Tahadhari: Kuhamisha Fedha za Banks FD kwenda BOT kunaweza kuleta Escrow Season II

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,864
3,851
Kila mtu anakumbuka jinsi fedha za Walipa kodi zilivyokwapuliwa toka Escrow Account pale BOT. Hebu tujiulize haya:-
1. Ni kiasi gani cha fedha kinazalishwa kwa kuweka fedha BOT, zaidi ya kile kinachozalishwa kwa kuweka fedha kwenye Commercial Banks Fixed Deposit Accounts?

2. Je, deposits za Commercial Banks zinakuzwa vipi, ili baadae deposits hizo zitumike kuwakopesha Wakulima, Wafanyakazi na Wafanyabiashara, na baadae kusisimua (Stimulate) shughuli za kiuchumi, kukuza soko la ajira na Serikali kukusanya kodi?

3. Je, ni kwa kiasi gani mapato ya Commercial Banks yataathirika, na kupelekea kupunguza wafanyakazi na kulipa kodi kiduchu?

4. Je, kuna ushahidi usio shaka juu ya kiasi gani cha fedha na kilichotwa na nani, kutoka Fixed Deposit Accounts za hizo Commercial Banks?

5. Je, BOT kuna malaika wasio na tamaa ya kuchukua fedha, na kama wapo, utatuhakikishia vipi kama hii sio mbinu ya wakubwa kuzisogeza fedha karibu ili wazipige kama walivyofanya kwenye Escrow Account?

Haya Maswali yakijibiwa, yatahalalisha uamuzi huo. Vinginevyo kutakuwa na shaka ya kuleta Escrow Season II, ambapo kwenye Season I watu walijibebea fedha kwenye sandarusi, Rambo, lumbesa, mabegi n.k. toka pale pale BOT.

Hayo tu kwa leo.
 
Ordinary level commerce: elucidate the role of central bank. Ref. SA Butt, Essentials of Commerce in East Africa. Majibu yako huko,
 
Mkuu sio kila mtu ana access na hicho material. At least ungeweka hints.
 
Kwa kuongezea nnadhani wengi wengependa kujua je ni sheria ipi na ni kifungu gani cha hiyo sheria inayoruhusu mabenki ya biashara kufungua akaunti maalum (fixed account deposit) kwa mujibu wa Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na hiyo interest inaenda wapi.? Je Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali zinauhusiwa kufungua akaunti maalumu (fixed account deposit) na je kuna matokeo chanya au hasi ya kufungua fixed account deposit.?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom