shaks001
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 1,246
- 1,070
Ujauzito ni baraka na furaha kwa familia lakini huwa unaambatana na changamoto zake kwenye baadhi ya familia.
Jana jioni mke wangu aliniambia ana hamu sana ya soda baridi aina ya Pepsi. Nikatimiza hilo, alikunywa ile soda ikabaki robo chupa akaiweka kwenye friji.Sasa nimerudi usiku kama saa tano hivi nikamkuta amelala, nilivyofungua friji nikasema ngoja niinywe ile soda maana nilikuwa na kiu sana ya soda.
Balaa lilianza pale alipoamka usiku saa 9 anataka kuinywa soda yake akaikosa.Nilipewa dhoruba kali usiku ule ikiambatana na kilio juu; soda yangu, soda yangu.
Nikajifanya jeuri simsikii,kilichofuata ni kuvutwa miguu mpaka nikaamka.
Nikamuomba msamaha anipe mud a mpaka kupambazuke nikamchukulie lkn utetezi wangu haukufua dafu mbele yake.
Akili ya kiume haishindwi kitu nikafikiria fasta nikakumbuka kuna bodaboda flan hivi huwa halali usiku. Nilivyompigia nikampata akaniletea soda lkn bahati mbaya akaleta ya takeaway badala ya chupa ya kawaida.
Likawa balaa lingine haitaki hiyo. Kilichofuata nilikaa nae sitting room mpaka kunakucha ndipo akaniruhusu nikalale.
Ndugu zangu kwa mtiti nilioupata usiku wa kuamkia leo nimekoma kuwachokoza hawa watu. Mjihadhari kuwachokoza yasije wakuta yaliyonikuta mimi.