokana na nature ya tukio lenyewe la ku-tapeliwa kama la aibu vile, unless kuwe na utaratibu mwingine wa kujiweka wazi kwamba umu0hanga wa tatizo hilo.
 
Labda kutundika majina ya hao matapeli, sidhani kama yule aliyetapeliwa atathubutu kuja kuweka bayana hapa kwamba ametapeliwa kutokana na nature ya tukio lenyewe la ku-tapeliwa kama la aibu vile, unless kuwe na utaratibu mwingine wa kujiweka wazi kwamba umu0hanga wa tatizo hilo.
Kweli nilimaanisha majina ya matapeli. Nimeedit post yangu. Nafikiri niliiacha bila ufafanuzi. Thanks for your observation.
 
Kama hawa wenye jf wakitumiwa ujumbe na watu na kuona ID fulani zinalalamikiwa sana basi hapo lazima wao watajua kuwa mtu/watu hao ni lazima kuna cha ukweli as watu hawawezi kuwaota kuripoti.

Mie naona ni wapewe ban ya life na baada ya hapo ID zao ziwekwe wazi, hii itasaidia sana watu kufanya biashara kwa uaminifu na kujua wanaangaliwa na mods.

Mtandao wa internet ni mgumu ila humu ni jukwaaa la wamiliki hivyo wana power zote za kulinda watumiaji. pia mnaweza ruusha kama mtu tapeli anatumie namba za simu kutapeli wengi hii haitakuwa na cha kushangaza ikiwekwa as wengine wataacha pia.

nikisema namba ni kusaidia tu najua watu wanaweza weka usajili majina feki, hyo hata line 10 wanaweza kuwa nazo ila namba wengi waijuijua na itasaidia pia juu ya na ID.

Mods wanauwezo hata waku locate ip add za watu so mkiona mtumiaji ID nyingi tapeli toka pale pale mshughulike.
 
ninaungana na anayesema kwamba id za matapeli zitangazwe. Lakini pia nafikiri haitatosha. Itapendeza kama tutakwenda mbali zaidi, kwa wale waliotapeliwa kuleta majina kamili ya hao matapeli. Ili baada ya kuwa na ushahidi wa kutosha, majina kamili pamoja na id zao yatundikwe hapa. Hilo litasaidia si tu wanachama wa jf, bali pia na raia wengine wa mtaani ambao huwa wanatembelea mitandao ya kijamii.
wasiwasi wangu ni kwamba watu wataanika hata watu ambaosio matapeli bali wanachuki nao binafsi
 
Ni Kweli Kabisa Sasa Ivi Matepeli Wamejaa Kila Mahali .kama Hawa Wanaojifanya Wanganga.sijawahi Kuona Mganga Anajitangazi. Bali Wale Aliowaponya Ndo Wanamtangaza
 
Labda kutundika majina ya hao matapeli, sidhani kama yule aliyetapeliwa atathubutu kuja kuweka bayana hapa kwamba ametapeliwa kutokana na nature ya tukio lenyewe la ku-tapeliwa kama la aibu vile, unless kuwe na utaratibu mwingine wa kujiweka wazi kwamba umu0hanga wa tatizo hilo.

hivi tukio la aibu litakalomzuia mtu kudai haki yake ni lipi?hakuna kipya chini ya jua nitakuja na data za tapeli picha na jina juu ulimwengu utamjua yeye ni mwizi na life itaendelea.hili linaanza lini invisible manake tapeli wangu jukwaa hili na la siasa huwa anashind na kutoa data za kisomi najua tu ameliza wengi
 
Naunga mkono hoja. Kweli humu JF kuna matapeli ingawa siyo wote. Mimi nimenunua sana kupitia JF na karibu mara zote nimeuziwa vitu genuine, kasoro mara moja. Nilinunua the so called universal solar charger for laptops and mobile phones. Muuzaji alimwaga sifa kibao mpaka nikaingia laini. Cha ajabu ni kwamba siyo charger hata kidogo bali ni kama universal battery ya laptops. Baada ya kumweleza matatizo yake muuzaji kakata mawasiliano, ingawa bado yumo JF.

Tujihadhari!!!
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom